Kufanya Biashara Na Allaah
Isiyoanguka Kwa Kusoma Qur-aan
Sifa njema anastahiki Allah (s.w), rehma na amani zimuuendee mbora wa
viumbe mtume wetu Muhammad (s.a.w.) na Maswahaba zake na wale wote waliopita
katika njia yake hadi siku ya mwisho..AMIN;
Tukiwa tuko katika mwezi wa Ramadhwaan tunaweza tukaisoma Qur’an
wakati huo huo tunafanya biashara isio na anguko na Allah……
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ
كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا
وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ))
(( لِيُوَفِّيَهُمْ
أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ))
((Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na
wakasimamisha Swalah, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika
Tulivyowaruzuku, hao hutaraji biashara isiyododa [isiyoanguka]))
((Ili Yeye Awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na
Awazidishie kutokana na fadhila Zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye
shukrani)) [Faatwir: 29-30]
Aayah hiyo ya mwanzo inajulikana kwamba ni 'Aaayatul-Qurraa'
(Aayah wa wasomaji). Ni Aayah pekee katika Qur-aan inayojulikana hivyo. Anasema
Shaykh Abu Bakar Al-Jazaairy katika kuifasiri kwake, kwamba: "Aayah hii
inawahusu wale ambao wanaikhitimisha Qur-aan kila mwezi au chini ya
mwezi". Na hivyo ndivyo Sunnah ilivyo kuikhitimisha Qur-aan kila mwezi
kama ilivyo dalili katika usimulizi kwenye Al-Bukhaariy.
Biashara ya mwanzo ni kusoma Qur-aan.
Biashara hii bila ya shaka itakuletea faida kubwa utakapoifanya mwezi huu
mtukufu wa Ramadhaan kwa vile ndio mwezi ulioteremshwa Qur-aan:
((شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ
أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى
وَالْفُرْقَان))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo
Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na
upambanuzi)) [Al-Baqarah: 185]
Vile vile:
حم ﴿1﴾ وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿2﴾ إِنَّا
أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ ﴿3﴾ فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ
﴿4﴾
1.
Haa
Miym
2.
Naapa
kwa Kitabu kinachobainisha
3.
Hakika
Tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.Katika usiku
huu hubainishwa kila jambo la hikima
[Ad-Dukhaan: 1-4]
Vile vile
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ
الْقَدْرِ
1.
Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul Qadr, Usiku wa Cheo
Kitukufu)) [Al-Qadr: 1-5]
Kwa hiyo mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa
Qur-aan na kuisoma kwa wingi ndivyo inavyopasa kwa kila Muislamu.Ikiwa kusoma
herufi moja ni sawa na thawabu kumi kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
,
عن
عبدالله بن مسعودٍ رضي الله عنه أن النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قال: (( من قَرأ
حرفاً من كتاب الله فَلَهُ به حَسَنَةٌ، والحسنَةُ بعشْر أمْثالها، لا أقُول الم
حرفٌ ولكن ألفٌ حرفٌ ولاَمٌ حرفٌ وميمٌ حرفٌ)) رواه الترمذي.
Imetoka kwa 'Abdillaah bin Mas'uud (Radhiya
Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema, ((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata hasanah
(jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi
'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi
moja na Miym ni herufi moja)) [At-Tirimidhiy]
Utakaposoma tu:
﴿
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
((Bismillahir-Rahmaanir-Rahiym))
ambayo ina herufi 19 hivyo 19 x 10 ni
sawa na thawabu190.
Suratun-Naas (Qul A'uudhu Birabbin-Naas)
ina herufi 80. Hivyo 80 x 10 = 800 thawabu ambazo utazichuma kwa chini ya
dakika moja! Basi itakuwaje biashara hii utakapoifanya kwa kusoma ukurasa
mzima? Au robo juzuu? Au nusu juzuu? Au juzuu nzima n.k.? Je, itakuwaje thawabu
endapo utakhitimisha Qur-aan nzima?
Jibriyl alikuwa akiteremka kila Ramadhaan
kumsikiliza Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akisoma Qur-aan na kumdarisisha:
"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ -صَلَّى
اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ-
أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ وَكَانَ
يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ
فَيُدَارِسُهُ الْقُرْآنَ" رواه البخاري
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) alikuwa ni mbora (mwenye matendo mema) wa watu, na alikuwa mbora zaidi
katika Ramadhaan kwa sababu Jibriyl alikuwa akimjia kila usiku wa Ramadhaan
akimfundisha Qur-aan)) [Al-Bukhaariy]
Hali Za
Maswahaba Na Salafus Swaalihiyn (Wema Waliotangulia) Na Qur-aan Katika
Ramadhaan:
'Uthmaan bin
'Affaan alikuwa akikhitimisha Qur-an kwa siku moja.
Baadhi ya Salaf
walikuwa wakikhitimisha kila siku tatu, wengineo kila wiki, wengineo kila kumi
moja. Walikuwa wakiisoma Qur-aan katika Swalah na nje ya Swalah.
Imaam
Ash-Shaafi'y alikuwa akikhitimisha Qur-aan mara nyingi mno katika Ramadhaan.
Al-Aswad alikuwa
akhitimisha kila siku mbili.
Az-Zuhri alikuwa
inapoingia Ramadhaan alijitenga na vikao vyote hata vya elimu na alikuwa
akishughulika na kusoma Qur-aan pekee.
Salafus Swaalih
aliyekuwa na duka, alikuwa akifunga duka lake mwezi wa Ramadhaan akishughulika
kusoma Qur-aan pekee.
Adabu za
kusoma Qur-aan:
1.
Kupiga
mswaki
2.
Kuchukua
wudhuu
3.
Kuelekea
Qibla
4.
(Wanawake)
kujifunika vizuri
5.
Kuelekea
Qiblah
6.
Anza
na Isti‘adha na BismiLLaah
7.
Soma
kwa sauti ya kupendeza.
8.
Zingatia
maneno ya Mola wako kwani ni amri kutoka Kwake:
((كِتَابٌ
أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ
أُوْلُوا الْأَلْبَابِ))
((Na hiki Kitabu,
Tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aayah zake, na wawaidhike
wenye akili)) [Swaad: 29]
1.
Unapopita
kwenye Aayah za adhabu jikinge nazo; muombe Allaah Akuepushe na adhabu na moto,
na unapopita katika Aayah za Rahma na Pepo usiache kumomba Allaah Akupatie hiyo
pepo.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
Atubarikie wakati wetu na Atuwezeshe kuifanya biashara hii kwa wingi khaswa
katika mwezi huu Mtukufu. Aamiyn.
Abuu khaythamah
Mussa Abdallah
No comments:
Post a Comment