Monday, December 24, 2012

HUKUMU YA KUSHEREKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA WAISLAM


Hukumu Ya Krismasi Na Mwaka Mpya!!!!!!



Shukrani Ziende kwa Allaah
Shaykh al-Islaam bin Taymiyah (Allaah Amrehemu) alisema kwenye fafanuzi yake katika Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Ama kuhusu sherehe za mushrikiyn: wanakusanya pamoja mambo yenye kutia wasiwasi, mahitaji ya mwili na uongo, hakuna chochote ndani yake ambacho kina faida ya kidini, na mwisho wa kutosheleza hizo shahawa, ni maumivu. Hivyo, vitendo vyao ni vya uongo, na kuvishuhudia kunamaanisha kuvifanya. Hii Aayah peke yake inawapandisha daraja na kuwapa moyo (wale ambao hawashuhudii uongo), ambayo ina maana ya kuwahimiza watu kuachana na kushiriki kwenye sherehe zao (mushrikuun) na aina nyenginezo za uongo. Tunafahamu kwamba ni vibaya kushiriki kwenye sherehe zao kwa sababu wanaitwa az-zuur (waongo). Inamaanisha kwamba ni haraam kufanya hivi kwa sababu zilizo nyingi, kwa sababu Allaah Ameiita ni az-zuur.
Allaah Anamlaumu yule anayezungumza uongo (az-zuur) hata ikiwa hamna yeyote atakaeathirika nao, kama ilivyo ndani ya Aayah ikikataza Dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia mkewe “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu”), ambapo Yeye Anasema (tafsiri ya maana):
{{…Wanasema neno baya na la uongo (zuuran)…}} [Al-Mujaadalah 58: 2].
Na Allaah Anasema (tafsiri ya maana):
{{…basi jiepusheni na uchafu wa masanamu na jiepusheni na usemi wa uongo.}} [Al-Hajj 22:30].
Hivyo yule ambaye anafanya az-zuur analaumiwa kwa mtindo huu. Ndani ya Sunnah:
Anas bin Maalik (Allaah Amrehemu) amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja (Madiynah) na walikuta siku mbili ambazo kipindi cha Jaahiliyyah watacheza (na kujipumzisha).” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Allaah Amekupeni kilicho bora zaidi kuliko mambo hayo: Yawm adh-Dhuhaa (‘Iyd al-adh haa) na Yawm al-Fitr (‘Iyd al-Fitr).” [Imesimuliwa na Abuu Daawuud].
Hii inaonesha wazi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya shaka alizuia Ummah wake kusherehekea sherehe za kikafiri, na alihakikisha kuziondosha kwa njia zozote zinazowezekana.
Ukweli wa kwamba dini ya Watu wa Kitabu inakubaliwa, haina maana kwamba sherehe zao zinakubalika au ziendelezwe na Ummah, kama yalivyo matendo yao mengine ya kikafiri yasivyokubalika, na dhambi zao pia hazikubaliki. Hakika, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifikia hadi kuamrisha Ummah wake kujitofautisha nao kwenye mambo mengi ambayo ni mubaah (yanaruhusiwa) na kwa taratibu nyingi za ibada, kwa sababu tu; kwamba vinapelekea kuwa sawa nao kwenye mambo mengine pia. Hii kuweka tofauti; ni kuonesha kizuizi katika nyanja zote, kwa sababu namna utakavyokuwa tofauti na watu wa Motoni, ndivyo utakavyokuwa mchache wa kutenda matendo ya watu wa Motoni.
Ushahidi wa mwanzo ni Hadiyth ya: “Kila watu wana sherehe zao, na hii ndio sherehe yetu” ambayo ina kusudio maalum kwamba; watu wote wana sherehe zao wenyewe, kama Allaah Anavyosema (tafsiri ya maana):
{{Na kila ummah ulikuwa na Qiblah walichokielekea…}} [Al-Baqarah 2: 148]
na
{{Na kila (ummah) katika nyinyi (bin Aadam) Tumeujaalia shari'ah yake na njia yake.}} [Al-Maaidah 5: 48].
Hii inamaanisha kwamba kila taifa lina njia zake wenyewe. Hiyo laam ndani ya li-kulli (“kwa kila”, “katika nyinyi”) ina maana kwa watu maalum. Hivyo, kama Mayahudi wana sherehe na Wakristo wana sherehe, ni za kwao wenyewe, na sisi hatuna sehemu yetu ndani ya hizo sherehe, kama vile tusivyotumia Qiblah kimoja au sheria zao.
Ushahidi wa pili ni: masharti aliyoweka ‘Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kukubaliana pamoja na Swahaabah na Fuqaaha wote baada yao ni: kwa wale Watu wa Kitabu ambao wamekubali kuishi chini ya hukumu za Kiislamu (ahl adh-dhimmah) wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ndani ya Daar al-Islaam (ardhi zilizo chini ya hukumu za Kiislamu). Kama Waislamu wamekubaliana kuwazuia ahl adh-dhimmah kusherehekea wazi wazi, ni namna gani itakuwa sahihi kwa Waislamu kushereheka nao wazi wazi? Kama Muislamu atawasherehekea, jee sio zaidi ya kafiri anavyofanya wazi wazi?
Sababu iliyokuwepo ya sisi kuwazuia wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ni kwa sababu ya machafu yaliyokuwemo humo. Kwa sababu ya dhambi au alama ya dhambi. Katika kesi yoyote, Muislamu anazuiwa kutenda dhambi au kujaribu kutenda dhambi. Hata kama hakuna uadui wowote kwa Muislamu kuwa nao pamoja katika kusherehekea wazi wazi isipokuwa kafiri kupata nguvu ya kuendelea na matendo yake. Inakuwaje Muislamu anatenda hivyo? Uadui uliokuwemo (ndani ya sherehe zao) utaelezwa chini, insha Allaah.
Al-Bayhaqiy amesimulia ikiwa na isnaad swahiyh kwenye Baab karaahiyat ad-dukhuul ‘ala ahl adh-dhimmah fi kanaa’isihim wat-tashabbuh bihim yawmi nawruuzihim wa maharjaanihim (Sura kuhusu karaha ya kuingia kwenye makanisa ya ahl adh-Dhimmah (Makafiri walio katika nchi ya Kiislam)  katika kuadhimisha Mwaka wao Mpya na sherehe nyengine): Kutokana na Sufyaan ath-Thawri na kutokana na Thawr bin Yaziyd na kutokana na ‘Atwa’ bin Diynaar ambao wamesema: ‘Umar amesema: “Musijifunze lugha ya wasiokuwa Waarabu, musiingie pamoja na mushrikiyn kwenye makanisa yao katika siku za karamu zao, kwani laana (za Allaah) zinawashukia juu yao.”
‘Umar bin al-Khattwaab amesema:
“Jiepusheni na maadui wa Allaah kwenye sherehe zao.” Imesimuliwa kutokana na Abuu Usaamah ikiwa na isnaad iliyo sahihi kwamba: ‘Awn alituambia kutokana na Mughiyrah kutokana na ‘Abdullaah bin ‘Amr: “Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.” ‘Umar alikataza kujifunza lugha zao, na hata kuingia kwenye makanisa yao katika siku ya sherehe yao, jee ni vipi kwa kufanya baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye siku hizo, au kufanya vitu ambavyo ni sehemu ya dini yao? Je, sio kufanya baadhi ya vitu wanavyofanya kwenye sherehe zao ni (uovu) zaidi ya kuingia tu kwenye sherehe zao? Kama laana za Muumba zitaanguka juu yao kwenye siku ya sherehe yao kwa sababu ya yale wanayofanya, je, adhabu hiyo haitokuwa sawa kwa yule anayefanya yale wanayotenda wao, au sehemu ya hayo? Je, sio maneno ya: “Jiepusheni na maadui wa Allaah, kwenye sherehe zao” yana maana kwamba tusikutane nao au kushirikiana nao kwenye siku hizi? Je, ni vipi kwa mtu ambaye hakika anasherehekea sherehe zao?
‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kwa uwazi:
“Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.”
Hii inamaanisha kwamba yule anayejikusanya nao kwenye mambo yote haya ni kafiri, au kwamba kufanya hivi ni miongoni mwa dhambi kubwa (kabaa’ir) kwamba itampelekea mmoja wao Motoni; maana ya iliyopita ni ile iliyo wazi kutokana na mpangilio wa maneno. Alitaja – Na Allaah Ndie Ajuaye Zaidi – yule anayeishi kwenye ardhi yao, kwa sababu wakati wa ‘Abdullaah bin ‘Amr na Swahaabah wengineo, walikuwa wakizuia sherehe zilizo wazi za kikafiri ndani ya ardhi za Waislamu. Na hakuna Muislamu aliyewaiga kwenye sherehe zao; hilo (la kusherehekea) pale ambapo wanapoishi kwenye ardhi za kikafiri. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa hata kulitambua jina la sherehe zao ambazo zilikuwa mahsusi kwa ajili yao, je, itakuwaje kwa kushereheka nao kisawasawa? Ahmad ametaja maana ya simulizi zilizopokelewa kutokana na ‘Umar na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwenye mada hii, na wafuasi wake walijadili masuala ya sherehe.
Imaam Abul-Hassan al-‘Aamidiy alisema: mwandishi anayejulikana kwa jina la Ibn al-Baghdaadi alisema ndani ya kitabu chake Umdat al-Haadhwir wa Kifaayat al-Musaafir: “Hairuhusiwi kuingia kwenye sherehe za Wakristo na Mayahudi.” Ahmad alitamka hili kwenye simulizi ya Muhannaa, na ushahidi wake wa hilo ni Aayah (tafsiri ya maana):
{{Na wale ambao hawashuhudii shahada za uongo (az-zuur)…}} [Al-Furqaan 25: 72].
Alisema: (Hizi sherehe ni) ash-Sha’aaniyn pamoja na sherehe zao. Alisema: Waislamu wazuiliwe kuingia kwenye masinagogi (makanisa ya Kiyahudi) na makanisa (ya Wakristo).”
Kutokana na Iqtidhwa’ as-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab al-Jahiym iliyoandikwa na Shaykh al-Islaam bin Taymiyah, uk. 183.
Kuwatakia kheri ya Krismasi Makafiri na hata sikukuu nyengine za dini tofauti ni haraam kwa mujibu wa makubaliano ya wengi, kama Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu) alisema kwenye Ahkaam Ahl adh-Dhimmah.
“Kuwatakia kheri Makafiri katika mwenendo ambao ni kwa ajili yao ni haraam kwa makubaliano ya wengi, kama ilivyo haraam kuwatakia kheri katika sherehe zao na funga zao kwa kusema ‘Kila la kheri katika sherehe’ au ‘Nakutakia sherehe njema’, na mengineyo. Hata kama yule anayesema haya ameepushwa na ukafiri, lakini bado imekatazwa. Ni kama vile kumpa hongera mtu kwa kuuhami msalaba, au zaidi ya hivyo. Ni kama mfano wa dhambi iliyo kubwa sawa na kumpa hongera mnywaji ulevi, au kumuua mtu, au kuwa na mahusiano ya kinyama, na mengineyo. Wengi miongoni mwa wasio na heshima ya dini yao wanaangukia kwenye kosa hili; hawakai kufikiria ubaya wa vitendo vyao. Yeyote anayempa hongera mtu kwa kutovukwa na adabu au bid’ah au ukafiri amejiweka wazi na laana pamoja na ghadhabu za Allaah.”

Kuwapatia hongera makafiri kwenye sherehe za kidini ni haraam kama alivyokwenda mbali Ibn al-Qayyim kwa kufananisha na kwamba yule anayetoa salamu hizo amekubali au ameidhinisha matendo yao ya kikafiri, hata kama mtu hatovifanya mwenyewe vitu hivyo. Lakini Muislamu asikubali mienendo ya kikafiri wala kumpa hongera yeyote kwa ajili yao, kwa sababu Allaah hakubali matendo yoyote kati ya hayo, kama Alivyosema (tafsiri ya maana):

{{Mkikufuru, basi Allaah hana haja nanyi; lakini Haridhii kufuru kwa waja Wake; na kama mkishukuru; hayo Yanamridhisha kwenu.}} [Az-Zumar 39:7].

{{…Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu…}} [Al-Maaidah 5:3].

Hivyo kuwapa pongezi kunazuiwa, hata ikiwa ni mwenzio kazini au vyenginevyo. Kama wao watatutakia kheri kwa kuadhimisha sherehe zao, hatutakiwi kujibu, kwasababu hizi sio sherehe zetu, na kwasababu sio sherehe ambazo zinakubalika na Allaah. Sherehe hizi ni uzushi ndani ya dini zao, na hata zile ambazo zimetajwa huko kabla zimetenguliwa na dini ya Kiislamu, ambayo Ameileta Allaah kwa wanaadamu wetu kupitia kwa bwana Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Anasema (tafsiri ya maana):

{{Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Aakhirah atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa)}} [Aaali-‘Imraan 3:85].

Ni haraam kwa Muislamu kukubali mialiko katika sherehe kama hizo, kwa sababu ni zaidi ya kuwatakia kheri kama inavyoonesha kushiriki katika sherehe zao. Vile vile, Waislamu wanazuiwa kuwaiga makafiri katika kuadhimisha huko kwa kushiriki kwenye tafrija parties, au kwa kubadilishana zawadi, au kutoa peremende au chakula, au kuacha kufanya kazi, n.k. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema “Yeyote anayewaiga watu ni mmoja wao.”

Shaykh al-Islaam bin Taymiyah amesema ndani ya kitabu chake Iqtidhwaa’ asw-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab Al-Jahiym:
“Kuwaiga katika baadhi ya sherehe zao inamaanisha kwamba mtu amefurahia imani zao za uongo na vitendo vyao, na anawapa matumaini kwamba wanaweza kuwa na nafasi ya kuwanyanyasa na kuwapeleka ovyo wanyonge.” Yeyote anayefanya mambo kama haya ni mtenda dhambi, ikiwa anafanya kwa ukarimu au urafiki, au kwa sababu anaona hayaa kukataa, au kwa sababu nyengine yoyote. Kwa sababu ni unafiki ndani ya Uislamu, na kwa sababu inawafanya makafiri kujisikia fakhari kwa dini yao.

Allaah Pekee ndiye tunayemuomba kuwafanya Waislamu kuwa fakhari na dini yao, kuwasaidia kuwa thaabiti katika kushikamana na dini yao, na kuwafanya kuwa washindi dhidi ya maadui zao, kwani Yeye Mwenye Nguvu ndiye Mwenye Kuweza.


Kutoka chapisho la http://www.alhidaaya.com/sw/node/2314

Sasa tunaweza kuweka Commments zetu karibuni wana MSATEKU

As.alaykum wanajumuiya ya MSATEKU..sasa tumerekebisha Blog yetu....kwa kuweka utaratibu wa kuacha Comments zako mara baada ya kupitia taarifa mbalimbali za Jumuiya....Sasa hivi utachotakiwa kufanya ni kuandika Comment yako hapo chini,kwa kwenda sehemu iliyoandikwa NO COMMENTS kama hazipo COMMENTS au kama zipo basi utakuta idadi zake,BOFYA HAPO then andika COMMENT yako  na ubofye sehemu iliyoandikwa Publish then utaletewa Characters ili kuhakikisha kama wewe sio Robots then ziandike kwa kufuata utaraibu wa maneno uliopewa....kama huyaelewi bonyeza nusu duara ili yabadilike na ukiyaona unayaelewa.......kitakachofuata ni kuonekana kwa comment yako,ila nawasihi tuwe wastarabu kwa kutoa comments zenye maadili na kujenga jumuiya yetu na sio kubomoa.....ni vizuri pia ukiandika jina lako ili tufahamiane.....

                                       Karibuni Sana.................

Saturday, December 15, 2012

Maendeleo ya jengo la Mradi wetu

Assalam Alaykum....zifuatazo ni picha mbalimbali za jengo letu la Mradi wa Mgahawa wa kisasa.....pamoja na Msikiti.....angalia mwenyewe tulipofikia mpaka sasa......

 Ujenzi unaendelea.....mapema wiki chache zilizopita...nenda chini ujionee picha za sasa.....





Picha za leo tarehe 15 - 12 - 2012 jioni,hii ni dalili nzuri ya kuwa jengo laendelea vizuri na linataraji kwisha mapema...Alla atufanyie wepesi katika hili.....

PICHA MBALIMBALI ZA SIKUKUU YA IDD AL HAJI KWA WANAJUMUIYA WA MSATEKU

Assalam Alaykum.......leo ndugu Muislam nakuletea picha mbalimbali za matukio ya sherehe za Sikukuu ya IDD Al Haji 2012,ambapo vijana wa MSATEKU walijumuika pamoja kusheherekea,shughuli zilianza asubuhuhi kwa kunywa chai ya pamoja na hadi mchana kwa kula pamoja pia......ama hakika tamaduni hii inazidi kuendelea katika Jumuiya yetu.....Allah atubaliki tuendeleze umoja wetu tuliokuwa nao............karibu ujionee picha hapo chini.......




 Mambo ya Chai hayo na Vijitambi na Maandazii...........karibu tule....
 Chai jamani karibuni........
 Baada ya Chai....vijana walikuwa wankumbushana mambo ya Dini..........na mambo ya kimaisha kiujumla huku wakisubili muda mchana ufikee.

 Amir wa Da`awa akimfuatilia maalim Ahmed.....kuwa anasoma vile inavyotakiwa......huku akitabasamu
 Tafakul baada ya chai......vipi mchana upo hapa jamani......nahisi wanajiuliza......
 Maukht nao walikuwepo kupiga vikombe......

 Baada ya chai vyombo vilioshwa......vijana waliajibika


 Maandalizi ya mchana yalifuata.....mbuzi aliangushwa.........

 Amir wa jumuiya akiwaongoza vijana kuchinja

 Mbuzi amechinjwa....vijana walikuwa madhubuti kuhakikisha Sunnah inatimia......na Mbuzi hakiimbiiiii
 Baada ya maandalizi ya mchana ni mcheleeeee.......shekh tukaribishe bhana......
 Maalim SESEME......peke yako yakhe......ama hakika raha ya mpunga sharti uvalie kilemba......
 Vijana wanaufinya hakika ilikuwa rahaaaaa....
 ulaji wa kisunna pia ulizingatiwa kwa vijana kujumuika pamoja.........hallow msiniwekeee nakula hukuhuku msikitini.......njie endeleeni.......anaovoelekea maalim Ahmed kuongea
Vidume vitatu tu......sahani TANO.......jamani rahaaaaaaa.........msosi ulikuwepo wa kutosha......