Sunday, November 2, 2014

KIKAO CHA JUMUIYA YETU YA MSATEKU KILIFANYIKA JUMAPILI 02/11/2013

Shekh Zubeir n/amiri taaluma na shekh Rajabu manager wa mgahawa wakitabasamu na kucheka kwa yale mazuri waliyokuwa wakiyasikia inapendeza sana kuwaona wanafurahi kuona mambo yanasonga mbele
Badhi ya wanajumuiya waliyo hudhuria katka kikao hicho mwaka wa kwanza walikuwepo pia, tunawakaribisha sana katika jumuiya yetu inshaallah
wanajumuiya wako makini kusikiliza yaliyojiri katika kikao
Amiri wa jumuiya al -akh Abdul Abubakari akielezea na kuweka wazi baadhi ya mambo ya jumuiya

Waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ya TEKU al-akh Nurdin Makono akiwa makini hakutaka kupoteza maelezo yoyote

Amiri wa jumuiya akieleza baadhi ya mambo khusiana na mgahawa na muelekeo wa jumiya
N/Amiri da'awa akielezea mambo yanayohusiana na idara yake kutoka katika ripoti yake
Baadhi ya wanamsateku waliohudhuria katika kikao hicho cha mwezi



Maukhti pia walihudhuria wakisikiliza kwa makini
N/Amiri taaluma akisoma ripoti ya idara yake pamoja nakutoa ufananuzi wa baadhi ya mambo
Katibu na Amiri wa jumuiya wakisikiliza kwa makini maswali yayoulizwa na wanajumiya ili wayajibu kwa ufasaha

Friday, October 31, 2014

UMUHIMU WA NDOA

Ungana na AMIR wa jumuiya ABDUL ABUBAKARI katika umuhimu wa ndoa hapa chini inshaallah



AWW,SIFA NJEMA NI ZA ALLAH NA REHMA NA AMANI ZI MSHUKIE KIPENZI CHETU MUHAMMAD  (S.A.W) NA AHLI ZAKE AMA BA’DA.NDUGU ZANGU WAISLAMU NATAKA KUKUMBUSHENI KATIKA NDOA.

Tendo la Ndoa ni Ibada - النّكاح عبادة
Uislamu umenyanyua hadhi ya suala la tendo la ndoa na kulifanya kuwa ni ibada, ibada ambayo wana ndoa wakiifanya hulipwa. Kwani kwa ndoa yao hii ya halali wamejiepusha na maasi na uchafu na wakaishi katika sakafu moja katika mazingira ya kufahamiana, kupendana, kushibana na mahusiano mazuri ya kubadilishana mapenzi yenye kulandana.
Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam)  juu yake amani na salamu anasema:
في بضع أحدكم صدقة
“…na katika kumuingilia mkeo ni sadaka.”(Muslim)
Tendo la ndoa ni sadaka anayotoa mume kwa mkewe, na katika ukamilifu wa neema ni mtu kuhisi kuwa haja zake zinashibishwa na ndipo hapo nafsi inapopata utulivu na malipo ya Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) .
Ibn al-Qayyim (RadhiyaLlahu 'anhu)  anasema: kila ladha husaidia ladha ya siku ya mwisho, ladha hiyo hupendwa na Inaridhiwa na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala)  na mtendaji hupata ladha katika sura mbili:
Upande wa mwanzo ni kule kustarehe na kujifurahisha na kupata utulivu wa macho.
Upande wa pili ni kule kumridhisha Allah (Subhaanahu wa Ta'ala)  na huko ni  kuifikisha nafsi katika daraja la ladha iliyo bora zaidi.
Ndu zangu katika iman na wahimiza vijana(mabarobaro), katika swala zima la ndoa kila mwenye uwezo wa kuoa aoe kwa sababu mtume mtukufu anatutaka kuoa,na Yule ambaye anauwezo wa kuoa na asioe, mtume (s.w.a) ndoa ni katika sunna yangu, mwenye kuacha sunna yangu sio katika sisi.
Eee dada yangu kubali kuolewa,acha kuweka vikwazo vingi visivyo na maana,kubali kusitirika usije ukadhalilika na ukadhalilisha dini yako, mtukufu wa daraja anasema mwanamke anasitirika kwa mambo mawili ima aolewe au azikwe vinginevyo ni mtihani, usidhani kukataa kuolewa umenusurika la hasha ila unatafuta ufisadi katika ardhi.
Kila mwenye mume ALLAH amsitiri na ambaye hana ALLAH awape mume bora na sio bora,na vilele kwa wanume ALLAH awape wanawake wenye sifa nzuri za kichamungu. Wabillahi tawfiq



Monday, October 27, 2014

WANAFUNZI WA KIISLAMU WA CHUO KIKUU CHA TEKU WAKISHEREKEA MAHAFALI YAO YA KUHITIMU

Dada yetu Amirat wa jumuiya pia alikuwepo ukhti Nzitu
 
                     Alikuwepo katibu wetu mstaafu brother Al-Amin akiwa na ukhti Sabrina
            hawa ni baadhi ya wanajumuiya wa msateku waliohitumu elimu yao ya chuo kikuu, ukht Ajuna, Hawa na Sabrina walikuwepo ktk mahafali hayo
Amiri wetu wa jumuiya ya Msateku brother Abdul Abubakari alikuwepo pamoja na mke wake ukhti Sabrina ambaye alikuwa anagraduate

Sunday, May 25, 2014

Mahafali ya wanachuo wa kiislam wa TEKU yakifanyika katika chuo cha Mbeya Institute of Technology(UST) wakijumuika na wenyeji wao MUST pamoja na wanachuo wa Hospitali ya Rufaaa Mbeya... Katika mahafali iyo iliyofanyika tarehe 25/05/2014 Lengo ilikuwa ni kuwaaga wanachuo wa Shahada na Stashahada.. Mgeni rasmi alikuwa ni naibu Amiri Taifa... akishirikiana na viongozi wengine wa mkoa... Tunamshukulu ALLAH mahafali tulimaliza salama....
Baadhi ya wanajumuiya wa vyuo hivyo wakiwa katika Hall la Mafaali ...

Amiri wa mkoa wa Mbeya akiwa mezaa kuu na viongozi wengine wa mbeya pamoja na mgeni rasmi... Aliesimama ni Amiri wA MKOA wa Mbeya....
Akhy mwarabu akiwaasa wahitimu wakatende wema huko wanapokwenda makazini as far as religious of Allah as concerned...
S
Shekh Ibrahim ambae ni mlezi wa wanachuo wa vyuo katika jiji la Mbeya... Akitoa mada kuhusu mshikamano...
Naibu Amiri wa Tanzania akitoa mada... akiwa kama Mguni Rasmi wa Mahafali iyo...
                          Waagwa kutoka Teku wakichukua vyeti vyao
Baadhi ya Matukio kwa wanachuo wa Teofilo Kisanji University baada ya kumaliza sherehe iyo ya Mahafali...


Monday, May 5, 2014

Siku ya mavazi ya kiislam  "Ijabu Day"... iliyofanyika msikiti mkuu wa Mbeya uliopo barabara ya NANE Mbeya mjini karibu na stand kuu.. Baadhi ya mashekhe waliohudhuria ni Shekh Abbas, Shekh Bombo na Shekh Pembe... Pamoja na maamiri wa Mkoa...
                            ....Maada mbalimbali ziliwasilishwa na mashe hao...
  Hao ni baadhi ya mashekh wakiwa katika iyo siku ya mavazi ya kiislam ikiwagusu dada zetu         na  mama zetu...
                      Shekh Abbas akiwasilisha mada nafasi ya elimu katika uislam...

                      Hao ni baadhi ya maukht waliohudhuria siku ya "Ijabu Day"
                                                   Shekh Pembe akiwasilisha mada..
                                  Baadhi ya waumini waliohudhuria katika "Ijabu Day"
                      Shekh Bombo akitoa mada basing on definition of jalabibi/hijjabu as far as
                       religious of Allah as concerned.
DJ Shekh Ally akifanya kazi yake.... more effectively and efficiently.
 
 Amiri wa chuo cha Teku akhy ABDUL akiakhirisha hafla iyo.

               

Sunday, April 27, 2014


                                                     Assalaaam alaikum.....
semina ya wanafunzi wa kiislam ambao wapo kidato cha SITA ambao wanatarajiwa kuanza mitihani yao ya mwisho tarehe 5/5/2014.. "semina iyo ilisimamiwa na mwalim mlez Shekh Ibraim na amiri wa mkoa.... ikiendeshwa na wanajumuiya wa MSATEKU wakiwa na Amir wao akhy Abdul"
Hao ni baadhi ya viongozi na wawasilisha  mada katika semina iyo... aliesimama ni mwalimu mlez shekh Ibrahim.

                          Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria katika semina iyo.

Huo ndo mchakato mzima wa chakula ulivyokua ukiendelea wakati wa semina..



                       Huo ndo mchakato mzima wa upataji wa chakula ulivyoendelea...

Sunday, April 13, 2014

                                                      Assalam alaikum..
kikao cha wanajumuiya wa MSATEKU kililichoendeshwa tarehe 1/04/2014 katika msikiti wao wa JIDDAH kikiudhuliwa na Amiri wa Mkoa.. "Dhumuni la kikao ni kutangaza uongozi mpya wa wanajumuiya hao".

Amir wa mkoa wa Mbeya Akitoa nasaha zake kabla ya uongozi mpya kutangazwa.. kwa ufupi alizungumzia jinsi gani jumuiya ya MSATEKU ilivyo katika mstari wa mbele kuendeleza UISLAM katika JIJI la MBEYA.. Akiwaaasa viongozi wajao kufanya ivyo ili kuipeleka mbele dini ya ALLAH.

Baadhi ya wanajumuiya wa MSATEKU waliohudhulia katika kikao cha kutangaza uongozi mpya...
Akhy Kafyome akiwa katika nyazifa ya kutangaza uongozi huo mpya wa MSATEKU...
    Maamiri wa vitengo mbalimbali wakirudisha mafaili ya vitengo vyao.. kabla ya uongozi mpya  kutangazwa..
Amir Abdul baada ya kuchaguliwa kwa mara ya pili katika nyazifa iyo ya Uamir kuongoza tena jumuiya ya MSATEKU... alitoa nasaha zake kwa ufupi...
Naibu katibu aliekabidhi manadara akitoa nasaha kwa niaba ya uongozi uliopita...