Hukumu Ya Krismasi Na Mwaka Mpya!!!!!!
Shukrani Ziende kwa Allaah
Shaykh al-Islaam bin Taymiyah (Allaah Amrehemu)
alisema kwenye fafanuzi yake katika Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Ama kuhusu sherehe za mushrikiyn:
wanakusanya pamoja mambo yenye kutia wasiwasi, mahitaji ya mwili na uongo,
hakuna chochote ndani yake ambacho kina faida ya kidini, na mwisho wa
kutosheleza hizo shahawa, ni maumivu. Hivyo, vitendo vyao ni vya uongo, na
kuvishuhudia kunamaanisha kuvifanya. Hii Aayah peke yake inawapandisha daraja
na kuwapa moyo (wale ambao hawashuhudii uongo), ambayo ina maana ya kuwahimiza
watu kuachana na kushiriki kwenye sherehe zao (mushrikuun) na aina nyenginezo
za uongo. Tunafahamu kwamba ni vibaya kushiriki kwenye sherehe zao kwa sababu
wanaitwa az-zuur (waongo). Inamaanisha kwamba ni haraam kufanya hivi kwa sababu
zilizo nyingi, kwa sababu Allaah Ameiita ni az-zuur.
Allaah Anamlaumu yule
anayezungumza uongo (az-zuur) hata ikiwa hamna yeyote atakaeathirika nao, kama
ilivyo ndani ya Aayah ikikataza Dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia
mkewe “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu”), ambapo Yeye Anasema (tafsiri
ya maana):
{{…Wanasema neno baya na la uongo (zuuran)…}} [Al-Mujaadalah
58: 2].
Na Allaah Anasema (tafsiri ya maana):
{{…basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na jiepusheni
na usemi wa uongo.}} [Al-Hajj 22:30].
Hivyo yule ambaye anafanya az-zuur analaumiwa kwa
mtindo huu. Ndani ya Sunnah:
Anas bin Maalik (Allaah Amrehemu)
amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja
(Madiynah) na walikuta siku mbili ambazo kipindi cha Jaahiliyyah watacheza (na
kujipumzisha).” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
akasema: “Allaah Amekupeni kilicho bora zaidi kuliko mambo hayo: Yawm
adh-Dhuhaa (‘Iyd al-adh haa) na Yawm al-Fitr (‘Iyd al-Fitr).” [Imesimuliwa na
Abuu Daawuud].
Hii inaonesha wazi kwamba Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya shaka alizuia Ummah wake
kusherehekea sherehe za kikafiri, na alihakikisha kuziondosha kwa njia zozote
zinazowezekana.
Ukweli wa kwamba dini ya Watu wa
Kitabu inakubaliwa, haina maana kwamba sherehe zao zinakubalika au ziendelezwe
na Ummah, kama yalivyo matendo yao mengine ya kikafiri yasivyokubalika, na
dhambi zao pia hazikubaliki. Hakika, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) alifikia hadi kuamrisha Ummah wake kujitofautisha nao kwenye mambo
mengi ambayo ni mubaah (yanaruhusiwa) na kwa taratibu nyingi za ibada, kwa
sababu tu; kwamba vinapelekea kuwa sawa nao kwenye mambo mengine pia. Hii
kuweka tofauti; ni kuonesha kizuizi katika nyanja zote, kwa sababu namna
utakavyokuwa tofauti na watu wa Motoni, ndivyo utakavyokuwa mchache wa kutenda matendo
ya watu wa Motoni.
Ushahidi wa mwanzo ni Hadiyth ya:
“Kila watu wana sherehe zao, na hii ndio sherehe yetu” ambayo ina kusudio
maalum kwamba; watu wote wana sherehe zao wenyewe, kama Allaah Anavyosema
(tafsiri ya maana):
{{Na kila ummah ulikuwa na Qiblah walichokielekea…}}
[Al-Baqarah 2: 148]
na
{{Na kila (ummah) katika nyinyi
(bin Aadam) Tumeujaalia shari'ah yake na njia yake.}} [Al-Maaidah 5: 48].
Hii inamaanisha kwamba kila taifa
lina njia zake wenyewe. Hiyo laam ndani ya li-kulli (“kwa kila”, “katika
nyinyi”) ina maana kwa watu maalum. Hivyo, kama Mayahudi wana sherehe na
Wakristo wana sherehe, ni za kwao wenyewe, na sisi hatuna sehemu yetu ndani ya
hizo sherehe, kama vile tusivyotumia Qiblah kimoja au sheria zao.
Ushahidi wa pili ni: masharti aliyoweka
‘Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kukubaliana pamoja na
Swahaabah na Fuqaaha wote baada yao ni: kwa wale Watu wa Kitabu ambao
wamekubali kuishi chini ya hukumu za Kiislamu (ahl adh-dhimmah) wasisherehekee
sherehe zao wazi wazi ndani ya Daar al-Islaam (ardhi zilizo chini ya hukumu za
Kiislamu). Kama Waislamu wamekubaliana kuwazuia ahl adh-dhimmah kusherehekea
wazi wazi, ni namna gani itakuwa sahihi kwa Waislamu kushereheka nao wazi wazi?
Kama Muislamu atawasherehekea, jee sio zaidi ya kafiri anavyofanya wazi wazi?
Sababu iliyokuwepo ya sisi
kuwazuia wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ni kwa sababu ya machafu
yaliyokuwemo humo. Kwa sababu ya dhambi au alama ya dhambi. Katika kesi yoyote,
Muislamu anazuiwa kutenda dhambi au kujaribu kutenda dhambi. Hata kama hakuna
uadui wowote kwa Muislamu kuwa nao pamoja katika kusherehekea wazi wazi
isipokuwa kafiri kupata nguvu ya kuendelea na matendo yake. Inakuwaje Muislamu
anatenda hivyo? Uadui uliokuwemo (ndani ya sherehe zao) utaelezwa chini, insha
Allaah.
Al-Bayhaqiy amesimulia ikiwa na
isnaad swahiyh kwenye Baab karaahiyat
ad-dukhuul ‘ala ahl adh-dhimmah fi kanaa’isihim wat-tashabbuh bihim yawmi
nawruuzihim wa maharjaanihim (Sura kuhusu karaha ya kuingia kwenye makanisa ya
ahl adh-Dhimmah (Makafiri walio katika nchi ya Kiislam) katika kuadhimisha Mwaka wao Mpya na sherehe
nyengine): Kutokana na Sufyaan ath-Thawri na kutokana na Thawr bin Yaziyd na
kutokana na ‘Atwa’ bin Diynaar ambao wamesema: ‘Umar amesema: “Musijifunze
lugha ya wasiokuwa Waarabu, musiingie pamoja na mushrikiyn kwenye makanisa yao
katika siku za karamu zao, kwani laana (za Allaah) zinawashukia juu yao.”
‘Umar bin al-Khattwaab amesema:
“Jiepusheni na maadui wa Allaah
kwenye sherehe zao.” Imesimuliwa kutokana na Abuu Usaamah ikiwa na isnaad iliyo
sahihi kwamba: ‘Awn alituambia kutokana na Mughiyrah kutokana na ‘Abdullaah bin
‘Amr: “Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea
Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali
hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.” ‘Umar alikataza kujifunza
lugha zao, na hata kuingia kwenye makanisa yao katika siku ya sherehe yao, jee
ni vipi kwa kufanya baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye siku hizo, au kufanya
vitu ambavyo ni sehemu ya dini yao? Je, sio kufanya baadhi ya vitu wanavyofanya
kwenye sherehe zao ni (uovu) zaidi ya kuingia tu kwenye sherehe zao? Kama laana
za Muumba zitaanguka juu yao kwenye siku ya sherehe yao kwa sababu ya yale
wanayofanya, je, adhabu hiyo haitokuwa sawa kwa yule anayefanya yale
wanayotenda wao, au sehemu ya hayo? Je, sio maneno ya: “Jiepusheni na maadui wa
Allaah, kwenye sherehe zao” yana maana kwamba tusikutane nao au kushirikiana
nao kwenye siku hizi? Je, ni vipi kwa mtu ambaye hakika anasherehekea sherehe
zao?
‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kwa uwazi:
“Yeyote anayeishi ndani ya ardhi
ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na
kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao
kwenye Siku ya Malipo.”
Hii inamaanisha kwamba yule
anayejikusanya nao kwenye mambo yote haya ni kafiri, au kwamba kufanya hivi ni
miongoni mwa dhambi kubwa (kabaa’ir) kwamba itampelekea mmoja wao Motoni; maana
ya iliyopita ni ile iliyo wazi kutokana na mpangilio wa maneno. Alitaja – Na
Allaah Ndie Ajuaye Zaidi – yule anayeishi kwenye ardhi yao, kwa sababu wakati
wa ‘Abdullaah bin ‘Amr na Swahaabah wengineo, walikuwa wakizuia sherehe zilizo
wazi za kikafiri ndani ya ardhi za Waislamu. Na hakuna Muislamu aliyewaiga
kwenye sherehe zao; hilo (la kusherehekea) pale ambapo wanapoishi kwenye ardhi
za kikafiri. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa hata kulitambua jina la
sherehe zao ambazo zilikuwa mahsusi kwa ajili yao, je, itakuwaje kwa
kushereheka nao kisawasawa? Ahmad ametaja maana ya simulizi zilizopokelewa
kutokana na ‘Umar na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwenye mada hii, na
wafuasi wake walijadili masuala ya sherehe.
Imaam Abul-Hassan al-‘Aamidiy
alisema: mwandishi anayejulikana kwa jina la Ibn al-Baghdaadi alisema ndani ya
kitabu chake Umdat al-Haadhwir wa
Kifaayat al-Musaafir: “Hairuhusiwi kuingia kwenye sherehe za Wakristo na
Mayahudi.” Ahmad alitamka hili kwenye simulizi ya Muhannaa, na ushahidi wake wa
hilo ni Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii
shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Alisema: (Hizi sherehe ni)
ash-Sha’aaniyn pamoja na sherehe zao. Alisema: Waislamu wazuiliwe kuingia
kwenye masinagogi (makanisa ya Kiyahudi) na makanisa (ya Wakristo).”
Kutokana na Iqtidhwa’ as-Swiraat al-Mustaqiym
Mukhaalifat Aswhaab al-Jahiym iliyoandikwa na Shaykh al-Islaam bin Taymiyah,
uk. 183.
Kuwatakia kheri ya Krismasi
Makafiri na hata sikukuu nyengine za dini tofauti ni haraam kwa mujibu wa
makubaliano ya wengi, kama Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu) alisema kwenye
Ahkaam Ahl adh-Dhimmah.
“Kuwatakia kheri Makafiri katika
mwenendo ambao ni kwa ajili yao ni haraam kwa makubaliano ya wengi, kama ilivyo
haraam kuwatakia kheri katika sherehe zao na funga zao kwa kusema ‘Kila la
kheri katika sherehe’ au ‘Nakutakia sherehe njema’, na mengineyo. Hata kama
yule anayesema haya ameepushwa na ukafiri, lakini bado imekatazwa. Ni kama vile
kumpa hongera mtu kwa kuuhami msalaba, au zaidi ya hivyo. Ni kama mfano wa
dhambi iliyo kubwa sawa na kumpa hongera mnywaji ulevi, au kumuua mtu, au kuwa
na mahusiano ya kinyama, na mengineyo. Wengi miongoni mwa wasio na heshima ya
dini yao wanaangukia kwenye kosa hili; hawakai kufikiria ubaya wa vitendo vyao.
Yeyote anayempa hongera mtu kwa kutovukwa na adabu au bid’ah au ukafiri
amejiweka wazi na laana pamoja na ghadhabu za Allaah.”
Kuwapatia hongera makafiri kwenye
sherehe za kidini ni haraam kama alivyokwenda mbali Ibn al-Qayyim kwa
kufananisha na kwamba yule anayetoa salamu hizo amekubali au ameidhinisha
matendo yao ya kikafiri, hata kama mtu hatovifanya mwenyewe vitu hivyo. Lakini
Muislamu asikubali mienendo ya kikafiri wala kumpa hongera yeyote kwa ajili
yao, kwa sababu Allaah hakubali matendo yoyote kati ya hayo, kama Alivyosema
(tafsiri ya maana):
{{Mkikufuru, basi Allaah
hana haja nanyi; lakini Haridhii kufuru kwa waja Wake; na kama mkishukuru; hayo
Yanamridhisha kwenu.}} [Az-Zumar 39:7].
{{…Leo nimekukamilishieni Dini
yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini
yenu…}} [Al-Maaidah 5:3].
Hivyo kuwapa pongezi
kunazuiwa, hata ikiwa ni mwenzio kazini au vyenginevyo. Kama wao watatutakia
kheri kwa kuadhimisha sherehe zao, hatutakiwi kujibu, kwasababu hizi sio
sherehe zetu, na kwasababu sio sherehe ambazo zinakubalika na Allaah. Sherehe
hizi ni uzushi ndani ya dini zao, na hata zile ambazo zimetajwa huko kabla
zimetenguliwa na dini ya Kiislamu, ambayo Ameileta Allaah kwa wanaadamu wetu
kupitia kwa bwana Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah
Anasema (tafsiri ya maana):
{{Na anayetaka dini isiyokuwa ya
Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Aakhirah atakuwa katika wenye khasara
(kubwa kabisa)}} [Aaali-‘Imraan 3:85].
Ni haraam kwa Muislamu kukubali
mialiko katika sherehe kama hizo, kwa sababu ni zaidi ya kuwatakia kheri kama
inavyoonesha kushiriki katika sherehe zao. Vile vile, Waislamu wanazuiwa
kuwaiga makafiri katika kuadhimisha huko kwa kushiriki kwenye tafrija parties,
au kwa kubadilishana zawadi, au kutoa peremende au chakula, au kuacha kufanya
kazi, n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alisema “Yeyote anayewaiga watu ni mmoja wao.”
Shaykh al-Islaam bin Taymiyah
amesema ndani ya kitabu chake Iqtidhwaa’ asw-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat
Aswhaab Al-Jahiym:
“Kuwaiga katika baadhi ya sherehe
zao inamaanisha kwamba mtu amefurahia imani zao za uongo na vitendo vyao, na
anawapa matumaini kwamba wanaweza kuwa na nafasi ya kuwanyanyasa na kuwapeleka
ovyo wanyonge.” Yeyote anayefanya mambo kama haya ni mtenda dhambi, ikiwa
anafanya kwa ukarimu au urafiki, au kwa sababu anaona hayaa kukataa, au kwa
sababu nyengine yoyote. Kwa sababu ni unafiki ndani ya Uislamu, na kwa sababu
inawafanya makafiri kujisikia fakhari kwa dini yao.
Allaah Pekee ndiye tunayemuomba
kuwafanya Waislamu kuwa fakhari na dini yao, kuwasaidia kuwa thaabiti katika
kushikamana na dini yao, na kuwafanya kuwa washindi dhidi ya maadui zao, kwani
Yeye Mwenye Nguvu ndiye Mwenye Kuweza.
Kutoka
chapisho la http://www.alhidaaya.com/sw/node/2314
Shukrani viongozi wetu kwa kutujali na kutuwekea mawaidha mazuri,Allah atawalipa inshallah Amin.
ReplyDelete