Head Secretary-MSATEKU |
Bismillahir Rahmanir Rahiim:
I'M PROUD
TO BE A MUSLIM:
1:) Islam is the
religion of peace
2:) Islam is the religion of peace and justice
3:) Islam
is the religion of peace and tolerance
4:) Islam is the
religion of peace and prosperity.
YOUR
BROTHER: Amry
Jaribu, Don’t forget me in your nice prayers THANKS.
Jumapili, tarehe
27 Januari, 2013. Assalam alaykum……
Hatuna budi kumshukuru Allah kwa kutupa nguvu na uzima
wa kukutana wote hapa katika msikiti wa jumuiya ya MSATEKU kwa lengo la kuambiana
mambo mawili, matatu kuhusiana na MBINU ZA UFAULU KWA MTAHINIWA,MAMBO YA
KUFANYWA NA YASIYOTAKIWA KUFANYWA NA MTAHINIWA
NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI.Namuomba Allah awapeni usikivu na mie kunipa
nguvu ya kuwasilisha mada zangu kwenu,wanafunzi wa KIDATO CHA SITA na
wengineo………..awali ya wote na nitaanza mada yangu kwa chachu hizi….
Mtihani ni kipimo cha imani (kidini), uelewa
au ufahamu wa mtu juu ya kitu fulani kwa mfano Mwenyezimungu (s.w) ametuandalia
mitihani mbali mbali kama maradhi au vifo ili kutupima imani zetu kama
tutafaulu au tutafeli. Pia katika mashule yetu imeandaliwa mitihani ili
kutupima ufahamu uelewa wetu juu ya yale ambayo tunayasomea.
Katika namna ya kujiandaa
na mitihani kupo kwa namna kuu mbili nazo ni;
(i) Maandalizi ya kivitendo,
hapa mtu hujiandaa pale tu anapoingia katika shule kutokana na kufahamu kuwa
ipo siku atafanya mitihani na kumaliza shule. Mitihani hiyo ndiyo ambayo
itakufanya uweze kufaulu na kwenda katika ngazi ya juu zaidi au kutokwenda.
Hivyo basi hatuna budi kujiandaa kwa namna yoyote ile iwayo ili tuweze kufaulu
na kuweza kuendelea katika ngazi za juu zaidi na hatimaye kuweza kutimiza yale
malengo yetu.
(ii) Maandalizi ya
kiimani, Katika maandalizi haya mtu huanza katika ngazi ya kifamilia,
kuanzia pale unapozaliwa hadi kufikia kiwango cha kuweza kujitegemea kwa maisha
yako na hatimaye kuwa baba au kuwa mama.
Hivyo hatuna budi basi
kuamini kuwa mitihani nikipimo cha kuamini Qadar (kheri au shari ) zinatokana
na Mwenyezimungu (s.w). Hivyo basi hatuna budi kuelewa kuwa tunadhimma ya
kutekeleza yale yote ambayo ndiyo sababu ya sisi kufaulu au kufeli katika
mitihani hiyo (KIIMANI) Hivyo katika maandalizi haya hatuna budi kuiendea mitihani
yetu katika namna ambayo Mwenyezimungu (sw) ataipendelea ambayo ni;
i. kusimama visimamo vya
usiku,
ii. Kuingia katika chumba
cha mtihani haliyakuwa tumetia udhu,
iii. Kuwahi katika
eneo la tukio (chumba cha mtihani) ili kuyazoea mazingira ya eneo husika,
iv. Kumtanguliza
Mwenyezimungu kwa kusoma suratul fat-ha(quran)
na suratul muadhwatain
(falaq& nnasi) mwisho ni saratul ikhlas ni vizuri idadi ya witri
ikiwezekana.
v. Kumsabahi Mwenyezimungu
kwa nyiradi mbalimbali (fupifupi).
NAMNA YA
KUFELI MITIHANI KWA MAKUSUDI
1. Usiwe na ratiba ya mitihani pamoja na ya
kujisomea.
2.
Anza na swali usilolijua ambalo litakuchanganya.
3.
Kutotumia uwezo wako wote katika kulijibu swali ambalo unalijua.
4.
Kufanya swali ambalo huna uelewa nalo kabisa ni akheri usilifanye na uliache
kwani utapolifanya utaonyesha udhaifu wako kwa wasahihishaji au ukitaka basi lifanye
mwisho baada ya maswali yote unayoyafahamu kuyafanya.
5.
We hisi kuwa ni vizuri kwa kutokuwa makini na muda, kwani waona kufanya mtihani
kwa muda si sehemu ya mtihani.
6. Usiende maktaba kusoma wala kujikumbusha
ulivyo soma darasani kwa muda wako wa ziada.
7. Usisome vitabu, wewe soma tu 'summary' za notes na kamusi ili ujue tu maneno magumu ya kuwatishia wengine kuwa wewe ni msomi na lugha ina panda kwa sana.
8. Kesha sana kila siku lala saa tisa usiku au kumi kabisa alfajiri wakati shule unatakiwa kuamka saa moja asubuhi kila siku.
9. Nenda club mara nyingi iwezekanavyo kama vipi kila siku ukiweza.
7. Usisome vitabu, wewe soma tu 'summary' za notes na kamusi ili ujue tu maneno magumu ya kuwatishia wengine kuwa wewe ni msomi na lugha ina panda kwa sana.
8. Kesha sana kila siku lala saa tisa usiku au kumi kabisa alfajiri wakati shule unatakiwa kuamka saa moja asubuhi kila siku.
9. Nenda club mara nyingi iwezekanavyo kama vipi kila siku ukiweza.
10. Kuwa mlevi na mwingi wa wanaume/wanawake wakati uko masomoni.
11. Ukipewa mtihani anza kufanya bila kusoma maelekezo kwanza.
12. Usisome wakati unategemea kufaulu mtihani kwa miujiza.
13. Usisikilize walimu wako au walezi/wazazi hususani kipindi mwisho, karibu na mitihani kama hiki.
14. Uwe mwenye kusoma kitu kipya (mada mpya) karibu na mitihani.
15. Uwe mpenda sifa, mjuaji wa kila kitu, majivuno ya kwenu mna pesa kufaulu sio ishu.
16. Mwalimu anapo fundisha usichukue notes kaa tu muangalie kama kideo na ongezea kusinzia ikibidi.Eti anatupotezea muda mitihani imekaribia.
17.Usijali alama unazopata katika mazoezi au mithani ya Majaribio mbalimbali, eti ukisema ‘after all is just a number!!
18.Waambie wenzio 'wametumwa na kijiji kuja kusoma ndio maana wanasoma sana' na wewe kusoma kwako sio ishu sana, after all ukifeli unaweza kuwa konda wa magari ya''baba/ mama, mjomba, shangazi, baba mdogo n.k''
19.Ukiwa katika mtihani wa usifanye yaangalie tu na hisabati soma kama notes usi kokotoe hata moja 'after all ni ugonjwa wa taifa'
20.Wakatishe wenzio tamaa ''kufauru masomo sio kufauru maisha'; ' wasomi mbona wengi halafu wote choka mbaya tu (kusoma sio dili) au mkubwa afeli bhana……..
21. Wewe toa mawaidha badala kujibu swali (Islamic knowledge).
22. Wewe jifanye walijua sana somo husika,
hivyo utalifaulu tu (Islamic Knowledge).
MAMBO KUMI(10) YA KUZINGATIA YA WAKATI WA MAANDALIZI YA MITIHANI:
KWANZA: kuzingatia muda, si vema kukurupuka na
kukimbizana nao na kujinyima usingizi wakati ratiba ya mtihani ilikuwa
inafahamika na ulikuwa na uwezo wa kujiandaa taratibu kuelekea kwenye siku
ya kutahiniwa kwako.
PILI: Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka.
Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye mitihani. Hakikisha unapata mitihani ya nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha hakuna swali hata moja ambalo linakushinda.
Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake na hivyo kujiandaa.
Ubahatishaji huu, lazima uambatane na kile nilichosema awali, yaani kuwa na kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia rudia.
ya kutahiniwa kwako.
PILI: Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka.
Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye mitihani. Hakikisha unapata mitihani ya nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha hakuna swali hata moja ambalo linakushinda.
Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake na hivyo kujiandaa.
Ubahatishaji huu, lazima uambatane na kile nilichosema awali, yaani kuwa na kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia rudia.
TATU: Orodhesha maeneo yote ambayo huyaelewi kwenye mtihani hiyo ya nyuma na
uyafanyie mazoezi kwa kupata ushauri kwa waalimu wako. Kama kuna mada
ambazo hujazielewa kwenye daftari lako hakikisha muda uliojiwekea utatosha
kuzielewa.
NNE: Haifai mwanafunzi kukimbia ma
elekezo
ya mwisho yanayotolewa darasani na mwalimu wako, kwani hayo ndiyo yatamuwezesha kufahamu kama umekamilika kwa kutahiniwa au bado kuna eneo linakutatiza.
TANO: Hakikisha kuwa kumbukumbu zako kichwani zinaongezeka kadiri unavyosoma, usiwe mtu wa kusahau sahau ulichosoma na ikiwezekana eneo ambalo unaonekana kulisahau ndilo ulipe
kipaumbele cha kujikumbusha, ikibidi hata kila siku.
SITA: Angalia kwa makini alama zako za mitihani ya majaribio, ikiwa umepata alama za chini ujue kuna mahali panahitaji nguvu za
ziada, shauriana na mwalimu wako
maeneo yote unayokosa au yanayokusumbua kabla ya siku ya mtihani.
SABA: Iliuwe na uhakika wa
kufanya vema mtihani wake anatakiwa kuzingatia dondoo zote zilizotolewa kwenye
kipengele
cha kuimarisha kumbukumbu kichwani, ambazo zimo ndani ya kitabu hiki.
NANE: Wakati mwingine ni vema ukausikiliza mwili, si vema kuulazimisha
kusoma hata kama unaona kuna udhaifu, baadhi ya wanafunzi hukesha wiki mbili
mfululizo wakisoma, matokeo yake mwili na akili huchoka na kushindwa kupokea
masomo vizuri. Muda wa kupumzika unahitajika.
TISA: Kabla ya mitihani unatakiwa
kujiamini kwa kushinda hofu. Eneo hili
ni muhimu sana kwani kuna wanafunzi hufeli si kwa
sababu hawakujiandaa, bali
hukumbwa na hofu muda mfupi kabla ya kuanza mitihani.
Hivyo ni muhimu mwanafunzi akaandaliwa kisaikolojia na waalimu pamoja na wazazi
wake jinsi atakavyoweza kufanya mtihani bila hofu.
KUMI: Imani ni hitimisho la mafanikio ya mwanafunzi,
haifai kuingia katika kipindi cha mtihani
ukiwa na mawazo hasi. Kinachotakiwa ni ari ya ushindi au kwa lugha nyingine ni
mawazo chanya. “LAZIMA NIFAULU MTIHANI HUU” Imani hii inaweza kujengwa na mtu
kupitia kujiamini mwenyewe au kuamini kwa msaada wa nguvu za imani yake ya
dini.
MBINU ZA KUFAULU KABLA NA BAADA YA
KUINGIA CHUMBANI CHA MTIHANI:
Kwanza unapaswa kuzingatia akilini kuwa unakabiliwa na mtihani, hivyo jikumbushe mambo yote uliyoelekezwa na mwalimu wako kuhusu mtihani, pili hakikisha kuwa unafahamu vema ratiba. Ukishaweka uzingativu, anza kupambana na hofu ambayo wengi huwa nayo siku ya mtihani. Jiambie kuwa unajiamini na utafanya vizuri mtihani wako. Epuka kuwaza kuwa mtihani utakuwa mgumu kwako.
Uone mtihani kama kitu cha kawaida na kitu ambacho kinakufanya upeo wako ukue na uelewa wako kuongezeka. Puuza hofu na vitisho vyote ulivyowahi kuambiwa juu ya mtihani.Ukiliweza hili taratibu utaanza kuona kujiamini kwako kunaongezeka.
Pia fahamu kuwa wewe si mtu wa kwanza kufanya mtihani kwani watu wengi walisha wahi kufanya mitihani na wakafaulu. Jiweke katika kundi la watakaofaulu vizuri na jiamini kuwa una uwezo huo. Siku ya mtihani amka mapema na anza kuandaa vifaa vyako vya kufanyia mtihani. Hakikisha una kalamu zaidi ya moja, rula, penseli, Mathematical set (mkebe) wenye vifaa vyote hasa katika masomo yanayohusisha hesabu na kuchora.
Pata kifungua
kinywa chepesi, kama ni chai au chochote ulichozoea kula asubuhi. Epuka kula sana
asubuhi kwani utaanza kusinzia kwenye chumba cha mtihani.
Kama unaishi mbali na shule,wahi kuondoka ili kuzuia vitu ambavyo vitakufanya uchelewe kwenye chumba cha mtihani kama foleni ya magari au umbali mrefu.
Kama unaishi mbali na shule,wahi kuondoka ili kuzuia vitu ambavyo vitakufanya uchelewe kwenye chumba cha mtihani kama foleni ya magari au umbali mrefu.
Hakikisha
vifaa vyako vyote vimekamilika kabla ya kutoka nyumbani,mfano
peni,penceli,mkebe,kitambulisho…..na vinginevyo vinavyohitajika kuingia navyo
katika chumba cha mtihani.
Pia hakikisha una saa ili uweze kuutumia vizuri muda uwapo ndani ya chumba cha mtihani.
Wakati unaendelea kujiandaa, unaweza kuendelea kujikumbushia vitu vidogo vidogo katika notisi zako unavyohisi vinaweza kuwemo kwenye mtihani ingawa siyo lazima kama umejiandaa vizuri.
Epuka mazungumzo yoyote yanayohusu mtihani. Kaa mbali na watu ambao wanazungumzia mabaya kuhusu mtihani kwa mfano “ mtihani huu ni mgumu” au “wengi walifeli mwaka jana” kwani kauli kama hizi zitakufanya ushindwe kujiamini.
Kaa kimya muda wote na epuka sehemu zenye kelele. Endelea kujiamini kuhusu ufaulu na jinsi utakavyofurahiwa na wazazi wako baada ya majibu kutoka. Tafuta ushujaa kwa watu waliokusomesha, ingia kwenye mitihani kwa lengo moja tu la kuibuka mshindi na si mshindwa.
Jiamini kuwa ulichokisoma kwa siku zote ulizokuwa shule kinatosha kukufanya ufaulu. Epuka kusoma vitu vipya muda mchache kabla ya kuingiaItulize kabisa akili yako.
Zingatia sana usafi wa mavazi na mwili kwani ukiwa mchafu utakosa utulivu uwapo ndani ya chumba cha mtihani.
NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI :
Hakikisha umeingia ndani ya chumba cha mtihani nusu saa kabla ya muda wa kuanza mtihani.Kama hamtaruhusiwa kuingia kabla, hakikisha upo jirani na chumba cha mtihani na unaelewa kila kitu kinachoendelea.
Endelea kutuliza akili yako na amini utafaulu kwa moyo mmoja. Tulia kimya ukitafakari namna utakavyoyajibu maswali kwa ufanisi.
Baada ya kuingia chumba cha mtihani na kupewa karatasi ya kujibia na karatasi ya maswali, endelea kutulia ukisubiri kusikia maelekezo kutoka kwa wasimamizi. Usikimbilie kufunua karatasi ya maswali na kuanza kujibu au kusoma kabla haujaruhusiwa kwani hilo ni kosa.
Hakikisha akili yako imetulia na wala usiwe na papara. Jiamini kuwa unaweza. Bila shaka utapewa muda wa kuanza kupitia maswali kabla ya kuanza kufanya mtihani. Utumie muda huo kusoma maelekezo ambayo yako juu ya karatasi (Instructions).
Soma kwa makini maelekezo yote na hakikisha umeyaelewa vizuri na ikiwezekana rudia kusoma kwa mara ya pili. Baada ya Kuhakikisha umeelewa vizuri maelekezo yote, anza kuyasoma maswali kabla ya kuanza kuyajibu. Elewa ni maswali yapi ni lazima kuyajibu (compulsory), fahamu mtihani una maswali mangapi jumla na fahamu kila swali lina maksi ngapi.
Hakikisha umeyasoma maswali yote, la kwanza mpaka la mwisho na weka alama kwenye maswali unayoyafahamu vizuri. Ukishayasoma yote, panga muda utakaoutumia kujibu kwa kila swali kutegemeana na uzito wa swali. Ukishamaliza sasa unaruhusiwa kuanza kuyajibu. Anza na yale unayoyajua vizuri kwani kwa kufanya hivyo utajikuta kujiamini kwako kukizidi kuongezeka.
Epuka kuanza kujibu maswali unayoyaona ni magumu kwako. Anza na yale mepesi kisha ndiyo uendelee na yale magumu.Utajikuta ukiufurahia sana mtihani wako na hofu itaisha kabisa. Hakikisha unafikiria kwa makini kabla ya kujibu swali lolote hata lile unaloliona ni jepesi.
Zingatia kuandika majibu yako kwa mwandiko unaosomeka vizuri ili msahishaji avutiwe na kazi yako. Hakikisha pia umeandika namba ya kila swali ulilolijibu. Hakikisha unajibu maswali kulingana na jinsi ulivyoulizwa. Ukiambiwa jibu kwa herufi (Multiple choice) basi fuata maelekezo. Kama umeambiwa jibu Kweli au si kweli ( True and False) fuata maelekezo kwa makini, usiweke manjonjo sana unaweza kupoteza maksi.
Namna ya Kuyapokea Matokeo:
Matokea ni zao
au chumo ambalo hutokea baada ya kufanyika kwa jambo fulani ,hivyo machumo
yaweza kuwa ni kuridhisha au kutoridhisha. Hivyo matokeo ya mitihani yetu
yaweza kuwa ni mazuri , ya kati na kati au yasiokuwa mazuri.
i. MATOKEO
MAZURI:
Hayo ni matokeo ambayo mtu
huyapata yakamuwezesha yeye/wewe kwenda katika ngazi ya juu ambayo anaitarajia/
unatarajia.
Watu
wengi wapatapo matokeo mazuri hupata kiwewe kutokana na furaha waliyonayo na
kukurupuka na kushindwa kufanya uamuzi uliosahihi.La umuhimu nikumuomba
Mwenyezimungu na kumshukuru na kutafuta ushauri kwa wale walio juu yako ni lipi
la kufanya kabla ya kufanya uwamuzi.
ii. Kati Kati:
Haya ni matokeo
ambayo mtu hupata alama/matokeo mazuri lakini kutokana na alama hizo
hazikumuwezesha yeye kupata kuisoma kozi ambayo ameitarajia. Mfano mtu ambaye
amepata gredi ya tatu (Division iii) na ametaka asome udaktari (medicine) .Ni
ngumu kupata kozi hiyo lakini kuna baadhi ya vyuo ambavyo anaweza kupata chuo
kutokana na alama hizo. Hivyo basi ni uzuri kutafuta ushauri kupitia
wanafunzi/waislam walio vyuoni ili kuweza kumshauri cha kufanya.
iii. MABAYA
(YASIYORIDHISHA)
Haya ni
matokeo ambayo hayatamuezesha mtu kujiunga, kuingia elimu ya juu (vyuo) katika
kiwango cha shaada(degree) maranyingi watu hawa huwa ni wenye kukata tamaa na
wengine kuamua kurudia mtihani ili waweze kufaulu hali yakuwa kuna njia
nyingine (mbadala) ambazo wanaweza kupitia na kufikia malengo yao mfano
ASTASHAHADA (CERTIFICATE), STASHAHADA (DIPLOMA), na hatimae kufikia SHAHADA
(DEGREE) na kisha kuendelea ngazi au kiwango cha juu zaidi kielimu.
USHAURI.
Nisingependa kumshauri mtu arudie mtihani kwa
maana utafiti umeonyesha kuwa wengi wanaorudia mtihani hawafanyi vizuri.
Lakini kwa wenye kuamua mitihani yawapasa
wafanye yafuatayo kwanza:
1. Kufanya
tathmini ya kina sababu zilizopelekea matokeo yake kuwa hivyo
2. Je sababu
hizo zinatatulika kirahisi
3. Basi atatue
matatizo hayo ndio aweze kurudia mtihani
Miongoni mwa sababu zinaweza kuwa;
a) Sababu za ndani/binafsi (internal factor)
b) Sababu za nje (external factors)
Sababu zote hizi mwisho wa siku
huchangia katika kuleta matokeo ama mazuri au mabaya, zinaweza kuwa za
kiuchumi, kifamilia, kimazingira, kijamii au kitaasisi (shule).
Baada ya
kutatua hizo sababu tunaweza kukubaliana na wewe katika mawazo yako ya kurudia
mtihani wako.
********* Wabillah Taufiq **********
Brother Mussa Khaini akiwa anatoa mada kuhusiana na mambo ya kujiandaa kisakolojia kwa Mtahiniwa kabla ya Mithani ya kidato cha Sita.
Brother Nassoro nae alikuwa ni kati ya watoa mada kwa wanasemina,hapa akiwa anasisitiza jambo kutokana na mada yake ya "maisha baada ya mitihani"
Pichani vijana wa kidato cha sita kutoka shule mbalimbali zamjini mbeya wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa,huku wakiwa wanachukua nukuu kwa yanayozungumzwa,tayari kwa utekelezaji wa kivitendo.
"Dahhhh.......WALI MAUA tayari, sasa itakuwaje hapa......ebu ona kitu cha njano katika sufuria...... " ndivyo anvyoonekana akisema ustadh Yusufu(mwenye kanzu)huku bibi harusi mtarajiwa(Zainabu Kalulu) akifurahi.......dada shamila na Ajuna wakifuatilia kinachoagizwa na kiongozi mwenzao.
Japo tupo jikoni je tutakula leo jamani.....????? ndiyo tafsiri zinazoenekana kwa picha mbili hapo juu...kwa maustadh wakiwa katika pozi tofauti ili muradi mambo yaende sawa kwa shughuli za jikoni na maandalizi mengine ya nje ya chumba cha semina.
Hatimaye paliliwa......!!!! wanasemina na watoa mada wakiwa katika makundi tofauti...walipata chakula cha mchna kwa pamoja.......WALI MAUA wenye Radha ya Pwani uliliwa......Mashaallah......!!!!!
Raha ya mchele sharti uvulie viatu.......na pia maji ya MBEYA SPRING WATER nayo yafuatieeeee......!!!!ni baadhi ya majukumu yaliyofanywa na Maustadh pichani......hakika ilikuwa rahaaaaaaaaa.
"......Rahaaaaa.......ya mchele Brother Jaribu ni sharti na ni lazima ukalie katika majaniiiii.....pia ni lazima sharti kanzu uipandisheeeee....."
ndivyo anavyoelekea kuyasema Brother Amour na Ridhiwan mara baada ya kufanya kazi ngumu sana ya kuwaleta pamoja vijana wa kidato cha sita na kufanikiwa kwa Semina.
Wacha ninawe mie.......!!!!vijana wakiwa wanaosha mikono yao tayari kwa safari ya kurudi makwao.
kwani hii ni wali mauwa au biriani?!!!!
ReplyDelete