Tuesday, August 7, 2012


Thread: Nike / Puma abuses Allah image on shoes

Overall activity: 0%

Nike Puma shoes with Allah written in Arabic style as logo for shoes have created controversy around the World especially among Muslims. A shoe logo design has been used by Nike Company, which is looked like the name of Allah (GOD). Allah has been written in Arabic style on Nike Puma shoes. Many people have protested Nike for designs and tell them, not to use this design in future. People also said that they will stop using Nike products until or unless they remove the sticker from shoes.
Nike Puma has made one pair of shoes and shoes has contained name Allah at Arabic style and people recognized the name and they have protested Puma a lot. Many people have thrown puma shoes from the store shelves. USA Muslims people are protesting Puma to stop making shoes with this logo.
Many Muslims Brothers have given so many bad comments to Puma for there act. Many people have started promoting there statement to other people to stop using Puma/Nike products. People are boycotting Puma and sending this news to every person of the world and they are telling “Do Not Close Eyes”, see it and boycott Puma. This news has been promoted on forums, twitter, face book, communities and other blogs to boycott Puma.
Protesters are also telling that, people should take out those designs shows immediately at any cost. This can not be bearable. Not only Muslims, Hindus are also protesting Puma to stop selling those designs. You can see Hindu, Muslim comments on puma in face book, communities. Every person are protesting them and telling them to stop making those design.
Many people have written petition for Puma / Nike shoes act. There are many people over the world protested. It is really essential for Puma to stop making those designs, because people are boycotting them again and again.
Logo has been written in Arabic style, so people recognized it lately but when they recognized that it is the name of supreme power Allah (GOD). Then they started boycotting Puma and Nike.
Nike company has used a design for there shoes which almost look alike ‘Allah’ written in may languages mainly an Arabic style for writing Allah (God),supreme power of the whole world. As follower of any religion, it means we have faith in one superpower, so its our duty to make sure that Nike must stop using this design in future, because its a disgrace to Allah (God).Overall activity: 0%








 
 

Saturday, August 4, 2012

Muundelezo wa makala motomoto za Amir wako mstaafu.

                                              

Sifa njema anastahiki Allah (s.w), rehma na amani zimuuendee mbora wa viumbe mtume wetu Muhammad (s.a.w.) na Maswahaba zake na wale wote waliopita katika njia yake hadi siku ya mwisho..AMIN
Ni mwezi wa kufanya biashara na muumba wetu….ameweka mwezi huu kw kuwa Allah anahuruma ya kupitilza kwetu sisi…makala hii inaelezea nyakati muhimu za kujipinda sana katika mwezi huu wa Ramadhwaan:
Nyakati Tatu Muhimu Za Kufanya Ibada – Zisikupite Katika Ramadhaan
Nyakati tatu hizi ni muhimu sana za kufanya ibada kutokana na fadhila zake kuu. Mwenye kupenda kuchuma thawabu nyingi asizikose khaswa katika mwezi huu Mtukufu Wa Ramadhaan ambao ni mwezi wenye malipo maradufu
1-Wakati wa mwanzo: Baina ya Alfajiri na jua kuchomoza:
Usimulizi uliothibiti kutoka katika Swahiyh Muslim (564/1) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba walikuwa wakibakia macho wakati huo hadi jua kuchomoza kwani ni wakati mja anapogaiwa rizki yake, na ni wakati wenye kheri nyingi, unampa siha nzuri ya mwili binaadamu, na kwa ujumla ni wakati wenye baraka nyingi za kila aina kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba:
((اللهم بارك لأمتي في بكورها)) الترمذي, أحمد, أبي داود, ابن ماجه
((Ewe Allaah, wabarikie Ummah wangu nyakati za asubuhi mapema)) [At-Tirmidhiy, Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah na imethibitishwa kuwa ni Hadiyth Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy]
Usimulizi huu umetoka kwa Maswahaba kadhaa ambao wameelezea kwamba: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipotaka kupeleka kikosi au jeshi aliwapeleka mwanzo wa asubuhi". Vile vile wamesimulia kwamba: "Swakhar alikuwa mtu tajiri ambaye alikuwa akipelekea biashara zake mwanzo wa asubuhi na matokeo yake ilikuwa ni kufuzu katika biashara na kupata faida kubwa sana".
Wamesimulia Salafus-Swaalih kwamba Ibn 'Abbaas naye alimkataza mtu kulala nyakati hizo alipomwambia:
"قُم، أتنام في الساعة التي تقسَّم فيه الأرزاق؟"
"Inuka! Je, unalala katika saa ambayo rizki inagaiwa?"
Ikiwa basi wakati huo ni kama hivyo ilivyoelezwa juu, basi vipi Muislamu auache wakati huu umpite khaswa katika mwezi huu mtukufu wa Ramdhaan?
Ibnul-Qayyim (Rahimahu-Allaah) katika kitabu chake 'Zaad Al-Ma'aad' amesema: "Usingizi wa asubuhi unanyima rizki kwani huo ni wakati ambao Muumba anaombwa rizki na wakati wa kugaiwa rizki. Hivyo usingizi unanyima rizki isipokuwa kwa dharura. Usingizi wakati huo pia ni madhara kwa mwili…"
Faida nyingine kubwa ya kubakia macho ukimdhukuru Allaah wakati huu:
Si chini ya muda wa saa na nusu utakuwa umepata thawabu za Hajj na ‘Umrah kamilifu:
عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال (( من صلى الفجر في جماعة ثم قعد يذكر الله حتى تطلع الشمس ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة تامة تامة تامة) ) أخرج الترمذي صححه الألباني .
Imetoka kwa Anas kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jama'ah kisha akakaa anamkumbuka Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy na kaisahihisha Al-Albaaniy]
Pindi ukifanya hivyo kwa mwezi mzima utakuwa umechuma thawabu za Hajj na ‘Umrah mwezi mzima. Hizo ni fadhila za siku za kawaida, seuze ukifanya mwezi mtukufu huu wa Ramadhaan? Jitahidi ndugu Muislamu kadiri uwezavyo kuchuma hizi thawabu kubwa ambazo zingelikukalifu mali, tabu za safari na mashaka ya kufika Makkah kutekeleza ibada hizo. Lakini kwa Rahma ya Allaah Ametujaalia tuweze kuzichuma tukiwa majumbani mwetu tena kwa wepesi kabisa. Wanaume thawabu zitazidi ikiwa watatekeleza wakiwa misikitini. Wanawake wanazipata fadhila hizo hata wakiswali majumbani mwao. Hata hivyo, pamoja na ujira wote huu, tusisahau kuwa fadhila hizo hazivunji wala hazifuti fardh ya kwenda Hajj kwa mwenye uwezo, asije mtu akadhani kufanya hayo kutakuwa kumetengua wajiibu wake wa kuhiji au kufanya ‘Umrah.
2- Wakati wa pili: Kabla ya Jua kuzama (Magharibi):
Huu ni wakati ambao bado Muislamu yuko katika Swawm na du'aa yake anayoiomba hairudi:
قال صلى الله عليه وسلم: ((ثلاثة لا ترد دعوتهم: الصائم حتى يفطر والإمام العادل والمظلوم)) وروى الترمذي بسند حسن
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (([Watu] watatu du'aa zao hazirudi; mwenye kufunga hadi afuturu/afutari, Kiongozi muadilifu na aliyedhulumiwa)) [At-Tirmidhiy kwa isnaad nzuri]
Kwa hiyo ni fursa ya kuitumia Muislamu aombe du'aa na haja zake wakati huu khaswa pia kwa vile ni wakati ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amehimiza Atukuzwe kama Anavyosema:
(( وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ))
((.. na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa)) [Qaaf: 39]
((وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا وَمِنْ آنَاء اللَّيْلِ فَسَبِّحْ وَأَطْرَافَ النَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرْضَى))
((…Na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla halijachwa, na nyakati za usiku pia umtakase, na ncha za mchana ili upate ya kukuridhisha)) [Twaahaa: 130].
(( وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَار))
((…Na omba msamaha kwa dhambi zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi)) [Ghaafir: 55]
3- Wakati wa tatu: Suhuur - Kabla ya Alfajiri
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewaaahidi Wacha Mungu Pepo kwa sababu sifa mojawapo yao ni kuomba maghfira kabla ya Alfajiri:
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُون)) ((آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُحْسِنِينَ)) ((كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ)) ((وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُون))
((Hakika Wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na chemchem)) ((Wanapokea Aliyowapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema)) ((Walikuwa wakilala kidogo tu usiku)) ((Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfira)) [Adh-Dhaariyaat: 15-18]
Kisha wamesifiwa tena kwa sifa hiyo hiyo pamoja na nyinginezo:
((الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالأَسْحَارِ))
((Wanaosubiri, wanaosema kweli, na watiifu, na wanaotoa sadaka, na wanaoomba maghafira kabla ya Alfajiri)) [Al-'Imraan: 17]
Muislamu asiache wakati huo umpite kwani ni wakati muhimu na wenye fadhila na faida kubwa kwa vile Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Huteremka wakati huo kutoka mbingu ya saba na kuweko mbingu ya ardhi kutukidhia haja zetu:
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((ينزل ربنا تبارك وتعالى كل ليلة إلى السماء الدنيا حين يبقى ثلث الليل الآخر فيقول: من يدعوني فأستجيب له؟ من يسألني فأعطيه؟ من يستغفرني فأغفر له )) البخاري و مسلم
Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia (mbingu ya kwanza) inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani ana shida Nimtekelezee? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Nani miongoni mwetu asiyemhitaji Mola wake kumkidhia haja zake na kumuondeshea shida zake? Nani asiyekuwa na madhambi asiyemhitaji Mola wake kumghufuria? Hivyo usiache wakati huu ukakupita khaswa kwa vile mwezi huu Mtukufu ambao kila jambo ulifanyalo lina fadhila na thawabu marudufu.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuwezeshe kudiriki nyakati hizo tatu na nyingine, tuwe katika ibada katika mwezi huu wa Ramadhaan na miezi yote mingineyo na Atujaalie kheri na Baraka nyingi, Atukidhie haja zetu, Atuondoshee shida zetu na Atughufurie madhambi yetu yote. Aamiyn
Abuu khaythamah
Mussa Abdallah

Makala za Amir Mstaafu kwa Wanajumuiya na Waislamu wote.


                                                                     










...........ndugu zangu Wanajumuiya (MSATEKU) natamiza ahadi yangu ya kuwaletea makala yangu niliyowaahidi,karibu msome na mfahidike na yaliyomo inshallah Amin.........(Mussa Majugwe)
Kufanya Biashara Na Allaah Isiyoanguka  Kwa Kusoma Qur-aan
Sifa njema anastahiki Allah (s.w), rehma na amani zimuuendee mbora wa viumbe mtume wetu Muhammad (s.a.w.) na Maswahaba zake na wale wote waliopita katika njia yake hadi siku ya mwisho..AMIN;
Tukiwa tuko katika mwezi wa Ramadhwaan tunaweza tukaisoma Qur’an wakati huo huo tunafanya biashara isio na anguko na Allah……
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ))
(( لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ))
((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalah, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika Tulivyowaruzuku, hao hutaraji biashara isiyododa [isiyoanguka]))
((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani)) [Faatwir: 29-30]
Aayah hiyo ya mwanzo inajulikana kwamba ni 'Aaayatul-Qurraa' (Aayah wa wasomaji). Ni Aayah pekee katika Qur-aan inayojulikana hivyo. Anasema Shaykh Abu Bakar Al-Jazaairy katika kuifasiri kwake, kwamba: "Aayah hii inawahusu wale ambao wanaikhitimisha Qur-aan kila mwezi au chini ya mwezi". Na hivyo ndivyo Sunnah ilivyo kuikhitimisha Qur-aan kila mwezi kama ilivyo dalili katika usimulizi kwenye Al-Bukhaariy.
Biashara ya mwanzo ni kusoma Qur-aan. Biashara hii bila ya shaka itakuletea faida kubwa utakapoifanya mwezi huu mtukufu wa Ramadhaan kwa vile ndio mwezi ulioteremshwa Qur-aan:
((شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَان))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 185]
Vile vile:
حم ﴿1﴾  وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿2﴾ إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ ﴿3﴾  فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ ﴿4﴾
1.        Haa Miym
2.        Naapa kwa Kitabu kinachobainisha
3.        Hakika Tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima
[Ad-Dukhaan: 1-4]
Vile vile
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ
1. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul Qadr, Usiku wa Cheo Kitukufu)) [Al-Qadr: 1-5]
Kwa hiyo mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa Qur-aan na kuisoma kwa wingi ndivyo inavyopasa kwa kila Muislamu.Ikiwa kusoma herufi moja ni sawa na thawabu kumi kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ,
عن عبدالله بن مسعودٍ رضي الله عنه أن النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قال: (( من قَرأ حرفاً من كتاب الله فَلَهُ به حَسَنَةٌ، والحسنَةُ بعشْر أمْثالها، لا أقُول الم حرفٌ ولكن ألفٌ حرفٌ ولاَمٌ حرفٌ وميمٌ حرفٌ)) رواه الترمذي.
Imetoka kwa 'Abdillaah bin Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja)) [At-Tirimidhiy]
Utakaposoma tu:
﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
((Bismillahir-Rahmaanir-Rahiym))
ambayo ina herufi 19 hivyo 19 x 10 ni sawa na thawabu190.
Suratun-Naas (Qul A'uudhu Birabbin-Naas) ina herufi 80. Hivyo 80 x 10 = 800 thawabu ambazo utazichuma kwa chini ya dakika moja! Basi itakuwaje biashara hii utakapoifanya kwa kusoma ukurasa mzima? Au robo juzuu? Au nusu juzuu? Au juzuu nzima n.k.? Je, itakuwaje thawabu endapo utakhitimisha Qur-aan nzima?
Jibriyl alikuwa akiteremka kila Ramadhaan kumsikiliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akisoma Qur-aan na kumdarisisha:
"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ- أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ الْقُرْآنَ" رواه البخاري
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mbora (mwenye matendo mema) wa watu, na alikuwa mbora zaidi katika Ramadhaan kwa sababu Jibriyl alikuwa akimjia kila usiku wa Ramadhaan akimfundisha Qur-aan)) [Al-Bukhaariy]
Hali Za Maswahaba Na Salafus Swaalihiyn (Wema Waliotangulia) Na Qur-aan Katika Ramadhaan:
'Uthmaan bin 'Affaan alikuwa akikhitimisha Qur-an kwa siku moja.
Baadhi ya Salaf walikuwa wakikhitimisha kila siku tatu, wengineo kila wiki, wengineo kila kumi moja. Walikuwa wakiisoma Qur-aan katika Swalah na nje ya Swalah.
Imaam Ash-Shaafi'y alikuwa akikhitimisha Qur-aan mara nyingi mno katika Ramadhaan.
Al-Aswad alikuwa akhitimisha kila siku mbili.
Az-Zuhri alikuwa inapoingia Ramadhaan alijitenga na vikao vyote hata vya elimu na alikuwa akishughulika na kusoma Qur-aan pekee.
Salafus Swaalih aliyekuwa na duka, alikuwa akifunga duka lake mwezi wa Ramadhaan akishughulika kusoma Qur-aan pekee.
Adabu za kusoma Qur-aan:
1.        Kupiga mswaki
2.        Kuchukua wudhuu
3.        Kuelekea Qibla
4.        (Wanawake) kujifunika vizuri
5.        Kuelekea Qiblah
6.        Anza na Isti‘adha na BismiLLaah
7.        Soma kwa sauti ya kupendeza.
8.        Zingatia maneno ya Mola wako kwani ni amri kutoka Kwake:
((كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُوْلُوا الْأَلْبَابِ))
((Na hiki Kitabu, Tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aayah zake, na wawaidhike wenye akili)) [Swaad: 29]
1.        Unapopita kwenye Aayah za adhabu jikinge nazo; muombe Allaah Akuepushe na adhabu na moto, na unapopita katika Aayah za Rahma na Pepo usiache kumomba Allaah Akupatie hiyo pepo.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atubarikie wakati wetu na Atuwezeshe kuifanya biashara hii kwa wingi khaswa katika mwezi huu Mtukufu. Aamiyn.
Abuu khaythamah
Mussa Abdallah

Tuesday, July 24, 2012

Dua

Hakika ni dua njema kwa wanajumuiya wote pamoja na waislamu kuombea kila siku...........pia kumuomba Allah atubaliki...........
.
TUNDA LA NNE..........Hesabu kuelekea mwisho wa Ramadhan.
Watu wengi wameanza kuhesabu kwamba siku ya PILI au ya TATU,ama ya NNE tayari imepita lakini jiulize umeshafanya nini ndani ya mwezi huu kuanzia chungu MOSI ,PILI,TATU na kuendelea......umestaghafiru mara ngapi? Umewasema wangapi? Umeswali rakaa ngapi za Sunnah? Umesoma Qur-an juzuu au sura ngapi? Umetoa sadaka mara ngapi? TAFAKALI NDUGU MUISLAMU PIA CHUKUA HATUA........

Sunday, July 22, 2012

MINBARI YA RAMADHAN




  


 MINBARI YA RAMADHAN RAMADHANIMINBARI YA RAMADHANI
Hii ni kutokana na mnasaba wa kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani. Minbari ya Ramadhani itakuwa ikikuletea mawaidha yahusiyanayo na funga ya Ramadhani, ili uweze kuijua funga na hatimaye uweze kufunga kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kama alivyofunga Bwana Mtume -Rehema na Amani zimshukie - ambaye ndiye kigezo chetu chema. Sambamba na Minbari ya Ramadhani, BLOG yako ya MSATEKU itakuwa ikikuletea TUNDA LA RAMADHANI. Kupitia tunda la Ramadhani utajifunza hadithi mbili tatu za Mtume zihusianazo na funga tukufu ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani. Hadithi hizi zitakuwa zikifuatiwa na maelezo mafupi ili kuziweka wazi kwa wasomaji.
 i) MINBARI YA RAMDHANI NA KHUTBA YA MTUME KATIKA KUUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI :
Jueni na eleweni enyi ndugu zanguni Waislamu kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amejaalia mafanikio ya duniani ni ya muda mfupi, yenye kwisha na kuondoka, na mafanikio ya akhera ndiyo yenye kusalia/kubakia milele. Haya mafanikio ya kudumu, hayapatikani ila kwa kupitia barabara ngumu ya "TAQ-WA" kumcha Mwenyezi Mungu na kumtii na kumfuata Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie-. Katika jumla ya nguzo kuu za Taqwa ni kuufunga huu mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao Allah ameujaalia kuwa ni REHMA kwa viumbe. Nao kama mjuavyo ndio mwezi ambao imeteremshwa ndani yake Qur-ani Tukufu ikiwa ni muongozo kwa watu wote. Muongozo uliosheheni hoja wazi za uongofu na upambanuzi baina ya haki na batili. Ramadhani pia ni mwezi ambao hufunguliwa ndani yake milango ya pepo na kufungwa milango ya moto. Ni kwa kuuzingatia umuhimu na nafasi ya mwezi wa Ramadhani, ndipo Bwana Mtume akaitoa Khutba yake tukufu, khutba ya kihistoria, khutba kongwe katika kuupokea na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Imepokelewa na Salmaan Alfaarisy - Allah amuwie Radhi - amesema : Alitukhutubia Mtume wa Mwenyezi Mungu - Rehema na Amani zimshukie - katika siku ya mwisho ya mwezi wa Shaabani, akasema : "Enyi watu, umekufikieni mwezi mtukufu wenye baraka. Ndani ya mwezi huu umo usiku wa LAYLATIL QADRI usiku ambao ni bora kuliko miezi alfu moja. Mwenyezi Mungu amejaalia funga ya mwezi huu kuwa ni FARADHI na kisimamo (cha ibada) cha usiku wake kuwa ni SUNNAH. Atakayejikurubisha (kwa Mola wake) ndani ya mwezi huu kwa (kutenda) jambo lolote la kheri, (malipo, jazaa yake) itakuwa ni kama mtu aliyetekeleza fardhi katika miezi mingine. Na atakayetekeleza fardhi katika mwezi huu, atakuwa ni kama mtu aliyetekeleza fardhi sabini katika miezi mingine. Na mwezi huu ni mwezi wa SUBIRA, nao ni mwezi ambao mwanzo wake ni REHEMA na katikati yake ni MAGHFIRA/MSAMAHA WA ALLAH na mwisho wake ni KUACHWA HURU NA ADHABU YA MOTO. Yeyote atakayemfuturisha mfungaji ndani ya mwezi huu, (ujira wa futari hiyo) utakuwa ni maghfira ya madhambi yake (mfuturishaji) na kuachwa huru na adhabu ya moto na atapata ujira kama aupatao mfungaji bila ya kupungua chochote katika ujira/thawabu zake (mfungaji)". Tukasema : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sio sote tunaweza kupata (kitu) cha kumfuturisha huyo mfungaji. (Mtume) akawajibu : "Mwenyezi Mungu humpa thawabu hizi yule atakayemfuturisha mfungaji ndani ya mwezi huu kwa onjo/funda ya maziwa au (kokwa ya) tende au funda ya maji. Na atakayemshibisha ndani ya mwezi huu mfungaji, itakuwa ujira (wa shibe hiyo) ni maghufira ya madhambi yake (mshibishaji) na Mola wake atamnywesha katika hodhi (birika) langu funda moja ambayo hatopata kiu baada yake kabisa. Na atakuwa na ujira kama aupatao mfungaji bila ya kupungua chochote katika ujira wake (mfungaji). Na atakayempunguzia kazi mtumishi/mfanyakazi wake ndani ya mwezi huu, Mwenyezi Mungu atamghufiria madhambi yake na kumuacha huru na adhabu ya moto. Basi kithirisheni sana ndani ya mwezi huu mambo manne. Mtamridhisha Mola wenu kwa kutenda mambo mawili kati ya manne hayo; na mambo mawili hamjikwasii (hamna budi) nayo. Ama hayo mambo mawili mtakayoridhisha nayo Mola wenu ni shahada (kushuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ALLAH) na mumtake maghfira. Na ama yale mambo mawili msiyojikwasia nayo ni mumuombe Mola wenu pepo na mjilinde/mjikinge kwake na (adhabu) ya moto". Ibn Khuzaymah katika sahihi yake.
MAELEZO : Ikiwa tunafuatana pamoja, tunaweza tukaigawa hadithi hii tukufu ambayo ni khutba kongwe iliyo hai hadi leo na itaendelea kuwa hai mpaka mwisho wa dunia. Khutba hii iliyotolewa na Khatibu mahiri, Bwana Mtume katika kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, inagawanyika katika sehemu kuu tatu au tuseme ina vipengele vikuu vitatu. Ukiizingatia hadithi utakuta mwanzo wa khutba yake, Bwana Mtume - Rehema na Amani zimshukie - anawafahamisha maswahaba na umma mzima juu ya utukufu, ubora, cheo na nafasi ya mwezi wa Ramadhani. Kuna hekima/falsafa gani ndani ya maelezo haya ? Mtume anauelezea mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa namna gani ili muislamu aujue, kwani waswahili husema asiyekujua hakuthamini. Akishaujua atauthamini na kuupa hadhi yake unayostahili. Kuuthamini na kuupa heshima mwezi wa Ramdhani ni kuzidisha sana TWAA kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya namna mbali mbali za ibada na mambo mengine ya kheri.
Sehemu ya pili ya hadithi, Bwana Mtume anataja fadhila/faida na ubora wa mwezi wa mtukufu wa Ramadhani na kuwa ibada yeyote inayofanywa ndani ya mwezi huu hailingani kithawabu/kiujira na ile ibada inayofanywa katika miezi mingine. Kwa hiyo basi, Ramadhani ni ndio musimu wako wa ibada. Kadhalika Bwana Mtume anatuelezea malipo na thawabu adhimu anazozipata mja mwenye kumfuturisha nduguye muislamu katika mwezi huu wa Ramadhani. Hapa Bwana Mtume anaashiria moyo wa ukarimu na upendo utakiwao waislamu wajipambe na kuwa nao. Kwani waislamu wakipendana watakuwa ni wamoja na mshikamano, na wakishikamana watautawala ulimwengu na hapatakuwa na nguvu ya kuwashinda, si magharibi wala mashariki.
Kisha ndipo Bwana Mtume akaikhitimisha khutuba yake kwa kutoa wito muhimu kwa waislamu. Akawataka wakithithirishe sana kumpwekesha Mola wao kwa kuleta kalima ya shahada na wamtake sana maghfira. Hali kadhalika akawataka waislamu wakithirishe mno kumuomba Mola wao pepo na wamuombe awakinge na moto wa jahanamu. Ili kuutekeleza wito huu ndipo wanazuoni wetu wema -Allah awarehemu- wakatuwekea uradi uletwao msikitini ndani ya mwezi wa Ramadhani. Chimbuko la uradi huu ni ile sehemu ya mwisho ya hadithi. Uradi wenyewe ni huu :
ASH-HADU AN LAA ILAHA ILLA-LLAHU NASTAGHFIRULLAH, NAS-ALUKAL-JANNATA WANA'UDHU BIKA MINAN-NAAR ALLAHUMMA INNAKA AFUWWUN, TUHIBBUL-AFWA FA'FU 'ANNAA YAA KARIIM
Tunashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah, Tunakuomba maghfira (msamaha wa madhambi) Ewe Allah, Tunakuomba pepo na tunajikinga kwako na moto, Ewe Allah, wewe mimi ni msamehevu na unapenda msamaha, basi tusamehe Ewe KARIMU.
Haya shime ndugu zanguni waislamu, tukithirishe kuuleta uradi huu ndani ya mwezi wa mavuno; mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeuitikia wito wa Bwana Mtume kwa maslahi na faida yetu wenyewe.
TUNDA LA RAMADHANI :
Karibu ndugu yangu muislamu katika bustani ya Bwana Mtume -Rehema na Amani zimshukie - uchume utakavyo na kula kiasi chako matunda matamu, mazuri yasiyokwisha hamu; matunda ya Ramadhani. Ili ufaidike na kunufaika na matunda haya unatakiwa uingie ndani ya bustani hii tukufu kwa unyenyekevu, utulivu, adabu, heshima na usikivu.
TUNDA LA KWANZA - DUA YA KUFUTURU
Amepokea Ibn Majah kutokana na hadithi ya Abdillah Ibn Amri (amesema Mtume) : YUNA MFUNGAJI WAKATI WA KUFUTURU KWAKE DUA ISIYOREJESHWA (yenye kujibiwa bila ya kipingamizi)". Ni kwa sababu hiyo ndiyo Mtume alikuwa akisema (wakati wa kufuturu) :
[ALLAHUMMA INNIY LAKA SWUMTU WA'ALAA RIZQIKA AFTWARTU FAGH-FIRLIY MAA QADDAMTU WA MAA AKHARTU DHAHABAD-DHWAMAU WABTALLIT-'URUQU WATHABATAL AJRU IN-SHAALLAHU TAALA]
Maana yake : "Ewe Mola wa haki ni kwa ajili yako tu nimefunga na nimefuturu kwa riziki yako. Basi (nakuomba) unisamehe dhambi zangu zilizotangulia na zijazo. Kiu kimeondoka na mishipa imelowana na ujira umethibiti pindipo atakapo Mwenyezi Mungu Mtukufu"
Haya shime ndugu zanguni waislamu, tumuige Mtume wetu katika hili na mengineyo ili tutengenekewe duniani na akhera. Usikubali kuipoteza fursa hii adimu ya kukubaliwa duao, omba na Mola Karimu atakupa.
TUNDA LA PILI : FADHILA ZA KUHARAKIA KUFUTURU :
Imepokelewa hadithi kutoka kwa Abuu Hurayrah - Allah amuwie Radhi - amesema, Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu - Rehema na Amani zimshukie- "AMESEMA MWENYEZI MUNGU : HAKIKA WAJA WANGU WAPENDEZAO SANA KWANGU NI WALE WAHARIKIAO KUFUTURU" Ahmad na Tirmidhi.
MAELEZO : Ni vema mtu akafanya haraka kufuturu, maadam ana uhakika wa kutua/kuzama kwa jua. Ikiwa hana uhakika, basi ni vema akasubiri adhana ili asije akafuturu kabla ya muda. Haya zingatia upendwe na Mola wako.

TUNDA LA TATU:Vipi Umsaidie Mwanao Afunge Mwezi Wa Ramadhani?

Ndungu Zangu katika iman(mwanajumuiya)Siyamu Ya Mtoto Ni Mas'uliya Ya Mama ,kabla ya Baba .. Nimas'uliya Kubwa Kwasababu Mtoto Hajuwi Umuhimu Wa Siyamu Katika Umri wake..Mama Mtu Anashtuka Kuwa Mtoto Wake Anamwambiya Kuwa Yeye Kafunga Lakini Hajuwi Kuwa Mwanawe Anakula.
Ndugu Zangu Kina Mama hata akina baba, Ukijuwa Kuwa Mtoto Wako Alikuwa Akila Nahuku Akikuwambiya Kuwa Yeye Kafunga Fanya yafuatayo :

1: Ukishamjua Mtoto Anafunga jaribu Kumpa vijizawadi Kwa Kila Siku
Anayo Funga. Au muwahiidi zawadi katika sikukuu ya IDD,kwa mfano kumnunulia nguo nzuri au viatu vizuri.

2: Usimfokee Na Kumwambia Kuwa Wewe Unasema Uwongo Unajidai
Umefunga Lakini Unakula Nyuma Yangu ...mwambiye Kwa Njiya
Nyengine Na Kumtolea Hadithi Za Watoto Walokuwa Wakisema
Uwongo Kwa Wazee Wao Na Natija Yake Bila Yeye Kuhisi
Unamkusudia Yeye.

3: Kumfundisha Mtoto Kufunga Kidogo Kidogo Kwa Mujibu wa Umri
Wake.

4: Kumsifu Mbele Ya Wenziwe Anapo Funga.

5: Hakikisha unawaunganisha a wanaofunga Katika Family kwa
Kufturu Pamoja Ili Ajuwe Kuwa Alokuwa Hawafungi wanafanya Makosa.

6: Usiweke Chakula Anachokipenda Mtoto Wako Mbele Yake
(sweets) Kabla Ya Iftar Akaja Akadhaifika.

7: Ahisi Mtoto Wako Katika Mwezi Mtukufu Wa Ramadhan Umuhimu
Wa Mwezi Wa Ramadhani .. Kumchukuwa Katika Darsa Kukaa Naye
Nakusoma Quraan na Hadith ...



Thursday, July 19, 2012

Mara baada ya chakula, maongezi ya kubadilisha mawazo katika mambo mbalimbali hususani katika masuala ya maendeleo na taarifa mbalimbali yalianza......
Hawa nao waliahakikisha nyama ya mbuzi inatendewa haki.........brother Dadi na Omary bin Said