Rais Mstaafu, Mwalimu A. H. Mwinyi akihutubia katika
maadhimisho ya Tamasha la Kiswahili.
Rais Mstaafu, Mwalimu Ali Hassan Mwinyi siku ya
Jumamosi Juai 6, 2013 katika ukumbi wa Hamton Place alikamilisha sherehe za
miaka 3 ya blog ya Vijimambo pamoja na Tamasha la Kiswahili lililoandaliwa na
Jumuiya ya Watanzania na uongozi wa Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC,
nchini Marekani.
Baadhi ya Watanzania kutoka maeneo mbalimbali walihudhuria na kuisikiliza hotuba ya Rais na Mwalimu Mwinyi aliyoitoa ambayo iligusia misingi ya matumizi ya baadhi ya maneo ya Kiswahili ambayo tunayatumia kwa makosa kwa kuchanganya umoja ama wingi wake. Alitoa mifano ya matumizi ya maneno yafutayo:
UMOJA na WINGI
Ni sahihi kusema “madhehebu” na siyo sahihi kusema, “dhehebu”. Neno madhehebu halina wingi. Hakuna neno dhehebu.
Ni sahihi kusema mahitaji, lakini si sahihi kusema hitaji
Mafao na siyo fao
Ni mahakama, hakuna hakama

Majuto ni neno
moja, hakuna neno juto
Mateso ni sahihi, hakuna teso
Sahihi kusema madhila na siyo dhila
Maradhi na siyo radhi (radhi ni neno jingine lenye maana nyingine. Mathalani kumwona mwendawazimu na

kusema, "yule kakosa radhi kwa baba
yake...")
Neno shule halina wingi (ni singular, asili yake Kijerumani), Shule moja, shule hamsini (hakuna mashule)
Askari (akiwa mmoja, wakiwa mia bado ni askari) siyo maaskari
Polisi (mmoja au wengi) hakuna neno mapolisi
Saa (saa haina wingi). Si sahihi kusema, “nimesafiri kwa masaa mengi” bali sahihi kusema nimesafiri kwa saa...)
Hesabu (haina wingi, inabakia kuwa hesabu) hakuna mahesabu
Upungufu, hakuna neno mapungufu
Uamuzi, hakuna neno maamuzi
Ni uhusiano, hakuna neno mahusiano
Na ni ushirikiano, siyo neno mashirikiano. Halipo neno hilo katika Kiswahili sanifu.
MATUMIZI YA SILABI
Matumizi ya silabi 'sha' maana yake ni kisababishi/inasababisha. Kwa mfano, si sahihi kusema, "Nimemwenda Marekani sina nyumba ilinibidi nikodishe" kwa kuwa kama huna kitu, wewe utasema, "Nimekwenda Marekani sina nyumba ilinibidi nikodi". Mimi sina nyumba nikodishe? Na mwenye nyumba akodishe? Hapana, 'sha' ni kisababishi. Asiye na nyumba akodi, na mwenye nyumba akitaka akodisha. Ama, “Juma nusura kunifukuzisha kazi kwa fitina yake”. Yaani ningefukuzwa kazi kwa fitina ya Juma.
KUHESABU
Hesabu: Vitu huhesabiwa moja, mbili, tatu n.k., ila watu huhesabiwa mmoja, wawili, watatu, wanane, tisa n.k., kwa sababu maneno tunayoyaazima kutoka kwenye lugha nyinginezo, tusiyaingilie kuyachokoa. Sita, Saba, Tisa ni Kiarabu, si Kiswahili, ndiyo maana twasema Watu, ng’ombe sita, saba, tisa.

No comments:
Post a Comment