Wednesday, October 30, 2013

kikao cha wanajumuiya wa MSATEKU kilichofanyika oktoba 27 katika msikiti wa wanajumuiya wa msateku... katika kikao icho waliudhulia baadhi ya waitimu wa 2010/13 ambao walikuwa wanajumuiya...miongoni mwao alikuwepo akhy SESEME, brother JARIBU na RIZIWANI..

  baadhi ya matukio...... wakati wa kikao......


Baada ya kikao wanajumuiya walikwenda JIDDAH RESTAURANT kupata chakula cha mchana.. 
karibuni sana JIDDAH kunachakula kizuri na tunawapishi mahili kabisa... bila shaka ukifika JIDDAH RESTAURANT roho yako itasuuzika kwa uduma zetu...

Saturday, October 26, 2013

Mahafali ya TEKU 2013

Siku ya tarehe 26/10/2013.....chuo cha TEKU kiliazimisha mahafali ya Sita(6) tangu kuanzishwa kwake....baadhi ya Wanajumuiya na viongozi wa wastaafu wa Msateku walikuwa washiriki wa mahafali hiyo.....lakini cha kumshukuru ALLAH kiongozi mstaafu wa Idara ya Elimu katika MSATEKU pia alikuwa Naibu Amir wa TAMSYA Mbeya AMOUR ABDALLAH....alitunukiwa zawadi ijulikanayo kama TEKU PRIZE baada ya kufanya vizuri katika masomo kwa mwaka 2010-2013 kwa kupata matokeo ya jumla ya G.P.A ya 4.7 hakika anapaswa kupongezwa na pia Jumuiya ya MSATEKU....zifuatazo ni baadhi ya matukio hayo.


Mshindi wa zawadi ya TEKU PRIZE....Amour Abdallah....aliibuka kidedea kama mwanafunzi bora katika mwaka wa masomo 2010-2013 kwa kupata G.P.A ya 4.7......HONGERA SANA BROTHER.....!!!!

 Baadhi ya viongozi wastaafu waliohitimu 2013 kutoka kulia ni Brother Jaribu,Kato Mudathiru,Hassan Mavue na Seseme Shaabani.

 Hakika ni kwa kumshukuru Mungu.....BROTHER JARIBU (katibu mkuu Mstaafu wa MSATEKU) nae alikuwepo....hapo ni katika maandamano.
 kabla ya mahafali kuanza......
 hakika ilifana.....
 zawadi zilitolewa......
 Tabasamu baada ya kumaliza DEGREE ya kwanza....HONGERENI SANA.

TAKBIRR......!!!!!!TAKBIRRR.........!!!!TAKBIRRR......!!!!

Assalam Alaykum.....!!!!!wanajumuiya wa MSATEKU na wale waislamu wote kwa ujumla ......hatuna budi kumshukuru ALLAH.....kwa hatua tuliyofikia hivi sasa katika maendeleo ya MRADI wetu wa Mgahawa....hakika ALLAH wa kushukuliwa katika yote mazuri tuliyoyafikia......Tayari mradi wetu wa Mgahawa umeanza kazi na mambo yanaendelea ndani ya MSATEKU.....Mgahawa unaitwa JIDDAH....na umeanza kuwa maarufu katika eneo la BLOCK T.......zifuatazo ni picha za Mgahawa huo...ndani na nje.....yapata mwezi sasa tangu kuanza rasmi.....ulianza tarehe 26 /09/ 2013.
 Jiddah Restaurant.....ndio maneno yanayosemeka kwa nje ya mgahawa wetu

 Ndani ya mgahawa kuna wateja na wafanyakazi wetu.....suala la usafi na muonekano nadhifu limezingatiwa.
 karibu mteja...........
 mambo ya asubuhi hayoo....chai ya maziwa, ya Mdarasini....,Tangawizi......pamoja na SUPU ya Ngo'mbe utapata.

 Hakika kunavutia........karibuni sanaaa JIDDAH.....