Wednesday, July 10, 2013

Mawaidha kwa njia ya Video Mada watu Kumi waliosamehewa kufunga na Shekh Nurdin Kishk........!!!!!!!karibuni sana....


Msateku wafuturu kwa pamoja........

As.alaykum....!!!!huku mitihani ikiendelea ambapo hatimaye ni Kesho sawa na tarehe 11/7/2013, Msateku kwa pamoja leo walipata futari ya pamoja katika chungu Mosi...hakika ilivutia na ilikuwa rahaa kwa vijana hawa.....nakupatia baadhi ya picha za tukio hilo...lilofanyika katika Mgahawa na Msikiti wa Jumuiya.

 baadhi ya wanajumiuya pichani...wakipata futariii
 Maukht nao walikuwepo.......wakipata futuruuuuuuuuuu

Mwalimu Rais Mwinyi katika Tamasha la Kiswahili









Rais Mstaafu, Mwalimu A. H. Mwinyi akihutubia katika maadhimisho ya Tamasha la Kiswahili.
Rais Mstaafu, Mwalimu Ali Hassan Mwinyi siku ya Jumamosi Juai 6, 2013 katika ukumbi wa Hamton Place alikamilisha sherehe za miaka 3 ya blog ya Vijimambo pamoja na Tamasha la Kiswahili lililoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania na uongozi wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC, nchini Marekani.

Baadhi ya Watanzania kutoka maeneo mbalimbali walihudhuria na kuisikiliza hotuba ya Rais na Mwalimu Mwinyi aliyoitoa ambayo iligusia misingi ya matumizi ya baadhi ya maneo ya Kiswahili ambayo tunayatumia kwa makosa kwa kuchanganya umoja ama wingi wake. Alitoa mifano ya matumizi ya maneno yafutayo:

UMOJA na WINGI

Ni sahihi kusema “madhehebu” na siyo sahihi kusema, “dhehebu”. Neno madhehebu halina wingi. Hakuna neno dhehebu.

Ni sahihi kusema mahitaji, lakini si sahihi kusema hitaji

Mafao
 na siyo fao

Ni mahakama, hakuna hakama
Majuto ni neno moja, hakuna neno juto

Mateso
 ni sahihi, hakuna teso

Sahihi kusema madhila na siyo dhila

Maradhi
 na siyo radhi (radhi ni neno jingine lenye maana nyingine. Mathalani kumwona mwendawazimu na 
kusema, "yule kakosa radhi kwa baba yake...")

Neno shule halina wingi (ni singular, asili yake Kijerumani), Shule moja, shule hamsini (hakuna mashule)

Askari (akiwa mmoja, wakiwa mia bado ni askari) siyo maaskari

Polisi (mmoja au wengi) hakuna neno mapolisi

Saa (saa haina wingi). Si sahihi kusema, “nimesafiri kwa masaa mengi” bali sahihi kusema nimesafiri kwa saa...)

Hesabu (haina wingi, inabakia kuwa hesabu) hakuna mahesabu

Upungufu, hakuna neno mapungufu

Uamuzi
, hakuna neno maamuzi

Ni uhusiano, hakuna neno mahusiano

Na ni ushirikiano, siyo neno mashirikiano. Halipo neno hilo katika Kiswahili sanifu.


MATUMIZI YA SILABI

Matumizi ya silabi 'sha' maana yake ni kisababishi/inasababisha. Kwa mfano, si sahihi kusema, "Nimemwenda Marekani sina nyumba ilinibidi nikodishe" kwa kuwa kama huna kitu, wewe utasema, "Nimekwenda Marekani sina nyumba ilinibidi nikodi". Mimi sina nyumba nikodishe? Na mwenye nyumba akodishe? Hapana, 'sha' ni kisababishi. Asiye na nyumba akodi, na mwenye nyumba akitaka akodisha. Ama, “Juma nusura kunifukuzisha kazi kwa fitina yake”. Yaani ningefukuzwa kazi kwa fitina ya Juma.

KUHESABU

Hesabu: Vitu huhesabiwa moja, mbili, tatu n.k., ila watu huhesabiwa mmoja, wawili, watatu, wanane, tisa n.k., kwa sababu maneno tunayoyaazima kutoka kwenye lugha nyinginezo, tusiyaingilie kuyachokoa. Sita, Saba, Tisa ni Kiarabu, si Kiswahili, ndiyo maana twasema Watu, ng’ombe sita, saba, tisa.