AWW,SIFA NJEMA NI ZA
ALLAH NA REHMA NA AMANI ZI MSHUKIE KIPENZI CHETU MUHAMMAD (S.A.W) NA AHLI ZAKE AMA BA’DA.NDUGU ZANGU
WAISLAMU NATAKA KUKUMBUSHENI KATIKA NDOA.
Tendo la Ndoa ni Ibada
- النّكاح عبادة
Uislamu umenyanyua
hadhi ya suala la tendo la ndoa na kulifanya kuwa ni ibada, ibada ambayo wana
ndoa wakiifanya hulipwa. Kwani kwa ndoa yao hii ya halali wamejiepusha na maasi
na uchafu na wakaishi katika sakafu moja katika mazingira ya kufahamiana,
kupendana, kushibana na mahusiano mazuri ya kubadilishana mapenzi yenye
kulandana.
Mtume (Swalla Llaahu
'alayhi wa sallam) juu yake amani na salamu anasema:
في بضع أحدكم صدقة
“…na katika
kumuingilia mkeo ni sadaka.”(Muslim)
Tendo la ndoa ni
sadaka anayotoa mume kwa mkewe, na katika ukamilifu wa neema ni mtu kuhisi kuwa
haja zake zinashibishwa na ndipo hapo nafsi inapopata utulivu na malipo ya
Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) .
Ibn al-Qayyim
(RadhiyaLlahu 'anhu) anasema: kila ladha husaidia ladha ya siku ya
mwisho, ladha hiyo hupendwa na Inaridhiwa na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala)
na mtendaji hupata ladha katika sura mbili:
Upande wa mwanzo ni
kule kustarehe na kujifurahisha na kupata utulivu wa macho.
Upande wa pili ni kule
kumridhisha Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) na huko ni kuifikisha
nafsi katika daraja la ladha iliyo bora zaidi.
Ndu zangu katika iman
na wahimiza vijana(mabarobaro), katika swala zima la ndoa kila mwenye uwezo wa
kuoa aoe kwa sababu mtume mtukufu anatutaka kuoa,na Yule ambaye anauwezo wa
kuoa na asioe, mtume (s.w.a) ndoa ni katika sunna yangu, mwenye kuacha sunna
yangu sio katika sisi.
Eee dada yangu kubali
kuolewa,acha kuweka vikwazo vingi visivyo na maana,kubali kusitirika usije
ukadhalilika na ukadhalilisha dini yako, mtukufu wa daraja anasema mwanamke
anasitirika kwa mambo mawili ima aolewe au azikwe vinginevyo ni mtihani,
usidhani kukataa kuolewa umenusurika la hasha ila unatafuta ufisadi katika
ardhi.
Kila mwenye mume ALLAH
amsitiri na ambaye hana ALLAH awape mume bora na sio bora,na vilele kwa wanume
ALLAH awape wanawake wenye sifa nzuri za kichamungu. Wabillahi tawfiq
No comments:
Post a Comment