E!
UVAAJI HIJABU UNAFAIDA AU NI MADAI YA KIISLAMU?
As.alaykum!!!!!!!!!!!!!!!!! wanajumuiya ya MSATEKU pamoja na Waislamu wote ulimwenguni.
|
Ashukuriwe mola mmiliki wa mbingu na Ardhi,mlezi wa viumbe vyote na
rehema na amani iwe juu ya kipenzi chake Muhammad{s.a.w.}na maswahaba wake wema
waliofata mwenendo wake mwema hadi siku ya mwisho.
Baada ya utangulizi mfupi,uislamu umetoa
mafunzo mema katika kila nyanja na harakati zote za mwanadamu ili aishi maisha mema yasiyokuwa na dosari.
Uislamu uliokwishatoa
mafunzo mengi kunako Mwanamke au Wanawake na jamii na jinsi ya kujihifadhi na
kujihifadhi kunamaana gani? Je! Mwanamke jinsi atakavyo taka kujihifadhi ndivyo anavyotakiwa jihifadhi? Au
ni kutokana na mafunzo ya kiislamu au
mafunzo ya dini alokuwa nayo?!!...
Mitume waliyopita ulinganiaji wao haukua na tofati bali kila
mmoja alikuwa muendelezaji sera za waliomtangulia kabla,utakapo kuwa ni mfuatiliaji
sera za mitume walopita utakuta kuwa swala la hijabu si la uislamu bali ni
uendelezaji yale yalobakishwa na dini zilizopita…
Hijabu ni sitara na hifadhi njema inayomuweka
mwanamke kuwa bora katika jamii, tofauti na zama kabla ya Mtume Muhammad{s.a.w}
ambapo mwanamke alikuwa kama takataka bila kuwa na hadhi yoyote.
Hijabu ilikuwepo kabla ya kutumwa
Muhammad{s.a.w}ilikuwa kwa maana ya kujihifadhi na kusafika moyo na kuzuwia
macho kunako vitu ambavyo vya weza sababisha kumpelekea mtu hisia zake kufanya
dhambi,sababu hiyo uislamu ulikuja kuboresha swala hili kwa maana;hijabu ni
kuhifadhi mwanamke viungo vya mwili wake wote ila uso mikono{viganja vya mikono} hivyo ndivyo
vyaruhusiwa kuwa wazi,miguu ni bora nayo kufunikwa,falsafa na lengo la uislamu
kulazimisha au kuwalazimisha waliyotangulia kujihifadhi hasa wanawake kila
kiungo chake ambacho chaweza sababisha kuamsha hisia upande wa pili{mwanaume}…
Kwa mantiki hii swala la hijabu si la uislamu
pekee bali Dini zilizopita pia lilikuepo.
FAIDA ZA HIJABU
Mwili wa mwandamu
unahitaji vitu tofauti ili uwe salama kutokana na maradhi ya hapa na
pale,mwenye kutaka kuwa salama na maradhi yampasa kutumia vitu au vyakula
ambavyo vya weka mwili kuwa salama kama matunda mbogamboga na
vyenginevyo,mazowezi nayo ni miogooni mwavitu vitanavyo weka mwili kuwa salama.
Maisha na Uhai wa
mwanadamu ya memiili na kutegemea maji{oksijeni na haidorojeni} bila vitu hivyo
Uhai wa mwanadamu ungelikuwa hatarini.Bila shaka umbile la mwanadamu ni nzuri
na bora kwani Mwenyezi Mungu alipo muumba mwanadamu alimuweka kuwa bora na kila kiungo kuweka mahala pake bila kukosea sehemu isio stahili kiungo hicho.
Mwenyezi Mungu asema:{ لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ}
{Bila shaka
hakika tulimuumba mwanadamu kwa umbo
lilo bora kabisa kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini.}
Maneno yake mola yapo
wazi kabisa,umbile la mwandamu jinsi lilivyo kuwa nzuri halina kifani wala
methali ila tu usipo kuwa makini umbile hili waweza likosa au umbile hilo kuwa chini na kulikosa
milele.
Umbile la mwanamke ni
umbile lisilokuwa na dosari kwa sababu hiyo uislamu ukatoa mafunzo mazuri kuhusu kiumbe ambacho ni pambo na pambo hilo
lina njia tofauti ya kuhifadhiwa.
Uislamu ulipo muamrisha
mwanamke kuvaa hijabu ulikuwa na malengo,miongini mwayo ni kwamba mwili wa
mwanamke kama ilivyo kuwa wazi ni tofauti na mwanaume,mwili wake wapokea
magonjwa haraka hasa katika viungo vile ambavyo uilslamu umeamrisha
kuvihifadhi,matundu ya mwili wa mwanamke ni makubwa zaidi kuliko ya mwanaume na
matundu hayo kipindi mwanamke hajahifadhi mwili wake kama ipasavyo upumuaji wa mwili unakuwa ni zaidi na
oksijeni yaingia katika mwili bila mpangio wowote ule, na matundu hayo ya
funguka zaidi na mionzi ya Jua yaingia moja kwa moja bila kiziwizi sababu hiyo
ya weza sababisha maradhi tofauti kama upungukaji damu na maji na ngozi kuwa
kavu na kuhisi mchovu kila mara na mengineyo.
Faida ya hijabu ni kuhifadhi
mwili kutokana maradhi tofauti,
mwanadamu kuwa salama ndiyo uhai wake kama ilivyo wazi na maradhi ya mara kwa
mara umri husababisha umri na maisha yake kuwepo hatarini pia hijabu ya hifadhi
hadhi ya mwanamke tafauti na hapo kabla mwanamke alikuwa ni nija ya biashara
tu.
Khasara aipatayo mwanamke kwa sababu ya kutozingatia swala
hili la hijabu ni kwamba kama jinsi tulivyo nakili kutoka kwa Dr.Nadia Husaini
katika kitabu cheke cha{UMLIMWENGU WA WANAWAKE}anasema:{…HIJABU INATHARI NA MCHANGO MKUBWA KATIKA SIHA NA
AFYA YA MWANAMKE HIJABU KUWA NI HIMAYA YA MWILI KUZUIYA MARADHI, KUHIFADHI
NYWELE, KWANI NYWELE KIAFYA HAZITAKIWI KUPIGWA NA MIONZI YA JUA MOJA KWA MOJA
KWA SABABU OKSIJENI HAINA MCHANGO KATIKA
UKUWAJI WA NYWELE BALI HUSABABISHA NYWELE
KUWA NGUMU NA KUKATIKA NA HILI HII NI TATIZO LIMEZAGAA KATIKA JAMII,
NA KUTOKUJUA JINSI YA KUTATUA TATIZO
HILI, HALI YA KUWA UTATUWAJI TATIZO HILI NI SWALA DOGO TU, NALO NI KUVAA HIJABU…}
Faida ya hijabu ya rejea kwake mvaaji, lengo
kulinda na kuhifadhi Uhai hadhi yake, khasara ya kutovaa hijabu kimali ni kwamba
anakuwa mwenye matuzi mengi ya pesa lengo la kutibu maradhi au magonjwa
yaliyomsibu kwa kutozingatia hijabu, khasara ya kinasfi ni pindi anapo fikwa na
mauti bila kufikia malengo.
Je!! Mtu yuko tayari kufanya kitu kinacho
mdhuru au kujipa sumu kwa kuwa tiba anayo?!!
No comments:
Post a Comment