Monday, December 24, 2012

HUKUMU YA KUSHEREKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA WAISLAM


Hukumu Ya Krismasi Na Mwaka Mpya!!!!!!



Shukrani Ziende kwa Allaah
Shaykh al-Islaam bin Taymiyah (Allaah Amrehemu) alisema kwenye fafanuzi yake katika Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Ama kuhusu sherehe za mushrikiyn: wanakusanya pamoja mambo yenye kutia wasiwasi, mahitaji ya mwili na uongo, hakuna chochote ndani yake ambacho kina faida ya kidini, na mwisho wa kutosheleza hizo shahawa, ni maumivu. Hivyo, vitendo vyao ni vya uongo, na kuvishuhudia kunamaanisha kuvifanya. Hii Aayah peke yake inawapandisha daraja na kuwapa moyo (wale ambao hawashuhudii uongo), ambayo ina maana ya kuwahimiza watu kuachana na kushiriki kwenye sherehe zao (mushrikuun) na aina nyenginezo za uongo. Tunafahamu kwamba ni vibaya kushiriki kwenye sherehe zao kwa sababu wanaitwa az-zuur (waongo). Inamaanisha kwamba ni haraam kufanya hivi kwa sababu zilizo nyingi, kwa sababu Allaah Ameiita ni az-zuur.
Allaah Anamlaumu yule anayezungumza uongo (az-zuur) hata ikiwa hamna yeyote atakaeathirika nao, kama ilivyo ndani ya Aayah ikikataza Dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia mkewe “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu”), ambapo Yeye Anasema (tafsiri ya maana):
{{…Wanasema neno baya na la uongo (zuuran)…}} [Al-Mujaadalah 58: 2].
Na Allaah Anasema (tafsiri ya maana):
{{…basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na jiepusheni na usemi wa uongo.}} [Al-Hajj 22:30].
Hivyo yule ambaye anafanya az-zuur analaumiwa kwa mtindo huu. Ndani ya Sunnah:
Anas bin Maalik (Allaah Amrehemu) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja (Madiynah) na walikuta siku mbili ambazo kipindi cha Jaahiliyyah watacheza (na kujipumzisha).” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Allaah Amekupeni kilicho bora zaidi kuliko mambo hayo: Yawm adh-Dhuhaa (‘Iyd al-adh haa) na Yawm al-Fitr (‘Iyd al-Fitr).” [Imesimuliwa na Abuu Daawuud].
Hii inaonesha wazi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya shaka alizuia Ummah wake kusherehekea sherehe za kikafiri, na alihakikisha kuziondosha kwa njia zozote zinazowezekana.
Ukweli wa kwamba dini ya Watu wa Kitabu inakubaliwa, haina maana kwamba sherehe zao zinakubalika au ziendelezwe na Ummah, kama yalivyo matendo yao mengine ya kikafiri yasivyokubalika, na dhambi zao pia hazikubaliki. Hakika, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifikia hadi kuamrisha Ummah wake kujitofautisha nao kwenye mambo mengi ambayo ni mubaah (yanaruhusiwa) na kwa taratibu nyingi za ibada, kwa sababu tu; kwamba vinapelekea kuwa sawa nao kwenye mambo mengine pia. Hii kuweka tofauti; ni kuonesha kizuizi katika nyanja zote, kwa sababu namna utakavyokuwa tofauti na watu wa Motoni, ndivyo utakavyokuwa mchache wa kutenda matendo ya watu wa Motoni.
Ushahidi wa mwanzo ni Hadiyth ya: “Kila watu wana sherehe zao, na hii ndio sherehe yetu” ambayo ina kusudio maalum kwamba; watu wote wana sherehe zao wenyewe, kama Allaah Anavyosema (tafsiri ya maana):
{{Na kila ummah ulikuwa na Qiblah walichokielekea…}} [Al-Baqarah 2: 148]
na
{{Na kila (ummah) katika nyinyi (bin Aadam) Tumeujaalia shari'ah yake na njia yake.}} [Al-Maaidah 5: 48].
Hii inamaanisha kwamba kila taifa lina njia zake wenyewe. Hiyo laam ndani ya li-kulli (“kwa kila”, “katika nyinyi”) ina maana kwa watu maalum. Hivyo, kama Mayahudi wana sherehe na Wakristo wana sherehe, ni za kwao wenyewe, na sisi hatuna sehemu yetu ndani ya hizo sherehe, kama vile tusivyotumia Qiblah kimoja au sheria zao.
Ushahidi wa pili ni: masharti aliyoweka ‘Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kukubaliana pamoja na Swahaabah na Fuqaaha wote baada yao ni: kwa wale Watu wa Kitabu ambao wamekubali kuishi chini ya hukumu za Kiislamu (ahl adh-dhimmah) wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ndani ya Daar al-Islaam (ardhi zilizo chini ya hukumu za Kiislamu). Kama Waislamu wamekubaliana kuwazuia ahl adh-dhimmah kusherehekea wazi wazi, ni namna gani itakuwa sahihi kwa Waislamu kushereheka nao wazi wazi? Kama Muislamu atawasherehekea, jee sio zaidi ya kafiri anavyofanya wazi wazi?
Sababu iliyokuwepo ya sisi kuwazuia wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ni kwa sababu ya machafu yaliyokuwemo humo. Kwa sababu ya dhambi au alama ya dhambi. Katika kesi yoyote, Muislamu anazuiwa kutenda dhambi au kujaribu kutenda dhambi. Hata kama hakuna uadui wowote kwa Muislamu kuwa nao pamoja katika kusherehekea wazi wazi isipokuwa kafiri kupata nguvu ya kuendelea na matendo yake. Inakuwaje Muislamu anatenda hivyo? Uadui uliokuwemo (ndani ya sherehe zao) utaelezwa chini, insha Allaah.
Al-Bayhaqiy amesimulia ikiwa na isnaad swahiyh kwenye Baab karaahiyat ad-dukhuul ‘ala ahl adh-dhimmah fi kanaa’isihim wat-tashabbuh bihim yawmi nawruuzihim wa maharjaanihim (Sura kuhusu karaha ya kuingia kwenye makanisa ya ahl adh-Dhimmah (Makafiri walio katika nchi ya Kiislam)  katika kuadhimisha Mwaka wao Mpya na sherehe nyengine): Kutokana na Sufyaan ath-Thawri na kutokana na Thawr bin Yaziyd na kutokana na ‘Atwa’ bin Diynaar ambao wamesema: ‘Umar amesema: “Musijifunze lugha ya wasiokuwa Waarabu, musiingie pamoja na mushrikiyn kwenye makanisa yao katika siku za karamu zao, kwani laana (za Allaah) zinawashukia juu yao.”
‘Umar bin al-Khattwaab amesema:
“Jiepusheni na maadui wa Allaah kwenye sherehe zao.” Imesimuliwa kutokana na Abuu Usaamah ikiwa na isnaad iliyo sahihi kwamba: ‘Awn alituambia kutokana na Mughiyrah kutokana na ‘Abdullaah bin ‘Amr: “Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.” ‘Umar alikataza kujifunza lugha zao, na hata kuingia kwenye makanisa yao katika siku ya sherehe yao, jee ni vipi kwa kufanya baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye siku hizo, au kufanya vitu ambavyo ni sehemu ya dini yao? Je, sio kufanya baadhi ya vitu wanavyofanya kwenye sherehe zao ni (uovu) zaidi ya kuingia tu kwenye sherehe zao? Kama laana za Muumba zitaanguka juu yao kwenye siku ya sherehe yao kwa sababu ya yale wanayofanya, je, adhabu hiyo haitokuwa sawa kwa yule anayefanya yale wanayotenda wao, au sehemu ya hayo? Je, sio maneno ya: “Jiepusheni na maadui wa Allaah, kwenye sherehe zao” yana maana kwamba tusikutane nao au kushirikiana nao kwenye siku hizi? Je, ni vipi kwa mtu ambaye hakika anasherehekea sherehe zao?
‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kwa uwazi:
“Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.”
Hii inamaanisha kwamba yule anayejikusanya nao kwenye mambo yote haya ni kafiri, au kwamba kufanya hivi ni miongoni mwa dhambi kubwa (kabaa’ir) kwamba itampelekea mmoja wao Motoni; maana ya iliyopita ni ile iliyo wazi kutokana na mpangilio wa maneno. Alitaja – Na Allaah Ndie Ajuaye Zaidi – yule anayeishi kwenye ardhi yao, kwa sababu wakati wa ‘Abdullaah bin ‘Amr na Swahaabah wengineo, walikuwa wakizuia sherehe zilizo wazi za kikafiri ndani ya ardhi za Waislamu. Na hakuna Muislamu aliyewaiga kwenye sherehe zao; hilo (la kusherehekea) pale ambapo wanapoishi kwenye ardhi za kikafiri. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa hata kulitambua jina la sherehe zao ambazo zilikuwa mahsusi kwa ajili yao, je, itakuwaje kwa kushereheka nao kisawasawa? Ahmad ametaja maana ya simulizi zilizopokelewa kutokana na ‘Umar na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwenye mada hii, na wafuasi wake walijadili masuala ya sherehe.
Imaam Abul-Hassan al-‘Aamidiy alisema: mwandishi anayejulikana kwa jina la Ibn al-Baghdaadi alisema ndani ya kitabu chake Umdat al-Haadhwir wa Kifaayat al-Musaafir: “Hairuhusiwi kuingia kwenye sherehe za Wakristo na Mayahudi.” Ahmad alitamka hili kwenye simulizi ya Muhannaa, na ushahidi wake wa hilo ni Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Alisema: (Hizi sherehe ni) ash-Sha’aaniyn pamoja na sherehe zao. Alisema: Waislamu wazuiliwe kuingia kwenye masinagogi (makanisa ya Kiyahudi) na makanisa (ya Wakristo).”
Kutokana na Iqtidhwa’ as-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab al-Jahiym iliyoandikwa na Shaykh al-Islaam bin Taymiyah, uk. 183.
Kuwatakia kheri ya Krismasi Makafiri na hata sikukuu nyengine za dini tofauti ni haraam kwa mujibu wa makubaliano ya wengi, kama Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu) alisema kwenye Ahkaam Ahl adh-Dhimmah.
“Kuwatakia kheri Makafiri katika mwenendo ambao ni kwa ajili yao ni haraam kwa makubaliano ya wengi, kama ilivyo haraam kuwatakia kheri katika sherehe zao na funga zao kwa kusema ‘Kila la kheri katika sherehe’ au ‘Nakutakia sherehe njema’, na mengineyo. Hata kama yule anayesema haya ameepushwa na ukafiri, lakini bado imekatazwa. Ni kama vile kumpa hongera mtu kwa kuuhami msalaba, au zaidi ya hivyo. Ni kama mfano wa dhambi iliyo kubwa sawa na kumpa hongera mnywaji ulevi, au kumuua mtu, au kuwa na mahusiano ya kinyama, na mengineyo. Wengi miongoni mwa wasio na heshima ya dini yao wanaangukia kwenye kosa hili; hawakai kufikiria ubaya wa vitendo vyao. Yeyote anayempa hongera mtu kwa kutovukwa na adabu au bid’ah au ukafiri amejiweka wazi na laana pamoja na ghadhabu za Allaah.”

Kuwapatia hongera makafiri kwenye sherehe za kidini ni haraam kama alivyokwenda mbali Ibn al-Qayyim kwa kufananisha na kwamba yule anayetoa salamu hizo amekubali au ameidhinisha matendo yao ya kikafiri, hata kama mtu hatovifanya mwenyewe vitu hivyo. Lakini Muislamu asikubali mienendo ya kikafiri wala kumpa hongera yeyote kwa ajili yao, kwa sababu Allaah hakubali matendo yoyote kati ya hayo, kama Alivyosema (tafsiri ya maana):

{{Mkikufuru, basi Allaah hana haja nanyi; lakini Haridhii kufuru kwa waja Wake; na kama mkishukuru; hayo Yanamridhisha kwenu.}} [Az-Zumar 39:7].

{{…Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu…}} [Al-Maaidah 5:3].

Hivyo kuwapa pongezi kunazuiwa, hata ikiwa ni mwenzio kazini au vyenginevyo. Kama wao watatutakia kheri kwa kuadhimisha sherehe zao, hatutakiwi kujibu, kwasababu hizi sio sherehe zetu, na kwasababu sio sherehe ambazo zinakubalika na Allaah. Sherehe hizi ni uzushi ndani ya dini zao, na hata zile ambazo zimetajwa huko kabla zimetenguliwa na dini ya Kiislamu, ambayo Ameileta Allaah kwa wanaadamu wetu kupitia kwa bwana Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Anasema (tafsiri ya maana):

{{Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Aakhirah atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa)}} [Aaali-‘Imraan 3:85].

Ni haraam kwa Muislamu kukubali mialiko katika sherehe kama hizo, kwa sababu ni zaidi ya kuwatakia kheri kama inavyoonesha kushiriki katika sherehe zao. Vile vile, Waislamu wanazuiwa kuwaiga makafiri katika kuadhimisha huko kwa kushiriki kwenye tafrija parties, au kwa kubadilishana zawadi, au kutoa peremende au chakula, au kuacha kufanya kazi, n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema “Yeyote anayewaiga watu ni mmoja wao.”

Shaykh al-Islaam bin Taymiyah amesema ndani ya kitabu chake Iqtidhwaa’ asw-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab Al-Jahiym:
“Kuwaiga katika baadhi ya sherehe zao inamaanisha kwamba mtu amefurahia imani zao za uongo na vitendo vyao, na anawapa matumaini kwamba wanaweza kuwa na nafasi ya kuwanyanyasa na kuwapeleka ovyo wanyonge.” Yeyote anayefanya mambo kama haya ni mtenda dhambi, ikiwa anafanya kwa ukarimu au urafiki, au kwa sababu anaona hayaa kukataa, au kwa sababu nyengine yoyote. Kwa sababu ni unafiki ndani ya Uislamu, na kwa sababu inawafanya makafiri kujisikia fakhari kwa dini yao.

Allaah Pekee ndiye tunayemuomba kuwafanya Waislamu kuwa fakhari na dini yao, kuwasaidia kuwa thaabiti katika kushikamana na dini yao, na kuwafanya kuwa washindi dhidi ya maadui zao, kwani Yeye Mwenye Nguvu ndiye Mwenye Kuweza.


Kutoka chapisho la http://www.alhidaaya.com/sw/node/2314

Sasa tunaweza kuweka Commments zetu karibuni wana MSATEKU

As.alaykum wanajumuiya ya MSATEKU..sasa tumerekebisha Blog yetu....kwa kuweka utaratibu wa kuacha Comments zako mara baada ya kupitia taarifa mbalimbali za Jumuiya....Sasa hivi utachotakiwa kufanya ni kuandika Comment yako hapo chini,kwa kwenda sehemu iliyoandikwa NO COMMENTS kama hazipo COMMENTS au kama zipo basi utakuta idadi zake,BOFYA HAPO then andika COMMENT yako  na ubofye sehemu iliyoandikwa Publish then utaletewa Characters ili kuhakikisha kama wewe sio Robots then ziandike kwa kufuata utaraibu wa maneno uliopewa....kama huyaelewi bonyeza nusu duara ili yabadilike na ukiyaona unayaelewa.......kitakachofuata ni kuonekana kwa comment yako,ila nawasihi tuwe wastarabu kwa kutoa comments zenye maadili na kujenga jumuiya yetu na sio kubomoa.....ni vizuri pia ukiandika jina lako ili tufahamiane.....

                                       Karibuni Sana.................

Saturday, December 15, 2012

Maendeleo ya jengo la Mradi wetu

Assalam Alaykum....zifuatazo ni picha mbalimbali za jengo letu la Mradi wa Mgahawa wa kisasa.....pamoja na Msikiti.....angalia mwenyewe tulipofikia mpaka sasa......

 Ujenzi unaendelea.....mapema wiki chache zilizopita...nenda chini ujionee picha za sasa.....





Picha za leo tarehe 15 - 12 - 2012 jioni,hii ni dalili nzuri ya kuwa jengo laendelea vizuri na linataraji kwisha mapema...Alla atufanyie wepesi katika hili.....

PICHA MBALIMBALI ZA SIKUKUU YA IDD AL HAJI KWA WANAJUMUIYA WA MSATEKU

Assalam Alaykum.......leo ndugu Muislam nakuletea picha mbalimbali za matukio ya sherehe za Sikukuu ya IDD Al Haji 2012,ambapo vijana wa MSATEKU walijumuika pamoja kusheherekea,shughuli zilianza asubuhuhi kwa kunywa chai ya pamoja na hadi mchana kwa kula pamoja pia......ama hakika tamaduni hii inazidi kuendelea katika Jumuiya yetu.....Allah atubaliki tuendeleze umoja wetu tuliokuwa nao............karibu ujionee picha hapo chini.......




 Mambo ya Chai hayo na Vijitambi na Maandazii...........karibu tule....
 Chai jamani karibuni........
 Baada ya Chai....vijana walikuwa wankumbushana mambo ya Dini..........na mambo ya kimaisha kiujumla huku wakisubili muda mchana ufikee.

 Amir wa Da`awa akimfuatilia maalim Ahmed.....kuwa anasoma vile inavyotakiwa......huku akitabasamu
 Tafakul baada ya chai......vipi mchana upo hapa jamani......nahisi wanajiuliza......
 Maukht nao walikuwepo kupiga vikombe......

 Baada ya chai vyombo vilioshwa......vijana waliajibika


 Maandalizi ya mchana yalifuata.....mbuzi aliangushwa.........

 Amir wa jumuiya akiwaongoza vijana kuchinja

 Mbuzi amechinjwa....vijana walikuwa madhubuti kuhakikisha Sunnah inatimia......na Mbuzi hakiimbiiiii
 Baada ya maandalizi ya mchana ni mcheleeeee.......shekh tukaribishe bhana......
 Maalim SESEME......peke yako yakhe......ama hakika raha ya mpunga sharti uvalie kilemba......
 Vijana wanaufinya hakika ilikuwa rahaaaaa....
 ulaji wa kisunna pia ulizingatiwa kwa vijana kujumuika pamoja.........hallow msiniwekeee nakula hukuhuku msikitini.......njie endeleeni.......anaovoelekea maalim Ahmed kuongea
Vidume vitatu tu......sahani TANO.......jamani rahaaaaaaa.........msosi ulikuwepo wa kutosha......

Sunday, November 11, 2012

moja ya mada iliyowasilishwa katika semina elekezi ya mwaka wa kwanza (I)


Bismillahir Rahmanir Rahiim:

Brother Amry Jaribu (Msateku - Head Secretary)

I'M PROUD TO BE A MUSLIM:

1:) Islam is the religion of peace

 2:) Islam is the religion of peace and justice

3:) Islam is the religion of peace and tolerance

4:) Islam is the religion of peace and prosperity.

YOUR BROTHER: Amry Jaribu, Don’t forget me in your nice prayers THANKS.

Jumapili,tarehe 11 Novemba, 2012. Assalam alaykum……

Hatuna budi kumshukuru Allah kwa kutupa nguvu na uzima wa kukutana wote hapa katika msikiti wa jumuiya ya MSATEKU kwa lengo la kuambiana mambo mawili,matatu kuhusiana na maisha ya kuwa MWANAFUNZI WA TEKU NA KUJIANDAA ILI KUFAULU VIZURI.Namuomba Allah awapeni usikivu na mie kunipa nguvu ya kuwasilisha mada yangu kwenu,wanafunzi wa mwaka wa kwanza(I) na wengineo………..awali ya wote na nitaanza mada yangu kwa  chachu hizi….

 

 

NAMNA YA KUFELI SHULE KWA MAKUSUDI

1.Usiwe na ratiba ya kujisomea

2.Usiende maktaba kusoma wala kujikumbusha ulivyo soma darasani kwa muda wako wa ziada.

3.Usisome vitabu, wewe soma tu 'summary' za notes na kamusi ili ujue tu maneno magumu ya kuwatishia wengine kua msomi na lugha ina panda kwa sana.

4.Susia vipindi ukijisikia uvivu lala tu wakati wenzio wako darasani au safiri safari ya mbali kula starehe huko

5.Kesha sana kila siku lala saa tisa usiku au kumi kabisa alfajiri wakati shule unatakiwa kuamka saa moja asubuhi kila siku.

6.Nenda club mara nyingi iwezekanavyo kama vipi kila siku
ukiweza.

7.Kuwa mlevi na mwingi wa wanaume/wanawake wakati uko masomoni.

8.Wakati mwalimu anafundisha wewe piga story na rafiki yako na kubadirishana vi memo chini chini vya kuchekesha au cheza game kwe simu au chochote chenye game.

9.Ukipewa mtihani anza kufanya bila kusoma maelekezo kwanza.

10.Kua mtovu wa nidhani na unaye taka ugomvi kila siku na uende darasani ukiwa umelewa(hili si kwa waislamu).

11.Usisome wakati unategemea kufaulu mtihani kwa miujiza.

12.Usisikilize walimu wako au walezi/wazazi hapa TEKU tutawazungumzia Viongozi wa MSATEKU.

13.Uwe mchelewaji kwenda  kwenye vipindi shule na uwahi kuondoka kwenda nyumbani/bwenini

14.Uwe mpenda sifa,mjuaji wa kila kitu, majivuno ya kwenu mna pesa chuo sio ishu.

15.Mwalimu anapo fundisha usichukue notes kaa tu muangalie kama kideo na ongezea kusinzia ikibidi.

16.Usijali GPA au corse works unayopata baada ya mitihani yako 'after all is just a number!!

17.Waambie wenzio 'wametumwa na kijiji kuja kusoma ndio maana wanajituma sana' na wewe kusoma kwako sio ishu sana, after all chuo kikishindikana unaweza kuwa konda wa magari ya''baba/mama,mjomba,shangazi, baba mdogo nk''

18.Ukipewa maswali ya kujibu usifanye yaangalie tu na hisabati soma kama notes usi kokotoe hata moja 'after all ni ugonjwa wa taifa' na kama mmepewa kazi ya kundi wewe usishiriki chochote endelea na mambo yako upate 'marks' za bure

19.Wakatishe wenzio tamaa ''kufauru masomo sio kufauru maisha'; ' wasomi mbona wengi halafu wote choka mbaya tu (kusoma sio dili) au mkubwa afeli bhana……..

20.Ukiwa hujaelewa darasani usiulize kisa utaonekana mjinga.

What DO`s and DON’T`s  (NINI CHA KUFANYA? KUYAEPUKA HAYA YOTE)
10. Pick your major carefully.(yachukulie mambo yako kwa uangalifu na uzito wake) If your university doesn’t make you declare a major off the bat, don’t. Explore new things. Even if you must declare immediately, remember that you can always change your mind. Quiz people in programs you’re considering. Any regrets?
9. If you need help, ask for it. (kama unahitaji msaada,tafadhali omba)If you don’t understand something, ask your leacturer or leader. Many will help you. Another place to find help is the library, where employees can show you how to format your citations or find articles in academic journals. If you’re ever accused of cheating, your student union can help explain your rights.
8. If you’re going to need an extension, ask early. (kama wahitaji ruhusa omba mapema kabla ya kipindi ua ratiba husika haijafikia)If you ask early enough, many lecturer will grant extensions. But don’t annoy your prof by emailing and asking the night before it’s due.
7. Develop a rapport with your leacturer(kuwa na ukaribu au urafiki na Muhadhili wako). Ask questions, contribute to the discussion, stay after class for a minute to clarify something that you don’t understand. In university, you’ll need to make some effort to get noticed.Lecturer who know and like you may help you find jobs, provide references for grad school and will say yes if you ask them to supervise your independent study.
6. Take care of your mental health.(kuwa makini na afya ya ubongo wako) University is stressful, especially if you’re moving away from home for the first time. If you feel anxious or sad, don’t be ashamed to ask your friends for support. There’s also formal counselling from the school. Eating well and exercising can also help greatly.
5. Pick your roommates for second year carefully. (tafuta rafiki kwa makini kwa mwaka wa pili)Think about how you want to live. Your best friend won’t make the best roommate if he or she has different standards of cleanliness, a weird sleep schedule or a higher tolerance for noise. Talk about things like cleaning and splitting bills before you look for housing together. Read up on the laws before you sign a lease.
4. Get involved.(jichanganye/jishughulishe) If you’re in journalism, write for the school paper. If you’re in fine arts, get your work in student-run shows.  If you’re in business, enter case competitions. Participating in degree-related extracurriculars is a great way to network with future colleagues and learn new things.
3. Don’t bring your laptop to class(usiingie na laptop/ipod darasani). Sure, you can type faster than you can write by hand. But Facebook is pretty tempting when it’s in front of you. Plus, when you type your notes, you’re trying to take down every word, which means you’re not really thinking. The secret to success isn’t to take the most notes, but to take the most thoughtful notes. This is easier achieved on paper.
2. Know how to manage your money.(jua namna ya kuudhibiti pesa zako wako) buying prepared food(magengeni) and getting takeout coffee it will impoverish you also may leads you to debt. so learn to cook. Keep track of your spending for a month, to see where you’re overspending.
1. Learn to manage your time(jifunze kujali muda). This is the most important skill for university. Most of your assignments probably won’t be that difficult, but they’ll take longer than anything you’ve done before. Assignments for different classes will often be due at the same time. If you have several essays due in the last week of the semester, you won’t get them all done unless you start early

ways university is not like high school

1. How you write matters.(namna ya kuandika masuala yako) In high school, your teachers were likely happy if you wrote anything at all, and were probably ecstatic if you wrote something clear and gave an opinion or two. That won’t cut it at university. Leacturer expect essays to be formally structured and to provide analysis backed by evidence. They expect papers to be properly formatted, and they expect you to cite sources according to professional style guidelines. Dashing something off at the last minute — no matter how smart you are — won’t cut it.
2. Class is only a quarter of your course.(darasani ni robo ya kozi yako) New university students often make the false assumption that if they attend most of their classes, they are doing the course. But at university, the sitting in class is only a small part of the work. Most of the course is reading the assigned material, doing research for assignments, preparing presentations, meeting with your prof in her office, and writing essays. You should be doing at least three hours of work outside of class for every hour of class time.
3. No one is checking up on you.(hakuna wa kukufuatilia) Unlike high school, no one will come after you or notify your parents if you are falling behind. In fact, in one way, some lecturers like students who don’t do the work because that leaves them with fewer assignments to grade. So, on day one, scour your course outline and figure out how exactly your grade is going to be calculated. Know when things are due and get them done on time. Keep track of everything you hand in and what your current grade is in every course at every point in the year. Avoid unpleasant surprises at the end of term.
4. Expectations are based on the standards of the discipline. (mafanikio yako yanakutegemea nidhamu yako wewe mwenyewe)Your high school teachers have probably been taught that they need to do whatever they can to make sure you have success, even if it means changing what “success” means.  At university, standards tend to be more rigid. You have done well if you have met the standard that your prof thinks is reasonable for a first-year student in that discipline. Whether you did well relative to your own potential is irrelevant. As far as we’re concerned, your personal potential may not be university material.
5. It’s not about you; it’s about the work you do.(sio suala la wewe umefanya nini ila kazi gani umefanya) Many new university students are used to getting credit for “having really tried hard.” But leacturer aren’t grading you or your effort or your sincerity. They are grading the work you do. Many of your professors will never know your name.  If you are at a large university, they may not recognize you in the hallway.
6.Ongea na watu vizuri ili ufanikiwe
7.Waheshimu wenzako
8.Wajali wenyeji wako na hususani viongozi
9.Ishi ni wenzako vizuri hususani wale wa karibu yako mfano waislamu.
10.Jiheshimu mwenyewe kabla ya kuheshimiwa.


NAMNA YA KUJISOMEA VITABU :

Suala la kujifunza kwa kiasi kikubwa linafungamana na kusoma vitabu, kwa hiyo, tumeonelea tuzungumzie suala la kujisomea vitabu  kwa njia ya ufanisi zaidi.
Kwa bahati mbaya wanafunzi wengi tunajisomea vitabu kama wanavyosoma vitabu vya riwaya(hadithi) au visa. Yaani wanaanza kusoma ukurasa wa kwanza na kuendelea kusoma moja kwa moja hadi ukurasa wa mwisho. Wakati kwa hakika hii si njia nzuri ya kusoma vitabu hususani vitabu vya kiada. Kwani vitabu vya kiada vimeandikwa kwa lengo la kufundisha masomo yaliyomo ndani yake. Na vitabu vya kiada vimegawanywa kwa sura.
Na kila sura imegawanywa katika vitengo, na kila kitengo kina anuani yake. Na hii ni tofauti na vitabu vya riwaya(hadithi) ambavyo vimeandikwa kwa mtiririko mmoja kuanzia
mwanzo hadi mwisho.
Kwa hiyo yapasa kuzingatia kuwa anuani za vitabu vya kiada ni nukta muhimu zinazoonesha kitabu kinafundisha nini na katika ukurasa gani. Kwa hiyo, ni jambo zuri kusoma vitabu vya kiada kwa njia maalum kama walivyoibainisha wataalamu.

Njia tuliyoichagua kwa ufipisho inaitwa (KUSUKH), na kirefu chake ni:
• K ----- Kagua:
• U ----- Uliza:
• S ----- Soma:
• U ----- Uliza:
• K ---- Kariri:
• H ---- Hakiki:

Jinsi ya kuitumia njia ya KUSUKH
1. Kagua: Kabla ya kuanza kusoma, tumia dakika mbili tatu kukagua kile utakachosoma. Hapa tunamaanisha kuwa, soma anuani zote za kifungu utakachokisoma.
Pia hakikisha unasoma muhtasari wa kifungu hicho kama upo. Vilevile soma maswali ya kujikumbusha yaliyoambatanishwa na kifungu hicho kama yapo. Faida ya kufanya hivyo ni kupata fikra ya kile utakachokisoma. Kumbuka faida za kukagua kitu kabla ya kukitumia.
2. Uliza:
Baada ya kukagua, hatua inayofuata ni kuunda maswali ya kukusaidia kusoma kwa ufanisi. Na namna ya kuunda hayo maswali ni kama ifuatavyo: Geuza kila anuani iwe swali. Unaweza kuuliza kwa kutumia maneno yafuatayo: Vipi, lini, wapi, nani, inahusu nini, inafanya nini, muda gain nk. Kwa hakika ukibadilisha anuani na kuzifanya kuwa maswali, hilo linakusaidia kutambua wataka kufanya nini na kwa wakati gani.

3. Soma: Hatua ya tatu unatakiwa usome kwa makini kifungu chote ili upate majibu ya yale maswali uliojiuliza katika hatua ya pili.Hapa tuwe karibu na matumizi ya karamu na karatasi.Ili kuchukua mambo muhimu.

4. Uliza:
Baada ya kusoma, unda maswali mengine yanayohusiana na ufafanuzi uliotolewa katika kifungu. Kwa hakika maswali yanakupa changamoto za kufahamu na kukumbuka kile ulichokisoma.

5. Kariri
: Katika hatua hii, unatakiwa uyarudie yale maswali uliyoyatengeneza pamoja na majibu yake uliyoyapata katika kusoma kifungu husika. Yaani soma maneno yale yale kimoyomoyo au kwa sauti au fanya vitendo vile vile mara kwa mara, rudia rudia.
Ni vizuri kuandika kwa ufupi maswali na majibu ya kifungu husika, kwani imethibitika kuwa kuandika kunasaidia kufanya mtu ashike vizuri zaidi kile alichokisoma au kukisikia. Pia waweza kutumia maandishi hayo kwa kujiandaa na mtihani yakiwa ndio ufupisho.
6. Hakiki: Hatua ya mwisho ni kufanya uhakiki wa kile ulichojifunza kwa njia ya kusoma. soma maandishi kwa kuyachambua na kufafanua mambo mbalimbali yaliyomo. Funika kitabu na karatasi ya majibu, kisha jiulize yale maswali ya kifungu cha pili, na jaribu kujipima je, unaweza kuyajibu? Kama jibu ni ndio hongera, hata hivyo soma tena katika kitabu ili kuhakikisha kweli umejibu sahihi. Kama jibu ni hapana bado una nafasi, rejea kusoma kurasa za majibu yako na kitabu ili kujiimarisha.


VIDOKEZO KATIKA KUTUMIA NJIA YA KUSUKH.
1. Tumia akili katika kuunda maswali, jiulize maswali ya msingi sio mzaha mzaha, uliza maswali, kabla na baada ya kusoma.
2. Uliza maswali ya kifungu chote.
3. Kabla hujaanza kuandika majibu ya maswali uliyojiuliza, hakikisha umeshasoma kifungu chote.
4. Andika kwa kutumia maneno yako, yaani kwa ufahamu wako. Pia fanya vifupisho kwa mtindo utakaouonelea kuwa unakufaa.
5. Usijihangaishe kwa kuandika majibu marefu, bora kuandika maneno mawili matatu yanayokukumbusha tu, kwani wewe hurudii kuandika kitabu!
6. Kumbuka kuwa hayo majibu na ufupisho ni wako, kwa hiyo usihofu kuwa watu wengine hawatoufahamu.

KUSOMA KWA MAKUNDI
What is Group Discussion ?
A group discussion is simply a method instrumental in judging the team spirit, leadership qualities, out of the box thinking, and other managerial qualities in an individual. In a layman’s language, a group discussion is a discussion involving a group of around seven to eight participants.
Do you think an individual can work alone and produce results in an organization ?
The answer is No. Every individual works in a team and has to rely on his fellow workers for his easy working and better output. He has to be a good team player to make his mark in the ever challenging corporate world.

Here are Some Tips for a Successful Group Discussion(namna ya kutengenezakundi la mafanikio katika kusoma)
  • The first and the foremost tip for an individual to perform well in a GD is to learn the art of participation.(jifunze tabia ya kushiriki) Don’t expect others to force you to speak. Take the initiative, participate in the discussion and share your ideas with others. Never shout in a group discussion and always wait for your turn to speak. Remember it’s a discussion, not a fighting ground. Be polite but firm.
  • Try to take the initiative.(kuwa wa mwanzo kuanza kujadili hoja) Don’t wait for the others to start the discussion. Always volunteer yourself and start the discussions in an extremely confident manner. Introduce yourself and your team members and then start with the topic but one thing to remember here is that one must initiate the Group Discussion only when he or she is well versed with the topic. Don’t take the risk if you yourself are not very clear about your thoughts.
  • A leader is the one who actually gives the group discussion a direction and guides other team members when they seem to be lost or confused. Like a true leader, an individual must try his level best to refrain from personal favours. Don’t only ask your acquaintance to speak, give equal opportunity to other participants as well. As the leader of the group, he must ensure that the discussion does not end up in fighting and reaches a conclusion.
  • One must speak only if he is well prepared with the topic. (mtu azungumze kwa kujua nini anazungumza yani awe amejiandaa na mada au kinachojadiliwa)Don’t just speak for the sake of points or marks; speak only when you are absolutely sure about what you are speaking. Never depend on guess works in group discussions as it sometimes can seriously go against you. Avoid using slangs or crack jokes in between the discussions as it is considered highly unprofessional.
  • Never be rigid in group discussions.(usiwe mbishi jitahidi kubadilika) Always keep in mind that the other person is also as learned as you. Always listen to what he is saying and then only respond. Be a good and a patient listener. Don’t just simply draw conclusions as there is always a room for discussions. Debate logically and sensibly and try to take everyone along with you.
  • Read a lot and always keep your eyes and ears open.(kuwa makini na usiwe mtu wa kuuliza maswali hovyo) Always begin your day with the newspaper and know what is happening around you. An individual must be aware of the current events to succeed well in a group discussion.
  • Be alert always.(kuwa makini na unachokijadili na kuwa mwangalifu na tabia yako yaani jitambue) A participant usually gets around 15 minutes to think about the topic. You need to think fast and cover as much as you can. Always take care of your words. The content has to be sensible, crisp and well supported with examples or real life situations. Don’t adopt a laidback attitude or yawn in between group discussions.
  • Take care of your dressing as well.(kuwa makini na muangalifu na mavazi yako) Don’t wear flashy(zinazong`aa) clothes while going for a group discussion or interview. Female candidates should also avoid cakey makeup or flaunt heavy jewellery. The clattering sounds of bangles sometimes act as a disturbing element in formal discussions. Be in professional attire and avoid loud colours.
  • An individual must keep in his mind that group discussion is meant for bringing out the managerial skills of an individual. The organizer of the group discussion will never appreciate you or give you the credit if you shout or fight in group discussions. Be calm, composed, confident and neutral to create an impression in the discussion and win over others.

 

Do's and Dont's in a Group Discussion(Nini cha kufanya na kisifanywe katika kundi la majadiliano)

When you are participating in a group discussion, there are a number of things you will want to avoid. While doing the right things can allow you to become a valuable member of the group, doing the wrong things can cause you to disrupt the discussion, and you may find yourself alienated from the other members.
In this article, I will go over the Do's and Dont's of group discussions. By following these guidelines, you will enjoy being a part of group discussions, and you will contribute to the success of the group.

It is important to avoid putting down the ideas that are presented during the discussion.(epuka kuweka kapuni au kudhalau vitu vinavyojadiliwa ) This is especially important if the group is brainstorming ideas. When you put down ideas that are presented by someone else, you are humiliating them in front of the other members, and you are disrupting the brainstorming process. In addition to this, you can create conflict between you and the person you are ridiculing. Never attack the idea of someone else. It can cause other members to be uneasy about sharing their own ideas, because they may fear being ridiculed.

If you don't agree with a statement or idea that has been presented by other another member, address the issue in a polite manner.(kama hujakubaliana na jambo linajadiliwa liwasilishe kwa nidhamu) Instead of attacking their idea directly, why not come up with a better idea instead? It is also important avoid interrupting other members when they are speaking. This is extremely rude. If you feel the need to interrupt someone while they are speaking, try to interject as politely as you can. In some discussion groups, you may be required to raise your hands after someone has finished making a statement. If someone is interrupted by another person why they are speaking, this could create conflict. It may convey a message that what they are saying is not important.

When you are given a task to carry out, it is important for you to do it.(shiriki kufanya kazi ya kikundi) Remember, the group is a machine, and every part of that machine must work if it is to function properly. The members of the group are the pieces that make up the machine. If you are given a task to perform that must be done before the discussion is held, you will want to make sure it is done properly. If it is not done correctly, it can disrupt the flow of the discussion. It is important for you to offer encouragement to the other members. When you encourage the other members of the group, you will gain their respect, and this will allow them to work harder. Encouragement can build up a group discussion, while discouragement can tear it down.

It is important for you to show respect to all the members of the group, and they should show you respect as well.(jiheshimu na utaheshimiwa)When everyone has a mutual respect for each other, this will stop the conflicts which can completely destroy a discussion. If you are the leader of the group, it is essential for you to make sure the right topic is discussed. It should be something that is important to you and the other members. When this is case, the participants will work hard to make sure important issues are covered. If they are not interested in the topic, it will be hard to get them to focus on it. It is important for leaders to choose relevant topics that will be of interest to those who will be participating.

If you are having a brainstorming phase during the group discussion, do not dismiss any ideas that are presented. Give everyone the time to present ideas that they think can be useful in solving problems. Once the brainstorming session is over, let the group decide which ideas are the best.
Another thing that you will want to avoid doing is avoid getting into arguments with other members.(epuka migogoro) It is not productive, and will cause conflicts to occur. While there is nothing wrong with getting into positive arguments, they should not be allowed to get out of control. Show respect to everyone in the group. If you don't agree with a statement that is made by someone, say it in a tactful way.

NAMNA YA KUTENGENEZA GPA

What is a Grade Point Average (GPA)?


 Your Grade Point Average (GPA) is a measure of how well you are doing in your academic studies. At TEKU the academic grading scale goes from “A” to “D”, with corresponding grade points ranging from the highest “5” to the lowest “2”.  A student’s Grade Point Average, or GPA, is a mathematical calculation that indicates where an average of the grades falls on the scale.

Academic/Career/Developmental Programs
Letter Grade
Numerical Grade
Grade Points
Letter Grade Description
A

100-70
5


Excellent.  First Class Standing.  Superior Performance showing comprehensive, in-depth understanding of subject matter.   Demonstrates initiative and fluency of expression.
B+

69-60
4
Very Good.  Second Class Standing.  Clearly above average performance with knowledge of principles and facts generally complete and with no serious deficiencies.
B
59-50
3
Satisfactory or(Good) , Basic understanding with knowledge of principles and facts at least adequate to communicate intelligently in the discipline.
C
40-49
2
Pass.  Some understanding of principles and facts but with definite deficiencies.
D
39-35
1
Minimal Pass( Fail/Supplemantery),A passing grade indicating marginal performance.  Student not likely to succeed in subsequent courses in the subject.
E
 34-0
0
Unsatisfactory (Fail and Exclude), Knowledge of principles and facts is fragmentary; or student has failed to complete substantive course requirements.

2. What is a term grade point average (TERM GPA)?

Your term GPA is the average of your grades for only one semester.
For example, if a student earns grades of “A-“ in all courses, he or she would
have a TERM GPA of 3.67. A GPA of 3.67 or higher, is regarded as first Class Standing
.

How to calculate GPA:
Total of points over Total of Credits = GPA
Ili kuifanya GPA iwe nzuri,tuwe makini na kufanya vizuri kwa masomo yenye CRDTs kubwa mfano crdt 3 kuliko lile lenye CRDTs ndogo,lakini haina maana tuyapuuze yale yenye CRDTs ndogo,yatuongezea idadi ya points pia.Kwa mfano somo lenye CRDTs 3 ukipata A (yaani Grade 5) utakuwa umepata points 15 kuliko somo lenye CRDTs 2 ungepata A (yaani Grade 5) utakuwa umepata points 10.


Kwahiyo tujitahidi kukazania masomo yenye points nyingi kwa ufaulu mzuri. “So let us maintain our Course works”ili kuepuka madhara ya kuharibu GPA yetu.Kwasababu sheria ya TEKU below GPA 1.8 is reapeting a year and not “a DISCO” that is dis-qualified.
Therefore:
First Class
An overall average of 4.4 or higher
 
Upper Second
An overall average in the range of 3.5 – 4.3
 
Lower Second
An overall average in the range of 2.7 – 3.4
 
Pass degree
An overall average of between 2.0 and 2.6

                                                   Wabillah Taufiq..