NDUGU ZANGU IFAHAMIKE YA KWAMBA JUMUIYA BILA KATIBA ITAKUWA VIGUMU SANA KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA JUMIYA YETU, PIA IFAHAMIKE KWAMBA KATIBA HII IMEUNDWA KWA KUTUMIA KATIBA KUU YA TAMSYA NA PIA IFAHAMIKE YOTE AMBAYO YAMEPENDEKEZWA HAYAPO KINYUME NA QUR'AN NA SUNNAH.
RASIMU
YA KATIBA YA JUMUIA YA WANAFUNZI WA KIISLAM
CHUO
KIKUU TEOFILO KISANJI
Anwani ya jumuiya
2014
YALIYOMO
SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
Kifungu……………………………………………………………………………………………….1
1. Jina…………………………………………………………………………………………………....1
2. Anwani………………………………………………………………………………………………..1
3. Motto………………………………………………………………………………………………….1
4. Madhumuni…………………………………………………………………………………………....1
5. fasili
/ufafanuzi………………………………………………………………………………………....1
SEHEMU YA PILI
6.1.UANACHAMA WA MSATEKU UTAKUWA WA AINA MBILI……………………………….2
i.
Uanachama wa asili………………………………………………………2
ii. Uanachama
wa heshima………………………………………………….2
6.1.1UANACHAMA WA ASILI…………………………………………………………………….2
6.1.2.UANACHAMA WA
HESHIMA………………………………………………………………2
6.1.3.HAKI NA WAJIBU WA
MWANACHAMA………………………………………….……….2
6.1.4.KUJIANDIKISHA
KUWA MWANACHAMA KAMILI……………………………………..2
6.1.5.UKOMO WA
MWANACHAMA…………………………………………………………......2
6.1.6.MAADILI UA
MWANACHAMA…………………………………………………………….2
SEHEMU YA TATU
7. BODI YA
MSATEKU/WADHAMINI……………………………………………………………3
7.2.MATAWI YA MSATEKU………………………………………………………………….……3
7.3.UWAKILISHI……………………………………………………………………………….......3
7.3.1 MKUTANO MKUU WA
TAWI…………………………………....…………………………3
7.4.MKUTANO MKUU WA
WILAYA……………………………………………………………..3
7.5.MKUTANO MKUU WA
MKOA……………………………………………...………………..3
7.6. MKUTANO MKUU WA
TIFA...……………………………………………………………….4
SEHEMU YA NNE
8. IDARA ZA MSATEKU…………………………………………………………………………...5
8.1.IDARA YA ELIMU NA
AMALI………………………………….……………………………..5
8.1.1.IDARA YA
FEDHA,UCHUMI NA AMALI……………………………..…………………….5
8.1.2.IDARA YA
HABARI,UHUSIANO NA USTAWI WA JAMII…………………………………6
8.1.3.IDARA YA WANAWAKE……...………………………………………………………………6
SEHEMU YA TANO
9.KANUNI NA TARATIBU ZA
VIKAO…………………..………………………………………...6
9.1.KANUNI ZA VIKAO……………………………………………………………………………6
9.1.1.TARATIBU ZA VIKAO……………………………………..………………………………….6
9.1.2. MAHUDHURIO……………………………………………………………………………….6
SEHEMU YA SITA
10.SIFA ZA
VIONGOZI,MUDA NA TARATIBU ZA UTEUZI……………………………………...6
SEHEMU YA SABA.
11.VIONGOZI………………………………………………………………………………………..7
11.1 KAZI NA MAMLAKA YA
VIONGOZI………………………………………………..……….7
SEHEMU YA NANE
12-KANUNI NIDHAMU…………………………………………………………………………….8
SEHEMU YA TISA
13.MAREKEBISHO YA
KATIBA……………………………………………………….…………..8
SEHEMU YA KUMI
14.MENGINEYO…………………………………………………………………………………….9
SEHEMU YA KWANZA
1. JINA:
JUMUIYA YA KIISLAM YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI
2. ANWANI
MWENYEKITI/AMIR
JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAM,
CHUO KIKUU
TEOFILO KISANJI
HALMSHAURI YA JIJI ,MBEYA
S.L.P
MBEYA.
3.
MOTTO
WA JUMUIYA:
4.
MADHUMUNI.
i)
kukuza ufahamu wa wanachuo na vijana juu
ya uislamu na kutoa ufumbuzi wa kiislam kwa matatizo ya jamii ya sasa na ijayo .
ii) kusaidia
wanafunzi na vijana kujenga hulka ya kiislam kwa kutumia mafunzo ya kimaadili
,kiitikadi na kijamii .
iii) kukuza
moyo wa kindugu wa kiislam na ushirikiano na jumuiya nyingine zenye shabaha na
madhumuni kama msateku.
iv) kuwaunganisha
vijana na wanachuo katika kupambana na majamga yanayoikabili jamii.
v) kuwakilisha
wanachuo na vijana wa kiislam.Tanzania katika vikao vya kutaifa na kimataifa.
vi) kushirikiana
na jumuiya nyingine za kijamii kiserikali,kidin,kitaifa,na kimataifa katika kuiletea
maendeleo jamii na taifa kwa ujumla.
vii) kusimamia,kulinda
na kutetea haki za vijana nawanafunzi wa kiislam Tanzania.
viii.
kuendesha na kusimamia miradi ya
maendeleo ya huduma za jamii na kumiliki mali zinazohamishika na
zisizohamishika.
ix.
kujitolea kufanya kazi nyingine zenye
maslahi kwa wanachuo na wanafunzi wa kiislam na jamii kwa ujumla .
5.
FASILI/UFAFANUZI.
i. mahali popote ambapo maneno yanayotamkwa
chini yametumika katika katiba hii,yana maana au ufafanuzi au fasili
iliyotolewa juu yake ama iliyotolewa kishera iwapo pana sheria yoyote nchini
kuhusiana nayo:
ii. bodi ya wadhamini chombo cha wadhamini
wa jumuiya cheye wajumbe watano.
iii. jumuiya-ni mkusanyiko wa wanachuo wenye
lengo la kuendeleza na kustawisha zaidi maadili na maendeleo ya uislam.
iv kanuni-taratibu zinazoitafsiri katiba ya
kutoa mwongozo wa kutekeleza katiba ya jumuiya
SEHEMU YA PILI
6.
UANACHAMA
WA MSATEKU
i)
uanachama wa asili
ii) uanachama
wa heshima
6.1. UANACHAMA WA ASILI
-
utakua wazi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu
na taasisi mlezi.
-
mwanachuo wa kiislam kwa kulipa ada ya
wanachama,uanachama wa mwanachuo ni wa mtu mmoja mmoja
6.1.1.
UANACHAMA
WA HESHIMA
uanachama waheshima
utakuwa wazi kwa mtu yeyote bila kujali umri au jinsia kwa mtu yeyote bila
kujali umri au jinsia atakayependekezwa na kamati tendaji ya msateku wilaya,mkoa
au taifa na kuidhinishwa na kamati tendaji ya msateku taifa na atateuliwa
kutokana na umuhimu wake katika jumii kwa kulinda maslahi ya msateku.
6.1.2.
HAKI
NA WAJIBU WA MWANACHAMA WA ASILI
i)
kushiriki katika vikao vyote halali
vinavyomhusu.
ii) kushiriki
katika shughuli za jumuiya za kila siku kwa mujibu wa kanuni na taratibu
iii) kupendekeza
au/ na kuchagua viongozi wa jumuiya
iv) kupendekezwa
au/ na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa jumuiya
v) kushiriki
katika kamati za jumuiya kwa majibu wa kanuni na taratibu
vi) kujua
namna jumuiya inavyoendeshwa
vii) kuhoji
au /na kukosoa [ikibidi]uendeshwaji wa jumuiya kwa maslaha ya jumuiya na uislam
viii)
kushirikiana na viongozi pamoja na wanachama
wengine katika kufanya maamuzi inapobidi
6.1.3.
KUJIANDIKSHA
KUWA MWANAJUMUIYA /MWANCHAMA KAMILI
mwanajumuiya ataorodheshwa katika daftari
kuu la jumuiya kwa jina kamili na taarifa nyingine zinazomhusu mwanajumuiya.
6.1.4.
UKOMO
WA MWANAJUMUIYA/MWANACHAMA
i)
hakutoa ada yake kwa kipinde cha
semester nzima.
ii) akijitoa
katika jumuiya.
iii) akishindwa
kutimiza maadili ya jumuiya kwa mfano ulevi,uzinzi,wizi,kashfa,usengenyaji.
iv) akifariki
dunia .
v) mwanajumuiya
akikomaa uanachama hatorudishiwa ada zake.
6.1.5.
MAADILI
YA MWANAJUMUIYA
i)
mwajumuiya ni lazima azingatie maadili
yaliyoandikwa katika vitabu vyetu vitakatifu Qurani na hadithi zaMtumeMohamad[S.A.W]
SEHEMU
YA TATU
7.
BODI
YA MSATEKU/WADHAMINI
7.1. kutakuwepo
na bodi ya wadhamini ambayo itajulikana katika Katiba hii kama bodi itakayoundwa na kamati tendaji ya MSATEKU
taifa kwa kushauriana na sekretariati ya MSATEKU taifa na muda wake utakuwa ni
miaka miwili [2]
i.
bodi itajumuisha wajumbe watano,watatu
kati yao wataidhinishwa na mkutano mkuu,katibu mkuu na katibu mtendaji wataingia
kwa nafasi zao.
ii.
bodi itaweka sera ya jumuiya ya MSATEKU kusimamia
shughuli zake na kuweka juhudi katika kufikia madhumuni ya MSATEKU
iii.
bodi ndiyo msimamizi mkuu wa mali na
amana za MSATEKU
iv.
bodi itawakilisha jumuiya katika masuala
yate ya kisheria na mikataba.
v.
bodi itakua na haki ya kukopa na
kukopeshwa na kukopesha na kukopesheka kwa niaba ya [MSATEKU]
vi.
katika mkutano wake wa kwanza bodi
itamchagua mmoja wa wajumbe wake kati ya waliochaguliwa na mkutano mkuu kuwa
mwenyekiti.
vii.
katibu mtendaji atakuwa katibu wa kudumu
wa bodi
viii.
akidi ya mkutano wa bodi ya wadhamini haitopungua
idadi ya wajumbe 3 na uamuzi wake utapitishwa ikiwa utakubalika na zaidi ya
nusu ya wajumbea waliohudhuria mkutano . maamuzi yote katika bodi yatafuata
misingi ya Quar-an na sunnah za
mtume [s.a.w]
ix.
maamuzi yote katika bodi yatafuata
misingi ya Qur-an na sunnah za Mtume[S.A.W]
7.2. MATAWI YA MSATEKU
i.
kila chuo au asasi mwanachama wa MSATEKU
itakuwa ni tawi la MSATEKU
ii.
matawi yaliyotajwa kifungu 7.2[ i.]
yataunda MSATEKU ngazi ya wilaya
iii.
MSATEKU wilaya zitaunda MSATEKU mkoa
iv.
MSATEKU Ngazi ya mkoa zitaunda MSATEKU
taifa.
7.3. UWAKILISHI
7.3.1.
(a).
MKUTANO MKUU WA TAWI
i.
Mwenyekiti wa MSATEKU wa tawi
ii.
Makamu mwenyekiti wa tawi
iii.
katibu wa tawi
iv.
Naibu katibu wa tawi
v.
Wakuu na makatibu wa Idara/kamati za
MSATEKU wa tawi
vi.
Mwanachuo wote wa kiislam tawini
vii.
Mlezi wa MSATEKU tawini
(b) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA TAWI
i.
kupokea kujadili na kupitisha mihutasari
ya mikutano iliopita
ii.
kupokea,kujadili na kupitisha taarifa za
maendeleo ya MSATEKU Tawini
iii.
kupokea, kujadili na kupitisha taarifa
za maendeleo ya MSATEKU tawini
iv.
kuzungumza masuala yenye manufaa kwa
tawi nakuyatolea mapendekezo yake katika kamati ya utendaji ya tawi na wilaya
v.
kuchagua viongozi wa kamati ya utendaji ya
tawi
(c) KAMATI TENDAJI YA TAWI
i.
mwenyekiti wa tawi
ii.
makamu mwenyekiti wa tawi
iii.
katibu wa tawi
iv.
Naibu katibu wa tawi
v.
mweka hazina wa tawi
vi.
wakuu, makatibu wakuu na wajumbe wa
kamati au idara za MSATEKU katika tawi husika
(d) KAZI ZA KAMATI TENDAJI YA
TAWI
i.
kutekeleza mikatakati/mipango naahughuli
za msateku katika tawi
ii.
kutoa ripoti ya jumla ya maendeleo uya
shughuli za msateku kwenye mkutano mkuu wa tawi
iii.
kutekeleza mikakati mipango na maazimio
ya mkutano mkuu wa tawi
7.3.2. MKUTANO MKUU WA WILAYA
(a) KUTAKUWA NA
MKUTANO MKUU WA WILAYA UTAKAOHUDHURIWA NA:
i.
mwenyekiti na MSATEKU wilaya
ii.
makamu mwenyekiti wa MSATEKU wilaya
iii.
katibu wa MSETEKU wilaya
iv.
naibu katibu mtendaji wa MSATEKU wilaya MSATEKU
wilaya
v.
katibu mtendaji wa MSATEKU wilaya
vi.
mweka hazina na msaidizi wake wa msateku
wilaya
vii.
wenyeviti makamu wenyeviti na makatibu
wa idara au kamati za MSATEKU wilaya
viii.
Wakuu na makatibu wa idara au kamati za
MSATEKU wilaya
ix.
mlezi wa MSATEKU wilaya
x.
Mwenyekiti na Amira kutoka kila tawi ni
MSATEKU
(b) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA
WILAYA
i.
kupokea,kujadili na kupitia mihutasari
iliyopita
ii.
kupokea,kujadili nakupitisha taarifa za maendeleo
ya msateku wilaya
iii.
kuchagua viongozi wa kamati ya utendaji
msateku ngazi ya wilaya
iv.
Itapokea mipango,maazimio na mikakati na
maagizo ya mkutano mkuu wa mkoa na taifa kwa utekelezaji
(c)
KAMATI
TENDAJI YA MSATEKU WILAYA
i.
Mwenyekiti wa wilaya
ii.
Makamu mwenyekiti wa wilaya
iii.
katibu wa wilaya
iv.
Naibu katibu wa wilaya
v.
mweka hazina wa wilaya
vi.
wakuu,makatibu na wajumbe wa kamati au
idara za MSATEKU wilaya
(d)
KAZI
ZA KAMATI TENDAJI YA MSATEKU
i.
Kupokea,kujadili na kupisha mihutasari
ya mikutano iliyopita.
ii. kitakuwa ndicho chombo
kitakachoshughulika na kazi za kila siku za MSATEKU wilaya
iii.
Itatoa taarifa ya shughuli za MSATEKU
wilaya katika mkutano mkuu wa wilaya
iv.
itapokea mipango ,maazimio na mikakati
na /au maagizo ya mkutano mkuu wa wilaya na mkoa
7.3.3. MKUTANO MKUU WA MKOA
(a) KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU
WA MKOA UTAKAO HUDHURIWA NA
i.
Mwenyekiti MSATEKU mkoa
ii.
Makamu mwenyekiti MSATEKU mkoa
iii.
Katibu MSATEKU mkoa
iv. Naibu katibu MSATEKU mkoa
v.
Katibu mtendaji wa MSATEKU
vi. Wenyeviti,makatibu wa idara ,kamati za
MSATEKU mkoa
vii.
mweka hazina wa MSATEKU wa mkoa
viii. Mwenyekiti,Amira na wajumbe watatu
kutoka kila wilaya
ix.
mlezi wa MSATEKU wa mkoa
(b) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA MKOA
i.
Kupokea,kujadili na kupitisha mihutasari
ya mkutano iliyopita ya mkoa husika
ii.
kupokea,kujadili na kupitisha taarifa za
maendeleo ya MSATEKU mkoa
iii.
kuidhinisha uteuzi wa mlezi wa mkoa
iv.
kuchagua viongozi wa kamati tendaji ya
MSATEKU ngazi ya mkoa
v.
kuchagua wajumbe watatu watakaoungana na
mwenyekiti na Amira kuwakilisha mkoa katika mkutano mkuu wa MSATEKU taifa
(c)
KAMATI
TENDAJI YA MSATEKU MKOA
i.
Mwenyekiti MSATEKU
mkoa
ii.
Makamu mwenyekiti MSATEKU wa mkoa
iii.
katibu MSATEKU wa mkoa
iv.
Naibu katibu MSATEKU wa mkoa
v.
katibu wa mtendaji MSATEKU wa mkoa
vi.
wakuu,makatibu na wajumbe wa
kamati,idara za MSATEKU mkoa
(d) KAZI ZA KAMATI TENDAJI MSATEKU MKOA
i.
Kupokea,kujadili na kupitisha miutasari
ya mkutano uliopita
ii.
Iitakuwa ndicho chombo
kitakachoshughulikia na kazi za kila sikauy za MSATEKU mkuu
iii.
itatoa taarif ya shughuli za MSATEKU
mkoa katika mkutano mkuu wa mkoa
iv.
Itapokea mipango, maazimio na miakati na
au maagizoya mkutano mkuu wa mkoa na taifa kwa utekelezaji
7.3.4
MKUTANO MKUU WA TAIFA
(a) KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU WA TAIFA NA
MSATEKU MKUTANO MKUU
UTAKAOJUMUISHA;
i.
Rais/amir wa MSATEKU taifa
ii.
makam rais/naibu amir WAMSATEKU taifa
iii.
katibu mkuu wa MSATEKU taifa
iv.
Naibu katibu MSATEKU taifa
v.
Amira wa MSATEKU taifa
vi.
Katibu mtendaji wa MSATEKU taifa.
vii.
wajumbe wote wa kamati tendaji ya
MSATEKU taifa
viii.
wajumbe watano kutokaa kila mkoa
ix.
Wajumbe wengine kutoka ngazi mbalimbali
watakaoidhinishwa na kamati tendaji ya taifa kutokana na nyadhifa zao umuhimu
wao kwa mkutano mkuu.
(B) KAZI ZA MKUTANO MKUU WA TAIFA
i.
kupokea/kujadili na kupitisha
mihutasari iliyopita
ii.
kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo
nakutoa tathmini ya jumla ya shughuli za MSATEKU kwa mwaka uliopita
iii.
kuweka mpango kazi wa mwaka na mikakati
kwa ajili ua mwaka unaofuata
iv.
kuchagua viongozi na wajumbe wa kamati
tendaji wa ya MSATEKU
v.
kuidhinisha wajumbe wa sekretarieti ya
taifa itakapobidi
vi.
kuidhinisha wajumbe na bodi ya madhamini
vii.
kupokea kujadili na kudhinisha
mapendekezo au na mabadiliko ya katiba
SEHEMU YA NNE
8. IDARA ZA MSATEKU
8.1. IDARA YA ELIMU NA AMALI
(a) KUTAKUWA NA KAMATI YA ELIMU NA
AMALI ITAKUWA NA WAJUMBE
WAFUATAO;
i.
mwenyekiti/amir wa idara
ii.
katibu wa idara
iii.
na wajumbe watatu wa kuteuliwa na kamati
tendaji
(b)
KAZI NA MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU NA AMALI
i.
itakuwa idara ya kudumu inayoshughulikia
masuala yote ya elimu
ii.
kutekeleza na kushughulikia maamuzi na
maelekezo ya idara tendaji yanayohusu elimu
iii.
kupanga, kuratibu, kutekeleza, kusimamia
na kuratibu mipango na miradi mbalimbali ya MSATEKU
8.1.1. IDARA YA FEDHA UCHUMI NA MIPANGO
(a)
kutakuwa na kamati ya fedha, uchumi na mipango ya msateku itakayokuwa na
wajumbe
wafuatao:
i.
Mwenyekiti/amir wa idara
ii.
katibu wa idara
iii.
Mweka hazina
iv.
Wajumbe watatu wa kuteuliwa bna kamati
tendaji.
(b) KAZI NA MAJUKUMU YA IDARA YA FEDHA NA UCHUMI
i.
Itakuwa kamati ya kudumu inayaowajibika
na mipango hna maswala yote yahusuyo fedha
ii.
kukusanya michango ya wanachama kama
michango ya wanachama kama itakavyokubaliwa na kamati tendaji
iii.
kukusanya zawadi zaka na sadaka
iv.
kuandaa, kuatekeleza, kusimamia na
kuratibu na miradi mbalimbali ya MSATEKU
v.
kushughulikia uwekezeji katika milady
uchumi na huduma za jamii.
vi.
kutoa mwongozo namaelekezo juu ya
usimamizi matumizi na udhibiti wa fedha za MSATEKU katika ngazi zote
vii.
na kufanya shughuli nyingine zinazohusiana
na masuala ya uchumi na fedha zilizo ndani ya misingi ya sheria
8.1.2. IDARA YA HABARI UHUSIANO NA USTAWI WA
JAMII
(a) KUTAKUWA NA IDARA YA HABARI
UHUSIANO NA USTAWI WA
JAMII ITAKAYOKUWA NA WAJUMBE WAFUATAO;
i.
mwenyekiti /amir wa idara
ii.
katibu wa idara.
iii.
Wajumbe watatu wa kuteuliwa na kamati
tendaji.
(b)
KAZI NA MAJUKUMU YA IDARA
i.
kutekeleza maamuzi na kushughulika maelekezo
ya kamati ya utendaji yanayohusu mahusiano na ustawi wa jamii
ii.
kudumisha mawasiliano na mahusiano na
serikali na asasi nyingine za
ndani na zanje
za nchi.
iii.
kuweka
na kuhifadhi kumbukumbu zote zinazo husu wanajumuia
iv.
kusimamia na
kuratibu masuara yote
yanayohusiana na teknolojia
ya habari na mawasiliano
8.1.3
IDARA YA WANAWAKE
(a)
KUTAKUWA NA
KITENGO MAALUMU CHA WANAWAKE CHA
MSATEKU KITAKACHOUNDWA NA WAJUMBE WAFUATAO
i.
amira wa idara au kitengo
ii.
naibu
amira
iii.
katibu
iv.
naibu katibu
v.
wajumbe watakao teuliwa na
kamati kulingana na mahitaji
(b)
KAZI ZA
IDARA AU KITENGO CHA WANAWAKE
i.
kuratibu mambo yote yanayowahusu wanachuo
ii. kuelimisha wanawake wakikslamu juu ya hadhi
haki na wajibu wa wanawake wa kiislamu katika jamii .
iii.
kubuni na kutuelekeza shughuri ambazo zitajenga mwamko
wakiislamu kupitia mafundisho ya
kijamii na kiimani
iv.
kuwakilisha wasichana /wanachuo
wakiislamu katika mabalaza ya wanawake ya taifa na kimataifa
SEHEMU
YA TANO
9. KANUNI
NA TARATIBU ZA VIKAO
9.1. KANUNI ZA VIKAO
i.
mkutano wa msateku utaitishwa na kamati
tendaji, ngazi husika
ii.
kikao
chochote cha msateku kitakuwa halali kama kitaudhuriwa na wajumbe
husika kwa mujibu wa katiba hii
9.1.1. TARATIBU ZA VIKAO
i.
mkutano
mkuu wa msateku wakawaida utafanyika mara moja kwa mwaka
ii.
mkutano mkuu wadharura unaweza kufanyika wakati
wowote itakapohitajika kwa sharti la kutimia theluthi( 1/3
)
ya wajumbe wote
iii.
vikao
vya kamati tendaji vitafanyika kila baada ya wiki mbili au
wakati wowote ikitokea dharura
9.1.2. MAHUDHURIO
Akidi ya kikao Na mkutano wa msateku itakuwa nusu (
1/2
) ya idadi ya wajumbe halali wakikao au mkutano usiku isipokuwa pale
inapoelekezwa vinginevyo na katika hii
9.1.3. UAMUZI
i. uamuzi katika vikao au mkutano utafikiwa kwa njia ya makubaliano ya
wajumbe au kwa wingi wakura
ii. endapo idadi ya
kura zitalingana amiri atakuwa na
kura ya ziada ya uamuzi
iii. maamuzi
yote ya kikao lazima yawe katika misingi ya Quru-an na sunnah
SEHEMU
YA SITA
10.
SIFA ZA VIONGOZI ,MUDA , NA TARATIBU ZA
UTEUZI
10.1.
SIFA ZA VIONGOZI
i.
Awe muislamu mcha Mungu
ii.
awe mwenye elimu
iii.
awe mwenye tabia njema
iv.
awe mwenye afya njema
10.1.1.
MUDA WA UONGOZI
i.
viongozi wote wa kuchaguliwa au
kuteuliwa watadumu katika uongozi kwa
kipindi cha miaka miwili na wanaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine cha uongozi
ii.
viongozi wakuajiliwa watashika mdaraka
kulingana na masharti na maelekezo ya mikataba yao
10.1.2.
TARATIBU ZA
UCHAGUZI AU UTEUZI
i.
tume ya
uchaguzi itauhusu ngazi ya tawi wilaya na mkoa
ii.
katika ngazi ya msateku t aifa, sekretarieti
ya MSATEKU itakuwa tume
10.1.3.
UTARATIBU WA UCHAGUZI
i.
wana msateku ambao ni wajumbe wa mkutano
mkuu wa ngazi husika watapendekeza
majina ya wagombea kwakuzingatia ( ibara 10 .1 ) na si kujipendekeza
wenyewe.
ii. tume ya uchaguzi ya ngazi husika inaweza
kupendekekeza jina au majina kama itakuwa
hapana budi kufanya hivyo
iii.
wajumbe wote watapiga kura kuchagua
viongozi wa MSATEKU katika ngazi husika
iv.
tume ya uchaguzi itakayo undwa itakuwa
na wajibu wa kusimamia uchaguzi
10.1.4.
CHAGUZI WA MKOA
i. kila chuo kitapendekeza majina ya
wagombea kwa kuzingatia ( ibara 10.1 ) lakini majina au wagombea wawe
wanapendekezwa na si kujipendekeza wenyewe.
ii.
kamati ya uchaguzi ya mkoa inaweza
kupendekeza majina au jina kama itakuwa hakuna budi kufanya hivyo.
iii. wawakilishi wote waislamu chuoni
watapiga kura kuchagua viongozi wa mkoa
iv. kamati (tume ) ya chaguzi itakayoundwa
au sekretalieti ya mkoa itakuawa na wajibu wakusimamia uchaguzi
SEHEMU YA SABA
10.
VIONGOZI
10:1
WAFUATAO WATAKUWA VIONGOZI WA MSATEKU
i. rais ( amir ) au mwenyeketi
ii. makamu wa rais ( naibu amir )
iii.
katibu
mkuu
iv.
naibu katibu mkuu
v. katibu mtendaji
vi.
amirati
vii.
naibu amirati
viii. wakuu wa kamati au idara
ix.
mlezi
10.1.2
KAZI YA MAMLAKA YA VIONGOZI RAIS WA MSATEKU ( MWENYEKITI )
i.
atakuwa
msemaji mkuu wa msateku
ii.
atakuwa kiongozi na msimaizi mkuu wa shughuri
zote za msateku
iii.
at aongoza au atasiamia mikutano yote ya
kamati na mkutano mkuu
iv.
atapendekeza ajenda za mikutano
10.1.
3 MAKAMU WA RAIS (MAKAMU MWENYEKITI )
i. atatekeleza majukumu kama atakavyotakiwa
kufanya na rais
ii. atatekeleza majukumu ya rais (
mwenyekiti) pindi rais asipokuwepo
10.1.4 KATIBU MKUU
i.
atakuwa mtendaji mkuu wa msateku
ii.
atatoa taarifa ya vikao vyote vya kamati
tendaji ya mkutano mkuu
iii. atakuwa katibu wamikutano yote ya kamati
tendaji
iv. ataunda kamati tendaji maalumu nakufafanua kazi na muda wake
wa utekelezaji
v. atatoataarifa za shughughri za MSATEKU kwa kamati tendaji mara mbili kwa mwaka
vi. atapokea
taarifa za utendaji za mikoa
nakuandaa taarifa ya utendaji ya MSATAEKU taifa
10.1.5 NAIBU KATIBU MKUU
i.
atatekeleza mjukumu kama atakavyo takiwa
kufanya na katibu
ii.
atatekeleza majumu ya katibu pindi asipokuwepo
10.1.6.
KATIBU MTENDANDAJI
i.
atatekeleza shughuli za kila sikuza
msateku
ii.
atashugulikia mawasiliano nataarifa z
amsateku katika matawi
iii.
atasiadiana na katibu mkuu katika
kutekelezamajukumu yake
iv.
atekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na mwenyekiti
10.1.7
AMIRA WA MSATEKU
i.
atakuwa msemaji mkuu wa kitengo cha wanawake
ii.
atakuwa msimamizi wa maswala ya husuyo wanawake au wanachuo wa kike
iii.
atasimamia na kuongoza vikao vyote vya vitengo cha wanachuo wanawake
iv.
atahakikisha malengo
ya kitengo cha wana chuo wanawake yanafikiwa
10.1.8.
NAIBU
AMIRA WA TAIFA
i.
atasaidiana na amirah katika kutekeleza
mjukumu yote yake
ii.
atakaimu nafasi ya amira asipokuwepo
10.1.9.
WENYE VITI WA VITENGO AU IDARA ZA MSATEKU
i.
kuendesha vikao vyote vya vitengo
au idara zao
ii.
watawajibika na majukuimu yote kwmujibu
wa idara zao ‘
10.2.
MAKATIBU WAKAMATI AU VITENGO IDARA KUU ZA MSATEKU
a. katibu
wa elimu na amali
i.
atakuwa afisa taaluma wa msateku katka
ngazi husika
ii.
atawajibika kwa mipamgo
yote ya fedha na uchumi
wa jumia
b.
KATIBU WAHABARI
NA MAHUSIANO NA USTAWI
WA JAMII WA MSATAEKU
i.
atakuwa afisa uhusiano na ustawi wa jamii
ii.
atawajibika na maswala yote ya habari
mahusiano na ustawi wa jamii ya MSATEKU
c.
KATBU WA FEDHA
i.
atkuawa ndio msimamizi wa muweka hazina ( mhasibu ) wa
jumia
ii.
atawajibika kwa mipango yote ya fedha na
uchumi ya jumuiya.
d.
KATIBU WA
IDARA YA WANAWAKE
i.
ndiye Mtendaji mkuu wa kitenfo cha
wanawake wa kushirikiana na amirah na naibu Amirah
ii.
atawajibika kuratibu utekelezaji wa
majukumu ya kitengo cha wanawake cha
MSTATEKU katika ngazi zote
SEHEMU
YA NANE
11. KANUNI ZA NIDHAMU
i. wanachama na viongozi wote wa MSATEKU
wanatarajiwa kuwa waislam wema na wenye kuzingatia kwa makini maadili ya
kiislam na maagizo ya kidini
ii. uvunjaji wowote wa dhahiri wa ibara
ndogo hapo juu utachukuliwa hatua kali za kinidhamu na mamlaka husika
iii hatua
za kinidhamu zitakazochukuliwa ni kuanzia onyo kali kusimamishwa kwa muda au
kufukuzwa kabisa
iv. hatua zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote
anayevunja katiba hii au ambaye matendo yake mabaya yameathiri MSATEKU
v. mtu ambaye hatua za kinidhamu zinatakiwa
kuchukuliwa dhidi yake atapewa muda muafaka wa kujitetea
vi. kutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa
vyombo vya juu lakini kamati tendaji itakuwa ni chombo cha mwisho ca rufaa ba
maamuzi yake hayatatakiwa rufaa zaidi ya hapo
SEHEMU
YA TISA.
12. MAREKEBISHO YA KATIBA/ RASIMU.
12.1. Katiba
hii na seheme yake nyingine yoyote haitabadilishwa au kurekebishwa
isipokuwa kwa idhini ya zaidi ya nusu ya
wanajumuiya wote wa mkutano mkuu wa MSATEKU
12.1.1.
Pendekezo au mapendekezo au mapendekezo ya kurekebisha katiba hii
yatawasilishwa
itakayowasilishwa kwa bodi ya
wadhamini kwa majadiliano na mapendekezo kamati tendaji
itasambaza mapendekezo miongoni mwa
wanajumuia ili kuyatathmini miezi matatu kabla ya
mkutano mkuu
12.1.2. Kamati tendaji itawakilisha kwa mkutano mkuu
marekebisho yaliyopendekezwa pamoja
na sababu za msingi na pia
mapendekezo [ushauri] ya bodi ya wadhamini
12.1.3. Marekebisho yatawasilishwa kwa bodi ya
wadhamini baada ya kukubaliwa katika kikao
rasmi cha mkutano mkuu
SEHEMU
YA KUMI.
13.
MENGINEYO
i.
Kura zote zinazohusu uchaguzi zitapigwa
kwa siri
ii.
Wanajumuiya hai ndiye atakayehudhura
vikao vinavyohusiana kuwa na haki ya kupiga kura
iii. Watumishi wa jumuiya hawatakuwa na haki ya kupiga kura katika vikao vyote vya
jumuiya
iv.
Kutakuwa na kanuni za jumuiya ambazo
zitaenda sambamba na katiba ya jumuiya pale ambapo patakuwa na utatanishi
katiba itatawala /itaamua
v. Muda wa kukaimu utakuwa si zaidi ya
miezi kumi na mbili
vi.
Rasimu hii ya katibu na itaanza kutumika
baada ya kupitiwa na wana jumuiya katika mkutano mkuu wa msateku
Imeandaliwa
na
Buda
M.P