Wednesday, November 5, 2014

ASSALAM ALAIKUM WARAH-MATULLAHI WABARAKATUH, NDUGU ZANGU WANAJUMUIYA HII NDIO RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA, IMELETWA KWENU ILI MUISOME, MUIELEWE NA MCHANGIE MAONI YENU ILI TUIPITISHE INSHAALLAH

NDUGU ZANGU IFAHAMIKE YA KWAMBA JUMUIYA BILA KATIBA ITAKUWA VIGUMU SANA KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA JUMIYA YETU, PIA IFAHAMIKE KWAMBA KATIBA HII IMEUNDWA KWA KUTUMIA KATIBA KUU YA TAMSYA NA PIA IFAHAMIKE YOTE AMBAYO YAMEPENDEKEZWA HAYAPO KINYUME NA QUR'AN NA SUNNAH.





RASIMU YA KATIBA YA JUMUIA YA WANAFUNZI WA KIISLAM
CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI











Anwani ya  jumuiya














2014
YALIYOMO
                                                            SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI                                                                                                                         
Kifungu……………………………………………………………………………………………….1
1.      Jina…………………………………………………………………………………………………....1                                                                                                                        
2.      Anwani………………………………………………………………………………………………..1                                                                                                                  
3.      Motto………………………………………………………………………………………………….1                                                                                                                      
4.      Madhumuni…………………………………………………………………………………………....1                                                                                                           
5.      fasili /ufafanuzi………………………………………………………………………………………....1   

SEHEMU YA PILI

6.1.UANACHAMA WA MSATEKU UTAKUWA WA AINA MBILI……………………………….2  
                                     i.        Uanachama wa asili………………………………………………………2 
                                      ii.      Uanachama wa heshima………………………………………………….2
6.1.1UANACHAMA WA ASILI…………………………………………………………………….2
6.1.2.UANACHAMA WA HESHIMA………………………………………………………………2
6.1.3.HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA………………………………………….……….2
6.1.4.KUJIANDIKISHA KUWA MWANACHAMA KAMILI……………………………………..2
6.1.5.UKOMO WA MWANACHAMA…………………………………………………………......2
6.1.6.MAADILI UA MWANACHAMA…………………………………………………………….2
SEHEMU YA TATU
7. BODI YA MSATEKU/WADHAMINI……………………………………………………………3
7.2.MATAWI YA MSATEKU………………………………………………………………….……3
7.3.UWAKILISHI……………………………………………………………………………….......3
7.3.1 MKUTANO MKUU WA TAWI…………………………………....…………………………3
7.4.MKUTANO MKUU WA WILAYA……………………………………………………………..3
7.5.MKUTANO MKUU WA MKOA……………………………………………...………………..3
7.6. MKUTANO MKUU WA TIFA...……………………………………………………………….4



SEHEMU YA NNE
8. IDARA ZA MSATEKU…………………………………………………………………………...5
8.1.IDARA YA ELIMU NA AMALI………………………………….……………………………..5
8.1.1.IDARA YA FEDHA,UCHUMI NA AMALI……………………………..…………………….5
8.1.2.IDARA YA HABARI,UHUSIANO NA USTAWI WA  JAMII…………………………………6
8.1.3.IDARA YA WANAWAKE……...………………………………………………………………6
SEHEMU YA TANO
9.KANUNI NA TARATIBU ZA VIKAO…………………..………………………………………...6
9.1.KANUNI ZA VIKAO……………………………………………………………………………6
9.1.1.TARATIBU ZA VIKAO……………………………………..………………………………….6
9.1.2. MAHUDHURIO……………………………………………………………………………….6
SEHEMU YA SITA
10.SIFA ZA VIONGOZI,MUDA NA TARATIBU ZA UTEUZI……………………………………...6
SEHEMU YA SABA.
11.VIONGOZI………………………………………………………………………………………..7
11.1 KAZI NA MAMLAKA YA VIONGOZI………………………………………………..……….7
SEHEMU YA NANE
12-KANUNI NIDHAMU…………………………………………………………………………….8
SEHEMU YA TISA
13.MAREKEBISHO YA KATIBA……………………………………………………….…………..8
SEHEMU YA KUMI
14.MENGINEYO…………………………………………………………………………………….9









SEHEMU YA KWANZA
1.      JINA: JUMUIYA YA KIISLAM YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI
2.      ANWANI
MWENYEKITI/AMIR
JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAM,
CHUO KIKUU
TEOFILO KISANJI
HALMSHAURI YA JIJI ,MBEYA
S.L.P
MBEYA.

3.      MOTTO WA JUMUIYA:
4.      MADHUMUNI.
i)        kukuza ufahamu wa wanachuo na vijana juu ya uislamu na kutoa ufumbuzi wa kiislam kwa matatizo ya jamii ya sasa na ijayo .
ii)      kusaidia wanafunzi na vijana kujenga hulka ya kiislam kwa kutumia mafunzo ya kimaadili ,kiitikadi na kijamii .
iii)    kukuza moyo wa kindugu wa kiislam na ushirikiano na jumuiya nyingine zenye shabaha na madhumuni kama msateku.
iv)    kuwaunganisha vijana na wanachuo katika kupambana na majamga yanayoikabili jamii.
v)      kuwakilisha wanachuo na vijana wa kiislam.Tanzania katika vikao vya kutaifa na kimataifa.
vi)    kushirikiana na jumuiya nyingine za kijamii kiserikali,kidin,kitaifa,na kimataifa katika kuiletea maendeleo jamii na taifa kwa ujumla.
vii)  kusimamia,kulinda na kutetea haki za vijana nawanafunzi wa kiislam Tanzania.
viii.  kuendesha na kusimamia miradi ya maendeleo ya huduma za jamii na kumiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika.
ix.  kujitolea kufanya kazi nyingine zenye maslahi kwa wanachuo na wanafunzi wa kiislam na jamii kwa ujumla .

5.      FASILI/UFAFANUZI.
i. mahali popote ambapo maneno yanayotamkwa chini yametumika katika katiba hii,yana maana au ufafanuzi au fasili iliyotolewa juu yake ama iliyotolewa kishera iwapo pana sheria yoyote nchini kuhusiana nayo:
ii. bodi ya wadhamini chombo cha wadhamini wa jumuiya cheye wajumbe watano.
iii. jumuiya-ni mkusanyiko wa wanachuo wenye lengo la kuendeleza na kustawisha zaidi maadili na maendeleo ya uislam.
iv kanuni-taratibu zinazoitafsiri katiba ya kutoa mwongozo wa kutekeleza katiba ya jumuiya




SEHEMU YA PILI

6.      UANACHAMA WA MSATEKU
i)        uanachama wa asili
ii)      uanachama wa heshima

6.1.    UANACHAMA WA ASILI  
-          utakua wazi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi mlezi.
-          mwanachuo wa kiislam kwa kulipa ada ya wanachama,uanachama wa mwanachuo ni wa mtu mmoja mmoja


6.1.1.      UANACHAMA WA HESHIMA
uanachama waheshima utakuwa wazi kwa mtu yeyote bila kujali umri au jinsia kwa mtu yeyote bila kujali umri au jinsia atakayependekezwa na kamati tendaji ya msateku wilaya,mkoa au taifa na kuidhinishwa na kamati tendaji ya msateku taifa na atateuliwa kutokana na umuhimu wake katika jumii kwa kulinda maslahi ya msateku.

6.1.2.      HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA WA ASILI
i)        kushiriki katika vikao vyote halali vinavyomhusu.
ii)      kushiriki katika shughuli za jumuiya za kila siku kwa mujibu wa kanuni na taratibu
iii)    kupendekeza au/ na kuchagua viongozi wa jumuiya
iv)    kupendekezwa au/ na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa jumuiya
v)      kushiriki katika kamati za jumuiya kwa majibu wa kanuni na taratibu
vi)    kujua namna jumuiya inavyoendeshwa
vii)  kuhoji au /na kukosoa [ikibidi]uendeshwaji wa jumuiya kwa maslaha ya jumuiya na uislam
viii)                                                                                       kushirikiana na viongozi pamoja na wanachama wengine katika kufanya maamuzi inapobidi


6.1.3.      KUJIANDIKSHA KUWA MWANAJUMUIYA /MWANCHAMA KAMILI
   mwanajumuiya ataorodheshwa katika daftari kuu la jumuiya kwa jina kamili na taarifa nyingine zinazomhusu mwanajumuiya.

6.1.4.      UKOMO WA MWANAJUMUIYA/MWANACHAMA
i)        hakutoa ada yake kwa kipinde cha semester nzima.
ii)      akijitoa katika jumuiya.
iii)    akishindwa kutimiza maadili ya jumuiya kwa mfano ulevi,uzinzi,wizi,kashfa,usengenyaji.
iv)    akifariki dunia .
v)      mwanajumuiya akikomaa uanachama hatorudishiwa ada zake.

6.1.5.      MAADILI YA MWANAJUMUIYA
i)        mwajumuiya ni lazima azingatie maadili yaliyoandikwa katika vitabu vyetu vitakatifu Qurani na hadithi zaMtumeMohamad[S.A.W]




SEHEMU YA TATU

7.      BODI YA MSATEKU/WADHAMINI
7.1. kutakuwepo na bodi ya wadhamini ambayo itajulikana katika Katiba hii  kama bodi itakayoundwa na kamati tendaji ya MSATEKU taifa kwa kushauriana na sekretariati ya MSATEKU taifa na muda wake utakuwa ni miaka miwili [2]
                                i.            bodi itajumuisha wajumbe watano,watatu kati yao wataidhinishwa na mkutano mkuu,katibu mkuu na katibu mtendaji wataingia kwa nafasi zao.
                              ii.            bodi itaweka sera ya jumuiya ya MSATEKU kusimamia shughuli zake na kuweka juhudi katika kufikia madhumuni ya MSATEKU
                            iii.            bodi ndiyo msimamizi mkuu wa mali na amana za MSATEKU
                            iv.            bodi itawakilisha jumuiya katika masuala yate ya kisheria na mikataba.
                              v.            bodi itakua na haki ya kukopa na kukopeshwa na kukopesha na kukopesheka kwa niaba ya [MSATEKU]
                            vi.            katika mkutano wake wa kwanza bodi itamchagua mmoja wa wajumbe wake kati ya waliochaguliwa na mkutano mkuu kuwa mwenyekiti.
                          vii.            katibu mtendaji atakuwa katibu wa kudumu wa bodi
                        viii.            akidi ya mkutano wa bodi ya wadhamini haitopungua idadi ya wajumbe 3 na uamuzi wake utapitishwa ikiwa utakubalika na zaidi ya nusu ya wajumbea waliohudhuria mkutano . maamuzi yote katika bodi yatafuata misingi ya      Quar-an na sunnah za mtume [s.a.w]
                            ix.            maamuzi yote katika bodi yatafuata misingi ya Qur-an na sunnah za Mtume[S.A.W]

7.2. MATAWI YA MSATEKU
                                 i.            kila chuo au asasi mwanachama wa MSATEKU itakuwa ni tawi la MSATEKU
                               ii.            matawi yaliyotajwa kifungu 7.2[ i.] yataunda MSATEKU ngazi ya wilaya
                             iii.            MSATEKU wilaya zitaunda MSATEKU mkoa
                             iv.            MSATEKU Ngazi ya mkoa zitaunda MSATEKU taifa.
 
7.3.  UWAKILISHI

7.3.1.      (a). MKUTANO MKUU WA TAWI
                                    i.            Mwenyekiti wa MSATEKU wa tawi
                                  ii.            Makamu mwenyekiti wa tawi
                                iii.            katibu wa tawi
                                iv.            Naibu katibu wa tawi
                                  v.            Wakuu na makatibu wa Idara/kamati za MSATEKU wa tawi
                                vi.            Mwanachuo wote wa kiislam tawini
                              vii.            Mlezi wa MSATEKU tawini

(b) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA TAWI
                                         i.            kupokea kujadili na kupitisha mihutasari ya mikutano iliopita
                                       ii.            kupokea,kujadili na kupitisha taarifa za maendeleo ya MSATEKU Tawini
                                     iii.            kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za maendeleo ya MSATEKU tawini
                                     iv.            kuzungumza masuala yenye manufaa kwa tawi nakuyatolea mapendekezo yake katika kamati ya utendaji ya tawi na wilaya
                                       v.             kuchagua viongozi wa kamati ya utendaji ya tawi
                     
                        (c) KAMATI TENDAJI YA TAWI
                                             i.            mwenyekiti wa tawi
                                           ii.            makamu mwenyekiti wa tawi
                                         iii.            katibu wa tawi
                                         iv.            Naibu katibu wa tawi
                                           v.            mweka hazina wa tawi
                                         vi.            wakuu, makatibu wakuu na wajumbe wa kamati au idara za MSATEKU katika tawi husika

                         
                          (d) KAZI ZA KAMATI TENDAJI YA TAWI
                                                i.            kutekeleza mikatakati/mipango naahughuli za msateku katika tawi
                                              ii.            kutoa ripoti ya jumla ya maendeleo uya shughuli za msateku kwenye mkutano mkuu wa tawi
                                            iii.            kutekeleza mikakati mipango na maazimio ya mkutano mkuu wa tawi

            7.3.2.  MKUTANO MKUU WA WILAYA
                      (a) KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU WA WILAYA UTAKAOHUDHURIWA NA:
                                                 i.            mwenyekiti na MSATEKU wilaya
                                               ii.            makamu mwenyekiti wa MSATEKU wilaya
                                             iii.            katibu wa MSETEKU wilaya
                                             iv.            naibu katibu mtendaji wa MSATEKU wilaya MSATEKU wilaya
                                               v.            katibu mtendaji wa MSATEKU wilaya
                                             vi.            mweka hazina na msaidizi wake wa msateku wilaya
                                           vii.            wenyeviti makamu wenyeviti na makatibu wa idara au kamati za  MSATEKU wilaya
                                         viii.            Wakuu na makatibu wa idara au kamati za MSATEKU wilaya
                                             ix.            mlezi wa MSATEKU wilaya
                                               x.            Mwenyekiti na Amira kutoka kila tawi ni MSATEKU

                      (b) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA WILAYA
                                           i.            kupokea,kujadili na kupitia mihutasari iliyopita
                                         ii.            kupokea,kujadili nakupitisha taarifa za maendeleo ya msateku wilaya
                                       iii.            kuchagua viongozi wa kamati ya utendaji msateku ngazi ya wilaya
                                       iv.            Itapokea mipango,maazimio na mikakati na maagizo ya mkutano mkuu wa mkoa na taifa kwa utekelezaji

(c)    KAMATI TENDAJI YA MSATEKU WILAYA
                                       i.            Mwenyekiti wa wilaya
                                     ii.            Makamu mwenyekiti wa wilaya
                                   iii.            katibu wa wilaya
                                   iv.            Naibu katibu wa wilaya
                                     v.            mweka hazina wa wilaya
                                   vi.            wakuu,makatibu na wajumbe wa kamati au idara za MSATEKU wilaya

(d)   KAZI ZA KAMATI TENDAJI YA MSATEKU
                             i.    Kupokea,kujadili na kupisha mihutasari ya mikutano iliyopita.
                            ii.   kitakuwa ndicho chombo kitakachoshughulika na kazi za kila siku za MSATEKU wilaya
                           iii.  Itatoa taarifa ya shughuli za MSATEKU wilaya katika mkutano mkuu wa wilaya
                           iv.   itapokea mipango ,maazimio na mikakati na /au maagizo ya mkutano mkuu wa wilaya  na  mkoa
         

          7.3.3. MKUTANO MKUU WA MKOA
                  (a) KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU WA MKOA UTAKAO HUDHURIWA NA
                            i.              Mwenyekiti MSATEKU mkoa
                            ii.            Makamu mwenyekiti MSATEKU mkoa
                            iii.           Katibu MSATEKU mkoa
                            iv.           Naibu katibu MSATEKU mkoa
                             v.           Katibu mtendaji wa MSATEKU
                             vi.         Wenyeviti,makatibu wa idara ,kamati za MSATEKU mkoa
                            vii.          mweka hazina wa MSATEKU wa mkoa
                          viii.           Mwenyekiti,Amira na wajumbe watatu kutoka kila wilaya
                            ix.            mlezi wa MSATEKU wa mkoa
                (b) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA MKOA
                             i.            Kupokea,kujadili na kupitisha mihutasari ya mkutano iliyopita ya mkoa husika   
                           ii.            kupokea,kujadili na kupitisha taarifa za maendeleo ya MSATEKU mkoa
                         iii.            kuidhinisha uteuzi wa mlezi wa mkoa
                         iv.            kuchagua viongozi wa kamati tendaji ya MSATEKU ngazi ya mkoa
                           v.            kuchagua wajumbe watatu watakaoungana na mwenyekiti na Amira kuwakilisha mkoa katika mkutano mkuu wa MSATEKU taifa

(c)    KAMATI TENDAJI YA MSATEKU  MKOA
                                  i.            Mwenyekiti  MSATEKU  mkoa
                                ii.            Makamu mwenyekiti MSATEKU wa mkoa
                              iii.            katibu MSATEKU wa mkoa
                              iv.            Naibu katibu MSATEKU wa mkoa
                                v.             katibu wa mtendaji MSATEKU wa mkoa
                              vi.            wakuu,makatibu na wajumbe wa kamati,idara za MSATEKU  mkoa
               (d)  KAZI ZA KAMATI TENDAJI MSATEKU MKOA
                                 i.            Kupokea,kujadili na kupitisha miutasari ya mkutano uliopita
                               ii.            Iitakuwa ndicho chombo kitakachoshughulikia na kazi za kila sikauy za MSATEKU mkuu
                             iii.            itatoa taarif ya shughuli za MSATEKU mkoa katika mkutano mkuu wa mkoa
                             iv.            Itapokea mipango, maazimio na miakati na au maagizoya mkutano mkuu wa mkoa na taifa kwa utekelezaji
       7.3.4   MKUTANO MKUU WA TAIFA
              (a) KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU WA TAIFA NA MSATEKU MKUTANO MKUU
                    UTAKAOJUMUISHA;
                            i.            Rais/amir wa MSATEKU taifa
                          ii.            makam rais/naibu amir WAMSATEKU taifa
                        iii.            katibu mkuu wa MSATEKU taifa
                        iv.            Naibu katibu MSATEKU taifa
                          v.            Amira wa MSATEKU taifa
                        vi.            Katibu mtendaji wa MSATEKU taifa.
                      vii.            wajumbe wote wa kamati tendaji ya MSATEKU taifa
                    viii.            wajumbe watano kutokaa kila mkoa
                        ix.            Wajumbe wengine kutoka ngazi mbalimbali watakaoidhinishwa na kamati tendaji ya taifa kutokana na nyadhifa zao umuhimu wao kwa mkutano mkuu.

               (B) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA TAIFA
                            i.            kupokea/kujadili na kupitisha mihutasari  iliyopita
                          ii.            kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo nakutoa tathmini ya jumla ya shughuli za MSATEKU kwa mwaka uliopita
                        iii.            kuweka mpango kazi wa mwaka na mikakati kwa ajili ua mwaka unaofuata
                        iv.            kuchagua viongozi na wajumbe wa kamati tendaji wa ya MSATEKU
                          v.            kuidhinisha wajumbe wa sekretarieti ya taifa itakapobidi
                        vi.            kuidhinisha wajumbe na bodi ya madhamini
                      vii.            kupokea kujadili na kudhinisha mapendekezo au na mabadiliko ya katiba




SEHEMU YA NNE
      8.     IDARA ZA MSATEKU
      8.1.  IDARA YA ELIMU NA AMALI
          (a) KUTAKUWA NA KAMATI YA ELIMU NA AMALI ITAKUWA NA WAJUMBE
                WAFUATAO;
                  i.            mwenyekiti/amir wa idara
                ii.            katibu wa idara
              iii.            na wajumbe watatu wa kuteuliwa na kamati tendaji

            (b) KAZI NA MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU NA AMALI
                       i.            itakuwa idara ya kudumu inayoshughulikia masuala yote ya elimu
                     ii.            kutekeleza na kushughulikia maamuzi na maelekezo ya idara tendaji yanayohusu elimu
                   iii.            kupanga, kuratibu, kutekeleza, kusimamia na kuratibu mipango na miradi mbalimbali ya MSATEKU
       8.1.1. IDARA YA FEDHA UCHUMI NA MIPANGO
           (a) kutakuwa na kamati ya fedha, uchumi na mipango ya msateku itakayokuwa na wajumbe
                wafuatao:
                          i.            Mwenyekiti/amir wa idara
                        ii.            katibu wa idara
                      iii.            Mweka hazina
                      iv.            Wajumbe watatu wa kuteuliwa bna kamati tendaji.
            (b)  KAZI NA MAJUKUMU YA IDARA YA FEDHA NA UCHUMI
                            i.            Itakuwa kamati ya kudumu inayaowajibika na mipango hna maswala yote yahusuyo fedha
                          ii.            kukusanya michango ya wanachama kama michango ya wanachama kama itakavyokubaliwa na kamati tendaji
                        iii.            kukusanya zawadi zaka na sadaka
                        iv.            kuandaa, kuatekeleza, kusimamia na kuratibu na miradi mbalimbali ya MSATEKU
                          v.            kushughulikia uwekezeji katika milady uchumi na huduma za jamii.
                        vi.            kutoa mwongozo namaelekezo juu ya usimamizi matumizi na udhibiti wa fedha za MSATEKU katika ngazi zote
                      vii.            na kufanya shughuli nyingine zinazohusiana na masuala ya uchumi na fedha zilizo ndani ya misingi ya sheria   

        8.1.2. IDARA YA HABARI UHUSIANO NA USTAWI WA JAMII
        (a) KUTAKUWA NA IDARA YA HABARI UHUSIANO NA USTAWI WA
              JAMII ITAKAYOKUWA NA WAJUMBE    WAFUATAO;
                          i.            mwenyekiti /amir wa idara
                        ii.            katibu wa idara.
                      iii.            Wajumbe watatu wa kuteuliwa na kamati tendaji.
           (b)  KAZI NA MAJUKUMU YA IDARA
                  i.            kutekeleza maamuzi na kushughulika maelekezo ya kamati ya utendaji yanayohusu mahusiano na ustawi wa jamii
                ii.            kudumisha mawasiliano na mahusiano na serikali  na  asasi nyingine  za  ndani  na  zanje  za  nchi.
              iii.            kuweka  na  kuhifadhi kumbukumbu zote  zinazo husu wanajumuia
              iv.            kusimamia  na  kuratibu  masuara  yote  yanayohusiana na  teknolojia ya  habari na  mawasiliano

8.1.3        IDARA  YA WANAWAKE

(a)   KUTAKUWA  NA  KITENGO MAALUMU CHA WANAWAKE  CHA MSATEKU KITAKACHOUNDWA NA  WAJUMBE WAFUATAO
                     i.            amira wa idara au  kitengo
                   ii.            naibu  amira
                 iii.            katibu
                 iv.            naibu katibu 
                   v.            wajumbe watakao  teuliwa na  kamati kulingana  na  mahitaji

(b)   KAZI  ZA  IDARA AU KITENGO  CHA  WANAWAKE
             
  i.      kuratibu mambo  yote yanayowahusu wanachuo 
 ii.   kuelimisha wanawake  wakikslamu juu  ya hadhi  haki  na  wajibu wa wanawake wa kiislamu katika  jamii .
iii.  kubuni na kutuelekeza  shughuri ambazo zitajenga  mwamko  wakiislamu  kupitia mafundisho ya kijamii na  kiimani 
    iv.    kuwakilisha wasichana /wanachuo wakiislamu katika mabalaza  ya  wanawake ya taifa na kimataifa


SEHEMU YA TANO

  9.   KANUNI NA TARATIBU ZA VIKAO
   
 9.1. KANUNI ZA VIKAO
                i.            mkutano wa msateku utaitishwa na  kamati  tendaji, ngazi husika
              ii.            kikao  chochote cha  msateku  kitakuwa halali kama kitaudhuriwa na wajumbe husika kwa mujibu  wa katiba  hii
    
9.1.1.  TARATIBU ZA VIKAO
           i.            mkutano  mkuu wa msateku wakawaida utafanyika mara  moja kwa mwaka
         ii.            mkutano mkuu wadharura unaweza kufanyika   wakati  wowote itakapohitajika kwa sharti la kutimia theluthi( 1/3 )   ya wajumbe wote
       iii.            vikao  vya  kamati  tendaji vitafanyika kila baada ya  wiki mbili au  wakati wowote ikitokea dharura
   
  9.1.2. MAHUDHURIO

Akidi ya kikao Na mkutano wa msateku itakuwa nusu ( 1/2  ) ya idadi ya wajumbe halali wakikao au mkutano usiku isipokuwa pale inapoelekezwa vinginevyo na katika hii
  
  9.1.3.  UAMUZI
       i.   uamuzi katika vikao au mkutano  utafikiwa kwa njia ya makubaliano ya wajumbe  au kwa wingi  wakura
      ii.   endapo idadi  ya  kura zitalingana amiri  atakuwa na kura ya  ziada ya  uamuzi
    iii.    maamuzi  yote  ya  kikao lazima yawe katika misingi ya  Quru-an na sunnah
                                  

                                              SEHEMU YA  SITA

10. SIFA ZA  VIONGOZI ,MUDA , NA TARATIBU ZA UTEUZI

10.1. SIFA ZA VIONGOZI
        i.            Awe muislamu mcha Mungu
      ii.             awe mwenye elimu
    iii.             awe mwenye tabia njema
    iv.            awe mwenye afya njema

10.1.1.  MUDA WA UONGOZI
           i. viongozi wote wa kuchaguliwa au kuteuliwa  watadumu katika uongozi kwa kipindi cha miaka miwili na wanaweza kuteuliwa tena kwa kipindi  kingine cha uongozi
         ii.            viongozi wakuajiliwa watashika mdaraka kulingana na masharti  na maelekezo  ya mikataba yao

10.1.2. TARATIBU  ZA  UCHAGUZI AU  UTEUZI
        i.            tume ya  uchaguzi itauhusu ngazi ya tawi wilaya na mkoa
      ii.            katika ngazi ya msateku t aifa, sekretarieti ya  MSATEKU itakuwa tume
10.1.3.  UTARATIBU WA UCHAGUZI
    
    i.  wana msateku ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa ngazi husika watapendekeza  majina ya wagombea kwakuzingatia ( ibara 10 .1 ) na si kujipendekeza wenyewe.
      ii.  tume ya uchaguzi ya ngazi husika inaweza kupendekekeza jina au  majina kama itakuwa hapana budi kufanya hivyo
    iii. wajumbe wote watapiga kura kuchagua viongozi wa MSATEKU katika ngazi  husika
    iv.   tume ya uchaguzi itakayo undwa itakuwa na wajibu wa kusimamia uchaguzi

10.1.4. CHAGUZI WA MKOA

        i.  kila chuo kitapendekeza majina ya wagombea kwa kuzingatia ( ibara 10.1 ) lakini majina au wagombea wawe wanapendekezwa na si kujipendekeza wenyewe.
      ii.   kamati ya uchaguzi ya mkoa inaweza kupendekeza majina au jina kama itakuwa hakuna budi kufanya hivyo.
    iii. wawakilishi wote waislamu chuoni watapiga kura kuchagua viongozi wa mkoa
    iv.   kamati (tume ) ya chaguzi itakayoundwa au sekretalieti ya mkoa itakuawa na wajibu wakusimamia uchaguzi

SEHEMU  YA SABA

10. VIONGOZI
10:1 WAFUATAO WATAKUWA VIONGOZI WA MSATEKU
      
  i.      rais ( amir )  au mwenyeketi
  ii.      makamu wa rais ( naibu amir )
iii.     katibu  mkuu
 iv.   naibu katibu mkuu
 v.   katibu mtendaji
 vi.     amirati
vii.     naibu amirati
viii.   wakuu wa kamati au idara

    ix.    mlezi

10.1.2 KAZI YA MAMLAKA YA VIONGOZI RAIS WA MSATEKU ( MWENYEKITI )
    
     i.            atakuwa  msemaji mkuu wa msateku
       ii.             atakuwa kiongozi na msimaizi mkuu wa shughuri zote za msateku
     iii.            at aongoza au atasiamia mikutano yote ya kamati na mkutano mkuu
     iv.            atapendekeza ajenda za mikutano

10.1. 3 MAKAMU WA RAIS (MAKAMU MWENYEKITI )
   
     i.   atatekeleza majukumu kama atakavyotakiwa kufanya  na rais
      ii.   atatekeleza majukumu ya rais ( mwenyekiti)  pindi rais asipokuwepo

10.1.4  KATIBU MKUU
    
    i.      atakuwa mtendaji mkuu wa msateku
      ii.       atatoa taarifa ya vikao vyote vya kamati tendaji ya mkutano  mkuu
    iii.       atakuwa katibu wamikutano yote ya kamati tendaji
    iv.       ataunda kamati  tendaji maalumu nakufafanua kazi na muda wake wa utekelezaji
      v.       atatoataarifa za shughughri za MSATEKU  kwa kamati tendaji mara mbili  kwa mwaka
    vi.       atapokea  taarifa za  utendaji za mikoa nakuandaa taarifa ya utendaji ya MSATAEKU taifa

10.1.5 NAIBU KATIBU MKUU

        i.            atatekeleza mjukumu kama atakavyo takiwa kufanya na katibu
      ii.             atatekeleza majumu ya katibu pindi  asipokuwepo

10.1.6.  KATIBU MTENDANDAJI

       i.            atatekeleza shughuli za kila sikuza msateku
      ii.            atashugulikia mawasiliano nataarifa z amsateku katika matawi
    iii.            atasiadiana na katibu mkuu katika kutekelezamajukumu yake
    iv.            atekeleza majukumu  mengine atakayopangiwa na mwenyekiti

10.1.7 AMIRA WA  MSATEKU
      
  i.            atakuwa msemaji  mkuu wa kitengo cha wanawake
      ii.            atakuwa msimamizi  wa maswala ya husuyo wanawake au wanachuo  wa kike
    iii.            atasimamia na kuongoza vikao vyote  vya vitengo cha wanachuo wanawake
    iv.            atahakikisha  malengo  ya kitengo cha wana chuo wanawake yanafikiwa

10.1.8.  NAIBU  AMIRA WA TAIFA

        i.            atasaidiana na amirah katika kutekeleza mjukumu yote yake 
      ii.            atakaimu nafasi ya amira asipokuwepo

10.1.9.  WENYE VITI WA   VITENGO AU IDARA ZA MSATEKU
     
    i.            kuendesha vikao vyote vya vitengo au  idara zao
       ii.            watawajibika na majukuimu yote kwmujibu wa idara zao ‘

10.2. MAKATIBU WAKAMATI AU VITENGO IDARA KUU ZA MSATEKU

a.       katibu wa elimu na amali
        i.            atakuwa afisa taaluma wa  msateku katka  ngazi husika
      ii.            atawajibika  kwa mipamgo  yote  ya fedha na  uchumi  wa jumia

b.      KATIBU  WAHABARI  NA  MAHUSIANO NA  USTAWI  WA JAMII WA MSATAEKU

        i.            atakuwa afisa uhusiano na ustawi wa jamii
      ii.            atawajibika na maswala yote ya habari mahusiano na ustawi  wa jamii ya MSATEKU

c.        KATBU WA FEDHA

        i.            atkuawa ndio  msimamizi wa muweka hazina ( mhasibu ) wa jumia
      ii.            atawajibika kwa mipango yote ya fedha na uchumi ya jumuiya.

d.      KATIBU  WA  IDARA  YA WANAWAKE

       i.            ndiye Mtendaji mkuu wa kitenfo cha wanawake wa kushirikiana na amirah na naibu Amirah
      ii.            atawajibika kuratibu utekelezaji wa majukumu ya kitengo    cha wanawake cha MSTATEKU katika ngazi zote


SEHEMU YA NANE

11. KANUNI ZA NIDHAMU

        i. wanachama na viongozi wote wa MSATEKU wanatarajiwa kuwa waislam wema na wenye kuzingatia kwa makini maadili ya kiislam na maagizo ya kidini
      ii.   uvunjaji wowote wa dhahiri wa ibara ndogo hapo juu utachukuliwa hatua kali za kinidhamu na mamlaka husika
   iii hatua za kinidhamu zitakazochukuliwa ni kuanzia onyo kali kusimamishwa kwa muda au kufukuzwa kabisa
    iv.  hatua zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote anayevunja katiba hii au ambaye matendo yake mabaya yameathiri MSATEKU
    v. mtu ambaye hatua za kinidhamu zinatakiwa kuchukuliwa dhidi yake atapewa muda muafaka wa kujitetea
      vi.   kutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa vyombo vya juu lakini kamati tendaji itakuwa ni chombo cha mwisho ca rufaa ba maamuzi yake hayatatakiwa rufaa zaidi ya hapo

SEHEMU YA TISA.

 12.       MAREKEBISHO YA KATIBA/ RASIMU.

12.1.   Katiba hii na seheme yake nyingine yoyote haitabadilishwa au kurekebishwa
            isipokuwa kwa idhini ya zaidi ya nusu ya wanajumuiya wote wa mkutano mkuu wa MSATEKU

12.1.1. Pendekezo au mapendekezo au mapendekezo ya kurekebisha katiba hii yatawasilishwa
              itakayowasilishwa kwa bodi ya wadhamini kwa majadiliano na mapendekezo kamati tendaji
              itasambaza mapendekezo miongoni mwa wanajumuia ili kuyatathmini miezi matatu kabla ya
               mkutano mkuu

12.1.2.  Kamati tendaji itawakilisha kwa mkutano mkuu marekebisho yaliyopendekezwa pamoja
              na sababu za msingi na pia mapendekezo [ushauri] ya bodi ya wadhamini
12.1.3.  Marekebisho yatawasilishwa kwa bodi ya wadhamini baada ya kukubaliwa katika kikao
              rasmi cha mkutano mkuu


SEHEMU YA KUMI.

13. MENGINEYO

        i.      Kura zote zinazohusu uchaguzi zitapigwa kwa siri
      ii.       Wanajumuiya hai ndiye atakayehudhura vikao vinavyohusiana kuwa na haki ya kupiga kura
    iii.        Watumishi wa jumuiya hawatakuwa na  haki ya kupiga kura katika vikao vyote vya jumuiya
    iv.        Kutakuwa na kanuni za jumuiya ambazo zitaenda sambamba na katiba ya jumuiya pale ambapo patakuwa na utatanishi katiba itatawala /itaamua
      v.        Muda wa kukaimu utakuwa si zaidi ya miezi kumi na mbili
    vi.        Rasimu hii ya katibu na itaanza kutumika baada ya kupitiwa na wana jumuiya katika mkutano mkuu wa msateku   

                                   
















Imeandaliwa na
Buda M.P

3 comments:

  1. AWW,nimesoma nimeelewa na pendekeza mngeviacha vipengele vya wilaya

    ReplyDelete
  2. A.ALYKM, katika SEHEMU YA NNE ya katiba , PAMEORODHESHWA IDARA TATU ZA MSATEKU, IDARA YA ELIMU, HABARI NA UCHUMI. vipi kuhusu idara ya DA'AWA NA MAADILI, ikizingatiwa ndio msingi wa jumuiya kwani lengo la kukusanyana ni kutaka watu waishi kwa maadili ya kiislamu.UFAFANUZI

    ReplyDelete
  3. AWW tuliopita tungependa suala la maadili liwekewe highlight, ndio chanzo cha kuendesha jumuiya kwa ufasaha

    ReplyDelete