Friday, October 31, 2014

UMUHIMU WA NDOA

Ungana na AMIR wa jumuiya ABDUL ABUBAKARI katika umuhimu wa ndoa hapa chini inshaallah



AWW,SIFA NJEMA NI ZA ALLAH NA REHMA NA AMANI ZI MSHUKIE KIPENZI CHETU MUHAMMAD  (S.A.W) NA AHLI ZAKE AMA BA’DA.NDUGU ZANGU WAISLAMU NATAKA KUKUMBUSHENI KATIKA NDOA.

Tendo la Ndoa ni Ibada - النّكاح عبادة
Uislamu umenyanyua hadhi ya suala la tendo la ndoa na kulifanya kuwa ni ibada, ibada ambayo wana ndoa wakiifanya hulipwa. Kwani kwa ndoa yao hii ya halali wamejiepusha na maasi na uchafu na wakaishi katika sakafu moja katika mazingira ya kufahamiana, kupendana, kushibana na mahusiano mazuri ya kubadilishana mapenzi yenye kulandana.
Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam)  juu yake amani na salamu anasema:
في بضع أحدكم صدقة
“…na katika kumuingilia mkeo ni sadaka.”(Muslim)
Tendo la ndoa ni sadaka anayotoa mume kwa mkewe, na katika ukamilifu wa neema ni mtu kuhisi kuwa haja zake zinashibishwa na ndipo hapo nafsi inapopata utulivu na malipo ya Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) .
Ibn al-Qayyim (RadhiyaLlahu 'anhu)  anasema: kila ladha husaidia ladha ya siku ya mwisho, ladha hiyo hupendwa na Inaridhiwa na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala)  na mtendaji hupata ladha katika sura mbili:
Upande wa mwanzo ni kule kustarehe na kujifurahisha na kupata utulivu wa macho.
Upande wa pili ni kule kumridhisha Allah (Subhaanahu wa Ta'ala)  na huko ni  kuifikisha nafsi katika daraja la ladha iliyo bora zaidi.
Ndu zangu katika iman na wahimiza vijana(mabarobaro), katika swala zima la ndoa kila mwenye uwezo wa kuoa aoe kwa sababu mtume mtukufu anatutaka kuoa,na Yule ambaye anauwezo wa kuoa na asioe, mtume (s.w.a) ndoa ni katika sunna yangu, mwenye kuacha sunna yangu sio katika sisi.
Eee dada yangu kubali kuolewa,acha kuweka vikwazo vingi visivyo na maana,kubali kusitirika usije ukadhalilika na ukadhalilisha dini yako, mtukufu wa daraja anasema mwanamke anasitirika kwa mambo mawili ima aolewe au azikwe vinginevyo ni mtihani, usidhani kukataa kuolewa umenusurika la hasha ila unatafuta ufisadi katika ardhi.
Kila mwenye mume ALLAH amsitiri na ambaye hana ALLAH awape mume bora na sio bora,na vilele kwa wanume ALLAH awape wanawake wenye sifa nzuri za kichamungu. Wabillahi tawfiq



Monday, October 27, 2014

WANAFUNZI WA KIISLAMU WA CHUO KIKUU CHA TEKU WAKISHEREKEA MAHAFALI YAO YA KUHITIMU

Dada yetu Amirat wa jumuiya pia alikuwepo ukhti Nzitu
 
                     Alikuwepo katibu wetu mstaafu brother Al-Amin akiwa na ukhti Sabrina
            hawa ni baadhi ya wanajumuiya wa msateku waliohitumu elimu yao ya chuo kikuu, ukht Ajuna, Hawa na Sabrina walikuwepo ktk mahafali hayo
Amiri wetu wa jumuiya ya Msateku brother Abdul Abubakari alikuwepo pamoja na mke wake ukhti Sabrina ambaye alikuwa anagraduate