Saturday, August 18, 2012

EID MUBARAK BROTHERS AND SISTERS....!!!!!!


In The Name Of God The Most Merciful, Most Compassion

Eid Mubarak 2012 from MSATEKU

 

Eid Message from MSATEKU
It is with mixed emotions we approach the end of Ramadhan and Eid-Al-Fitr. We are extremely thankful and grateful to Allah Ta’ala for allowing us to benefit from the enormous spiritual benefits of Ramadhan, the fasting, taraweeh salaah, charity, recitation of Qur’aan etc. At the same time we are sad that this Mubarak and auspicious month is coming to an end.
For a true believer everyday of his or her life should be spent like how we generally spend our precious time in Ramadhan, full of virtuous acts.
Let us formulate strategies and ways to uphold this spirit and actions. Remember true and eternal happiness, bliss and joy can only be achieved by leading our lives according to the Commandments of Allah Ta’ala and following the beautiful and noble lifestyle (sunnah) of His Beloved Messenger Muhammad (S.A.W).
We should also remember that while we celebrate the joyous day of Eid-ul-Fitr there are millions of our brothers and sisters who are being oppressed and persecuted. Let us not forget about them. Let us enjoy this day of Eid in a manner pleasing to our Creator and Sustainer Allah Ta’ala.
We wish Eid Mubarak to you and your family and May Allah Ta’ala bless and grant you barakah (blessings) in this world and the akhirah(hereafter) .
May Allah accept your fasting and duas. Let us remember the Ummah which is in pain and distress in many parts of the world and if possible let us contribute in whatever way possible whether it be financially or by way of your sincere duas.
Make dua for those who have passed on.May Allah grant relief to those in need especially who wants to over through their supplemantaries and even Carries at TEKU(please believe on Him........
May Allah ease the plight of so many that are downtrodden and oppressed .
May Allah grant Shi’fa to those that are ill and may ALLAH grant us a death with Emaan and true success in both this world and the hereafter…Ameen
Eid Mubarak from the entire team at MSATEKU

Friday, August 17, 2012

zawadi ya Ummu Ayman kwa dada zangu




Assalam alaykum dada zangu wa kiislam...........!!!!Amir wenu mstaafu leo nawausia tena kwa mara nyingine tena..........karibuni sana mnifuatilie katika makala hii tena.......natanguliza zangu shukrani......lakini pia ni makala mhimu hata kwa BROTHERS kwa hiyo tushilikiane....


Imetafsiriwa na: Ummu Ummu Ayman
Sifa njema ni za Allaah, Bwana wa Ulimwengu, na rehma na amani zimshukie
Mtume wetu Muhammad na Aali zake na Swahaba zake.
“'Iyd” ni neno la kiarabu linalomaanisha jambo la kitabia au ada, lenye kurudi na
kujirejea. 'Iyd au sikukuu ni alama au nembo inayopatikana katika kila taifa, ikiwa
ni pamoja na mataifa yale yaliyotajwa katika vitabu vitukufu na yale ya waabudiao
masanamu, pamoja na wengineo, kwa sababu kusherehekea sikukuu ni jambo la
kimaumbile katika maumbile ya mwanaadamu. Watu wote wanapenda kuwa na
matukio maalumu ya kufanya sherehe, ambapo wanaweza kukukusanyika pamoja
na kuonyesha furaha zao.
Sikukuu za mataifa ya makafiri zinaweza kufungamanishwa na mambo ya kidunia,
kama kuanza kwa mwaka, kuanza kwa msimu wa kilimo, kubadilika kwa hali ya
hewa, kuanzishwa kwa dola, kutawazwa kwa kiongozi, n.k. Zinaweza pia
kufungamanishwa na matukio ya kidini, kama ambavyo nyingi ya sikukuu
zinazowahusu Mayahudi na Wakiristo tu, mfano Alkhamiys ambayo wanadai kuwa
meza maalum iliteremshwa kwa Yesu, Krismas, Mwaka Mpya, Siku ya
kushukuriana, na sikukuu ambazo watu hupeana zawadi. Hizi husherehekewa
katika nchi zote za Ulaya na Amerika ya Kaskazini hivi sasa, na katika nchi
nyengine ambazo ukristo una nguvu, hata kama nchi yenyewe si ya kikiristo
kiuhalisi. Baadhi ya wanaoitwa Waislam huweza kujiunga katika sikukuu hizi, kwa
sababu ya ujinga au unafiki.
Wamagiani (Magians) nao pia wana sikukuu zao, kama Mahrajaan, Namrud n.k.
Ma-baatini (Miongoni mwa Mashia) wana sikukuu zao pia, kama ‘Iyd al-Ghadiyr,
ambapo wanadai kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amempa ukhalifa ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) na maimamu kumi na moja baada
yake.
Waislamu Wanatambulika Kwa Sikukuu Zao
Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) "Kila Umma una
sikukuu yake na hii ni sikukuu yenu" yanaonyesha kuwa ‘Iyd hizi mbili ni maalumu
kwa Waislamu tu, na kuwa hairuhusiwi kwa Muislam kuwaiga makafiri na
washirikina katika jambo lolote ambalo ni maalumu ndani ya sherehe zao, iwapo
kama ni chakula, nguo, kuwasha moto au matendo ya ibada.
Watoto wa Kiislam wasiruhusiwe kucheza katika sikukuu hizo za kikafiri, au
kujipamba, au kujumuika na makafiri katika matukio hayo. Sikukuu zote za kikafiri
au zilizozushwa ni haraam, mfano kama sherehe za Siku ya Uhuru, maadhimisho
ya mapinduzi, miti ya sherehe za sikukuu au kutawazwa kwa kiongozi, siku za
kuzaliwa, Sikukuu ya Wafanyakazi, Sikukuu ya Nile, Shamm an-Nasiym (sikukuu
ya majira ya baridi ya Wamisri), siku ya walimu, na Maulidi ya Mtume (Kuzaliwa
kwa Mtume).
Waislam hawana sikukuu ukiacha ile ya ‘Iyd al-Fitwr na ‘Iyd al-Adhw-haa, kwa
sababu ya hadiyth iliyotolewa na Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
"Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja Madiynah
na watu walikuwa na siku mbili wakicheza na kufurahi. Akauliza, "Ni siku gani hizi
mbili?" Wakasema, "Tulikuwa tukicheza na kufurahi katika siku hizi zama za
ujaahiliyya" (zama za ujinga kabla ya Uislamu). Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) akasema, "Allaah Amekupeni siku bora kuliko hizo, nazo ni siku
ya ‘Iyd Al-Adhw-haa na siku ya ‘Iyd Al Fitwr". (Sunan Abi Daawuud 1134)
Yafuatayo ni maelezo kuhusu shari'ah na adabu za ‘Iyd mbili kwa mujibu wa
Sharia ya Kiislam:
Ahkaamul-'Iyd (Shari'ah Katika 'Iyd)
Kufunga
Ni haraam kufunga katika siku za ‘Iyd kutokana na hadiyth ya Abu Sa’iyd al-
Khudriy (Radhiya Allaahu ‘anhu), amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) amekataza kufunga katika siku ya Fitwr na katika siku ya
Kuchinja (Adhw-haa). (Imeripotiwa na Muslim, 827)
Shari'ah Katika Swalah Za 'Iyd
Baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa Swalah ya ‘Iyd ni waajib, huu ni mtizamo
wa wanavyuoni wa Kihanafi na Shaykh al-Islam Ibn Taymiyah (rahimahu Allaah).
Wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa
akiswali Swalah zote za ‘Iyd na hakuacha kufanya hivyo hata mara moja.
Wamechukua ushahidi katika ayah (yenye tafsiri),
"Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi" Al-Kawthar: 2
Yaani Swalah ya ‘Iyd na kuchinja baada yake, ambayo ni amri, na kwa ukweli
kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamrisha wanawake
watolewe kuhudhuria Swalah ya ‘Iyd, na kwamba mwanamke aliyekuwa hana
jilbaab aazime kutoka kwa ndugu yake
Baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa Swalah ya ‘Iyd ni Fardhu Kifaayah (fardhi
yenye kutosheleza). Huu ni mtizamo wa Kihanbali. Kundi la tatu linasema kuwa
Swalah ya ‘Iyd ni Sunnah iliyokokotezwa. Huu ni mtizamo wa Kimaalik na Kishaafi.
Wanachukua ushahidi ya hadiyth ya Bedui inayosema kuwa Allaah (Subhaanahu
Wa Ta’ala) Hakufaradhisha Swalah yoyote kwa waja Wake zaidi ya zile Swalah
tano. Kwa hiyo Waislam wafanye hima kuhudhuria Swalah ya ‘Iyd, hususan kwa
kuwa maoni ya kuwa ni waajib yameegemea katika ushahidi wenye nguvu.
Neema, baraka na malipo makubwa yanapatikana kwa kuhudhuria Swalah za ‘Iyd,
na kwa ukweli kuwa mtu atakuwa anafuata mwendo wa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kufanya hivyo, basi inatosha kuwa ni
changamoto.
Mambo Ya Lazima Na Wakati Wa Swalah Ya 'Iyd
Baadhi ya wanavyuoni wa Kihanbali wanasema kuwa sharti za Swalah ya ‘Iyd ni
iqaamah lazima isomwe na ni lazima iswaliwe kwa jamaa. Baadhi yao wamesema
kuwa sharti za Swalah ya ‘Iyd ni sawa na zile za Swalah ya Ijumaa, isipokuwa
katika khutba, ambapo kuihudhuria si lazima. Wengi miongoni mwa wanavyuoni
wanasema wakati wa Swalah ya ‘Iyd unaanza pale jua linapochomoza kwa masafa
ya urefu wa mshale, kwa linavyoonekana kwa macho matupu, na unaendelea
mpaka jua linapokaribia kuwa sawa sawa.
Maelezo Ya Swalah Ya 'Iyd
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “ Swalah ya ‘Iyd Fitwr na al-Adhw-haa
ni rakaa mbili zilizotimia, sio fupi fupi. Hii ni kwa mujibu wa maneno ya Mtume, na
muongo ni mwenye kulaaniwa.”
Abu Sa’iyd amesema: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amekuwa akija katika pahala pa kuswalia katika siku za Fitwr na al-Adhw-haa, na
jambo la mwanzo analofanya ni kuswali”.
Takbira inarejewa mara saba katika rakaa ya mwanzo na mara tano katika rakaa
ya pili, Qur-aan inasomwa baada yake katika kila rakaa.
Imeripotiwa kutoka kwa A’ishah: Takbira ya al-Fitwr na al-Adhw-haa ni mara saba
katika rakaa ya mwanzo na mara tano katika rakaa ya pili, mbali na Takbira ya
rukuu. (imeripotiwa na Abu Daawuud; imesahihishwa na jumla ya isnaad)
Iwapo mtu amejiunga na Swalah amemuwahi Imaam wakati wa Takbira hizi za
ziada, ni juu yake kusema “Allaahu Akbar” pamoja na Imaam, na halazimiki
kuzilipa Takbira ambazo zimempita, kwa sababu (takbira hizo) ni Sunnah, sio
waajib. Kuhusu nini kinatakiwa kisemwe baina ya Takbira, Hammaad ibn Salamah
ameripoti kutoka kwa Ibraahiym kuwa "Waliyd ibn ‘Uqbah aliingia msikitini wakati
Ibn Mas’uud, Hudhayfah na Abu Muusa wapo hapo, na akasema, “‘Iyd ipo hapa,
nini natakiwa kufanya?” Ibn Mas’uud akasema: “Sema ‘Allaahu Akbar’, msifu na
mshukuru Allaah, msalie Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na
omba du’aa, kisha sema ‘Allaahu Akbar’, msifu na mshukuru Allaah, mswalie
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)….n.k.’ (Imeripotiwa na at-
Twabaraaniy. Ni hadiyth sahihi iliyonukuliwa katika al-Irwaa’ na kwengineko).
Kusoma Qur-aan Katika Swalah Za 'Iyd
Imependekezwa (mustahabb) kuwa katika Swalah za ‘Iyd, imaam asome surat
Qaaf (sura ya 50) na surat al-Qamar (sura ya 54), kama ilivyoripotiwa katika
Swahiyh Muslim kuwa ‘Umar ibn Al-Khattwaab alimuuliza Abu Waaqid al-Laythi,
“Nini Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa
akisoma katika [‘Iyd] al-Adhw-haa na al-Fitwr?” Akasema, “Alikuwa akisoma Qaaf,
Wal-Qur-aan al-Majiyd [Qaaf 50:1] na Iqtarabat as-saa’ah wa’nshaqq al-qamar
[al-Qamar 54:1].
Ripoti nyingi zinaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alikuwa akisoma Surat al A’laa [87] na Suurat al-Ghaashiyah {88], kama ambavyo
alivyokuwa akizisoma katika Swalah ya Ijumaa. An-Nu’maan ibn Bashiyr
amesema:
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika '‘Iyd
mbili na siku ya Ijumaa Sabbih Isma Rabbikal-a'laa (Al-A'alaa 87:1) na Hal Ataaka
Hadiythul-Ghaashiyah (Al-Ghaashiyah 88:1)" Swahiyh Muslim 878
Samurah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika ‘Iyd mbili Sabbih Isma Rabbikal-a'alaa
(Al-a'alaa 87:1) na Hal Ataaka Hadiythul-Ghaashiyah (Al-Ghaashiyah 88:1)
Imesimuliwa na Ahmad na wengine ni Swahiyh [ Al-Irwaa 3/116]
Swalah Inaswaliwa Kabla Ya Khutbah
Moja ya shari'ah za ‘Iyd ni kuwa Swalah ni lazima iwe kabla ya khutbah, kama
ilivyoripotiwa katika Musnad Ahmad kutoka katika hadiyth ya Ibn ‘Abbaas, ambaye
ameshuhudia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali
kabla ya khutba siku ya ‘Iyd kisha akatoa khutba (Musnad Ahmad 1905. Hadiyth
hii pia iko katika Swahiyh mbili)
Yeyote Anayetaka Kuondoka Wakati Wa Khutbah Ameruhusiwa Kufanya
Hivyo
‘Abd-Allaah ibn al-Saab amesema: "Nilihudhuria '‘Iyd pamoja na Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na alipomaliza alisema, tutatoa khutba, kwa
hiyo anayetaka kukaa (na kusikiliza) khutba basi akae na anayetaka kuondoka
basi aondoke (Irwaa al Ghaliyl 3/96)
Swalah Isicheleweshwe Kwa Muda Mrefu
‘Abd-Allaah ibn Bishr, swahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam), alitoka pamoja na watu siku ya al-Fitwr au al-Adhw-haa, na akaonyesha
kutopendezwa kwa kuwa Imaam alikuja akiwa amechelewa sana. Akasema:
"Wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tungelikuwa
tumeshamaliza wakati wa sasa" na huo ulikuwa wakati wa Tasbiyh” (Imesimuliwa
na na Al-Bukhaariy).
Swalah Za Sunnah, Pahala Pa Swalah (Ya 'Iyd)
Hakuna Swalah za Sunnah ambazo zinaswaliwa kabla au baada ya Swalah ya ‘Iyd,
kama alivyoripoti Ibn ‘Abbaas kuwa "Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) alikuwa akitoka katika siku ya ‘Iyd na akaswali rakaa mbili, bila ya
chochote (Swalah yoyote) kabla au baada yake". Hali hii ni iwapo Swalah
itaswaliwa pahala pa kuswaliwa au sehemu ya wazi. Hata hivyo, iwapo watu
wataswali ‘Iyd msikitini, basi watatakiwa waswali rakaa mbili za Tahiyat al-Masjid
(Swalah ya kiamkizi cha msikiti) kabla hawajakaa kitako.
Iwapo Watu Hawatokuwa Na Habari Ya 'Iyd Mpaka Siku Ya Pili
Abu ‘Umayr ibn Anas ameripoti kutoka kwa ‘ami yake miongoni mwa Answaar
kuwa alisema: "Kulikuwa na mawingu na hatukuweza kuuona mwezi wa
Shawwaal, kwa hiyo tukaanza siku kwa kufunga, kisha ukaja msafara mwisho wa
siku na wakamwabia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa
wameona mwezi wa Shawwaal siku moja kabla, akawaambia watu waache
kufunga na wakaenda kuswali ‘Iyd siku ya pili" Imeripotiwa na Maimaam watano,
ni Sahiyh; Al-Irwaa' 3/102
Iwapo mtu amekosa Swalah ya ‘Iyd, mtazamo ulio sahihi kuliko yote ni kuwa
anaweza kuilipa kwa kuswali rakaa mbili.
Kuhudhuria Kwa Wanawake Katika Swalah Za 'Iyd
Hafswah (Radhiya Allaahu ‘anha) amesema: "Tulikuwa tukiwazuia wasichana
wenye hedhi kuhudhuria Swalah za ‘Iyd. Kisha akaja mwanamke kukaa katika
ngome ya Banu Khalaf na akatuambia kuhusu dada yake. Mume wa dada yake
alihudhuria vita kumi na mbili pamoja na Mtume (na akasema) , Dada yangu
alikuwa naye katika vita sita. Akasema tulikuwa tukiwatendea walioumia na
tukiwashughulikia wagonjwa. Dada yangu alimuuliza Mtume kama kuna ubaya
wowote kutokwenda kuswali ‘Iyd ikiwa hana jilbaab. Akasema "mwache rafiki yake
ampe moja wa jilbaab lake ili aweze kushuhudia baraka za ‘Iyd na aone kujumuika
kwa Waislamu" Ummu 'Atwiyah alipokuja nilimuuliza umemiskia Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema hivyo?" Akasema "Baba yangu
achinjwe kwa ajili yake" Na alikuwa hamtaji ila baada ya kusema "baba yangu
achinjwe kwa ajili yake". "Nimemsikia akisema kuwa wasichana na wale
wanaotawishwa au wasichana waliotawishwa na wanawake wenye hedhi ili
washuhudie baraka za ‘Iyd na kujumuika kwa waumini. Lakini wale wenye hedhi
wakae mbali na sehemu ya kuswali" (Swahiyh Al-Bukhaariy)
Vijana wa kike (‘awaatik, mmoja ‘aatiq) ni wale waliokwisha vunja ungo au wako
karibu na kufanya hivyo, au wamefikia umri wa kuolewa, au walio na thamani
katika familia zao, au wasiofanyishwa kazi zisizo na heshima. Inaonekana kuwa
wamekuwa wakizuiwa vijana hawa kutoka nje kwa sababu ya uovu uliojitokeza
baada ya kizazi cha kwanza cha Uislam; lakini Swahaabah hawakukubaliana na
hilo na wakaona kuwa shari'ah ya wakati wao lazima ibaki kama ilivyokuwa wakati
wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
“Jilbaab lake”- ametakiwa kuazima baadhi ya nguo ambazo hakuwa akizihitajia.
“Wanaotengwa/Wanaotawishwa”- ambao wanaowekewa paazia kipembeni mwa
nyumba ambamo wari hukaa nyuma yake.
“Wanawake walio katika hedhi”- huyyadh, mmoja haaidh– hii inaweza kurejea kwa
vijana wa kike waliofikia umri wa kukua, au wanawake waliomo katika siku zao na
wasio tohara.
“Wanawake walio katika hedhi wanatakiwa wajitenge na Swalah – pahala
penyewe” – Ibn al-Munayyir amesema: "Sababu ya kujitenga na sehemu ya
kuswali ni kuwa wakisimama pamoja na wanawake wanaoswali japokuwa
hawaswali, itaonekana kuwa hawana heshima na Swalah au hawajali kwa hiyo ni
bora kwao kuepuka kufanya hivyo"
Imesemekana kuwa sababu ya kutakiwa wanawake walio katika hedhi kujitenga
na sehemu ya kuswalia ni tahadhari, kuwa wanawake wasije karibu ya wanaume
bila ya sababu iwapo wao hawaswali, au wasiwaudhi wengine kwa damu au harufu
yake.
Hadiyth hii inamtaka kila mmoja kuhudhuria Swalah ya ‘Iyd, na kushirikiana baina
yao katika wema na ucha Mungu. Wanawake walio katika hedhi wasiachwe nyuma
katika kumtaja Allaah au sehemu njema kama mikusanyiko yenye madhumuni ya
kutafuta elimu na kumtaja Allaah – ukiachia misikitini. Hadiyth hii pia inaonyesha
kuwa wanawake wasitoke nje bila ya jilbaab.
Hadiyth hii inatuambia kuwa sio sawa kwa vijana wa kike na wanawake
wanaotawishwa kutoka nje bila ya sababu inayokubalika. Inasema kuwa
imependekezwa (mustahabb) kwa wanawake kuvaa jilbaab, na kuwa imeruhusiwa
kuazimana nguo. Pia imeonyesha kuwa Swalah ya ‘Iyd ni wajibu.
Ibn Abi Shaybah pia ameeleza kuwa Ibn ‘Umar alikuwa akienda na yeyote
anayeweza kwenda naye katika wanawake wa nyumbani kwake katika Swalah za
‘Iyd.
Hadiyth ya Umm ‘Atwiyah pia inaeleza sababu ya shari'ah hii, ni kuwa ili
wanawake waweze kushuhudia baraka ya ‘Iyd, waone mkusanyiko wa Waislam, na
wapate nao baraka na utukufu wa siku hii.
At-Tirmidhiy (Mwenyeezi Mungu Amrehemu) alisema katina Sunan yake, baada ya
kutaja Hadiyth ya Umm 'Atwiyah, "baadhi ya 'Ulamaa wamechukulia Hadiyth hii na
kuwaruhusu wanawake waende katika Swalah za ‘Iyd na wengineo
hawakupendezewa. Imeripotiwa kuwa 'Abdullah Ibn Al Mubaarak alisema, 'Sipendi
wanawake waende katika Swalah za ‘Iyd siku hizi. Na mwanamke akishikilia
kwenda basi mumewe amwachilie kwenda lakini anapokwenda avae nguo zake
kukuuu kabisa na asijipambe. Na akishikilia kujipamba basi asitoke nje. Na hali hii
mume anayo haki kumzuia kutoka nje. Imeripotiwa kuwa bibi 'Aishah (Radhiya
Allaahu ‘anhu) alisema, "Kama Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
angeliona hali za wanawake walivyo hivi sasa angeliwazuia kwenda misikitini kama
vile wanawake wa Bani Israaiyl walivyozuiliwa" Imeripotiwa kwamba Sufyaan Ath-
Thawriy hakupendezewa wanawake kwenda kuswali Swalah za ‘Iyd. (At-Tirmidhiy
495)
Umm ‘Atwiyah ametoa fatwa yake katika hadiyth iliyotajwa hapo juu, muda baada
ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufariki, na
haikuripotiwa kuwa yeyote miongoni mwa Maswahaba amepingana na fatwa hii.
Maneno ya ‘Aa’ishah (Radhiya Allaahu ‘anha), “Iwapo Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) angeona yanayofanyika kwa wanawake, angewazuilia
kwenda misikitini”, hayapingi hii fatwa (alimradi tu wanawake wanatimiza
masharti ya Kiislamu ya kutoka kwao nje) Ni vizuri zaidi iwapo ruhusa itatolewa
kwa wale wanawake wasiotoka kwa ajili ya kuwaangalia wanaume au kuangaliwa
wao, ambao kuhudhuria kwao hakutopelekea uovu wowote na wasiokwenda
kusongamana na wanaume mitaani au msikitini (yaani wanawake ambao kutoka
kwao hakutosababisha fitna au kishawishi kwake au kwa wanaume).
Wanaume wawakague wanawake wao wanapotoka nje kwa ajili ya Swalah
kuhakikisha kuwa hijabu zao ziko kamili, kwa sababu wao ndio “wachungaji”
wenye jukumu kwa “machunga” wao. Wanawake wanatakiwa watoke wakiwa
katika nguo zisizovutia, wasiwe wamejipamba au kujitia manukato. Wanawake
walio katika hedhi wasiingie msikitini au sehemu ya kuswalia; wanaweza kungojea
ndani ya gari, kwa mfano, ambapo wanaweza kusikia khutbah.
ADAAB ZA 'IYD
Kukoga
Moja ya heshima za ‘Iyd ni kukoga kabla ya kwenda katika Swalah. Imeripotiwa
katika ripoti sahihi katika al-Muwatta’ na kwengineko kuwa ‘Abd-Allaah ibn ‘Umar
alikuwa akikoga siku ya al-Fitwr kabla ya kuja pahala pa kuswalia. (al-
Muwattwa’428)
Imeripotiwa kuwa Sa'iyd ibn Jubayr alisema "Mambo matatu ni Sunnah siku ya
‘Iyd; kwenda kwa miguu katika uwanja wa kuswali (MuSwallaa), kukoga, na kula
kabla ya kutoka nje". Hivi ndivyo alivyosema Sa'iyd ibn Jubayr na labda
amejifunza haya kutoka kwa baadhi ya Maswahaba.
An-Nawawiy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ametaja kuwa wanavyuoni wamekubaliana
kuwa imependekezwa (mustahab) kukoga kabla ya Swalah ya ‘Iyd.
Sababu ya kuwa ni mustahab kukoga kabla ya Swalah ya Ijumaa na mikusanyiko
mengine pia inahusika katika suala la ‘Iyd vilevile.
Kula Kabla Ya Kutoka
Mtu asitoke kwenda pahala pa kuswalia ‘Iyd al-Fitwr kabla ya kula tende, kwa
sababu ya hadiyth iliyosimuliwa na Al-Bukhaariy kutoka kwa Anas ibn Maalik
ambaye amesema:
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki asubuhi ya ‘Iyd
Al Fitwr mpaka ale tende na alikuwa kila kwa hesabu ya witri. (Al-Bukhaariy, 953)
Imependekezwa (mustahab) kula kabla ya kutoka kwa sababu hii inahakikisha
kuwa hatukuruhusiwa kufunga katika siku hiyo, na ni onyesho kuwa Swawm sasa
imemalizika. Ibn Hajar (rahimahu Allaah) ameeleza kuwa hii ni kwa ajili ya
kuwakinga watu kuendeleza Swawm na pia inamaanisha utii kwa Allaah
(Subhaanahu Wa Ta’ala). (Fat-hul-Baariy, 2/446).
Iwapo mtu hatakuwa na tende, anaweza kufutari kwa chochote kilichoruhusiwa.
Kwa upande mwengine, katika ‘Iyd al-Adhw-haa, imependekezwa mtu asile mpaka
baada ya Swalah, ambapo mtu anatakiwa kula nyama ya mnyama mmojawapo
aliyechinjwa (kwa ajili ya siku hii).
Takbira (Allaahu Akbar) Katika Siku Ya 'Iyd
Hii ni moja ya Sunnah kubwa kabisa ya siku hii, kwa sababu ya maneno ya Allaah
(yenye tafsiri):
"......Mwenyezi Mungu Anakutakieni yaliyo mepesi wala Hakutakieni yaliyo mazito,
na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa
Amekuongoeni ili mpate kushukuru" [Al-Baqarah 2:185].
Ad-Daaraqutniy na wengine wameripoti kuwa wakati Ibn ‘Umar alipokuwa akitoka
katika ‘Iyd al-Fitwr na al-Adhw-haa, huwa anajitahidi kutoa Takbiyr mpaka
anapofika pahala pa kuswalia, kisha kuendelea na Takbiyr mpaka aje Imaam.
Tendo la kupiga Takbira kutoka nyumbani hadi pahala pa kuswalia, na mpaka
Imaam aingie, ni maarufu miongoni mwa Salaf (waliotangulia wema) na
limeripotiwa na waandishi wengi kama Ibn Abi Shaybah, ‘Abdur-Razzaaq na al-
Firyaabi katika kitabu chake Ahkaam al-‘‘Iydayn kutoka katika kundi la Salaf. Moja
ya mfano wake ni ripoti kuwa Naafi’ ibn Jubayr alikuwa akitoa Takbira na alikuwa
akishangaa kwa nini watu hawafanyi hivyo. Alikuwa akiwaambia watu, "Kwa nini
hamfanyi Takbira? Ibn Shihaab Az-Zuhri kasema, "Watu walikuwa wakipiga
takbira kuanzia wakati wanapotoka majumbani mwao hadi anapoingia Imaam".
Wakati wa kutoa Takbira katika ‘Iyd al-Fitwr unaanza usiku wa kuamkia ‘Iyd
mpaka wakati Imaam anapofika kuongoza Swalah.
Maneno Ya Takbira
Ibn Abi Shaybah ameripoti katika al-Muswannaf kuwa Ibn Mas’uud (Radhiya
Allaahu ‘anhu) alikuwa akitamka takbira katika siku za Tashriiq kama ifuatavyo:
“Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaah, wa Allaahu Akbar, Allaahu
Akbar wa Lillaahi’l-hamd (Allaah ni Mkubwa kabisa ….hakuna Mungu isipokuwa
Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, na sifa zote njema ni za Allaah)’. Ibn Abi
Shaybah aliripoti haya mahala pengine katika isnaad hiyo hiyo, lakini ikiwa na
pamoja na maneno “Allaahu Akbar” ikirejewa mara tatu.
Al-Muhaamili pia ameripoti kuwa Ibn Mas’uud alikuwa akisema : “Allaahu Akbar
kabiyran, Allaahu Akbar kabiyran, Allaahu Akbar wa ajall, Allaahu Akbar wa
Lillaahi’l-hamd (Allaah ni Mkumbwa kabisa, Allaah ni Mkubwa kabisa, Allaah ni
Mkubwa kabisa, Allaah ni Mkubwa kabisa na Mtukufu, na sifa zote njema ni za
Allaah)”. (al-Irwaa’, 3/126).
Kupongezana
Watu wanaweza kupeana pongezi na Salaam njema za ‘Iyd, bila ya kujali aina ya
maneno. Mfano wanaweza wakaambizana, “Taqabbal Allaah Minnaa Wa Minkum
(Allaah Azikubali [Swawm na ibada] zetu na zenu” au “‘Iyd Mubaarak” na mfano
wa hayo katika Salaam zilizoruhusiwa.
Tendo la kupeana Salaam limekuwa maarufu wakati wa Maswahaaba na
wanavyuoni kama Imaam Ahmad na wengine wameruhusu hilo. Kuna ripoti
zinazoonyesha imeruhusiwa kuwapongeza watu katika matukio maalum.
Maswahaba walikuwa wakipongezana wakati linapotokea jambo zuri, mfano pale
Allaah Alipokubali toba ya mtu n.k.
Hakuna shaka kuwa kumpongeza mtu kwa namna hii ni moja kati ya namna ya
heshima zaidi katika tabia njema na ni moja kati ya muamala mzuri sana wa jamii
ya Waislam.
Kuvaa Vizuri Zaidi Siku Ya 'Iyd
'Abdullaah bin 'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema, 'Umar alichagua jubbah
(nguo refu inayovaliwa juu ya kanzu) ambayo ilitengenezwa kwa hariri na ilikuwa
ikiuzwa kwa bei ya takhfifu sokoni, aliileta kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) na akasema, "ewe Mtume nunua hii na uvae kwa ajili ya ‘Iyd na
watakapokuja wageni" Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
akasema "Hizi ni nguo za yule ambaye hana sehemu akhera (imeripotiwa na Al-
Bukhaariy 948)
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikubaliana na mawazo ya
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) ya mtu kuvaa vizuri zaidi, lakini alikataa na
kupingana na mawazo ya kununua jubbah hilo kwa sababu lilikuwa
limetengenezwa kwa hariri.
Al-Bayhaqiy ameripoti kuwa Ibn ‘Umar alikuwa akivaa nguo zake nzuri siku ya
‘Iyd, kwa hivyo wanaume wanatakiwa wavae nguo nzuri zaidi walizokuwa nazo
wanapotoka kwa ajili ya ‘Iyd.
Kwa upande mwengine, wanawake, wajiepushe na mapambo wanapotoka kwa ajili
ya ‘Iyd, kwa sababu wao wamekatazwa kuonyesha mapambo yao mbele ya
wanaume wasio mahrim (wasio na uhusiano nao wa damu) zao. Mwanamke
anayetaka kutoka ameharamishiwa kujitia manukato au kujionyesha kwa njia ya
kushawishi mbele ya wanaume, kwa sababu yeye ametoka kwa ajili ya ibada tu.
Je, unafikiria kuwa ni sahihi kwa mwanamke muumini kumuasi Yule Ambaye yeye
(mwanamke) anatoka kwenda kumuabudu, na kwenda kinyume na amri Zake kwa
kuvaa nguo za kuvutia zenye kumbana na za rangi zinazong’ara au kujitia
manukano n.k?
Shari'ah Katika Kusikiliza Khutba Za 'Iyd
Ibn Qudaamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema katika kitabu chake cha al-Kaafi
(uk.234):
Imaam anapotoa Salaam (mwisho wa Swalah) atoe khutba sehemu mbili kama
khutbah ya Ijumaa kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alifanya hivyo. Khutba ya ‘Iyd ni tofauti na khutbah ya Ijumaa kwa mambo
manne, jambo la nne ambali ni Sunnah na sio fardhi kusikiliza kwa sababu
imeripotiwa kwamba 'Abdulla bin Al-Saa'ib alisema, "Nilihudhuria ‘Iyd na Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na alipomaliza kuswali, alisema
"tutatoa khutbah sasa kwa hiyo anayependa kukaa (na kusikiliza) akae na yeyote
anayetaka kuondoka basi na aondoke".
Katika al-Sharh al-Mumti’ ‘ala Zaad al-Mustanfi’ cha Ibn ‘Uthaymiin, 5/192,
kinasema:
“Maneno [ya Ibn Qudaamah], ‘kama khutbah mbili za Ijumaa’ inamaanisha kuwa
anatakiwa atoe khutbah mbili, hata kama kuna kutokubaliana katika jambo hili,
kama ambavyo tumetaja hapo juu. Khutbah ya ‘Iyd, imeegemea katika shari'ah
zilizo sawa na za Ijumaa, hata katika nukta ya kuzungumza wakati wa khutbah
hiyo ni haraam, lakini sio wajibu kuhudhuria, hali ya kuwa kuhudhuria khutbah ya
Ijumaa ni wajibu, kwa sababu Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)) Amesema:
"Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swalah siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri
ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara" Al-Jumu'aah :9
Kuhudhuria khutbah ya ‘Iyd sio wajibu, na mtu anaruhusiwa kuondoka, bali iwapo
atabakia, ni lazima asizungumze na yeyote. Hivi ndivyo muandishi alivyokusudia
aliposema ‘kama khutba mbili za Ijumaa’. “
Mmoja wa wanavyuoni amesema: “Si wajibu kusikiliza khutba za ‘Iyd, kwa sababu
kama ingelikuwa ni wajibu kuzihudhuria na kuzisikiliza basi ingekuwa ni haraam
kuondoka. Lakini kwa kuwa imeruhusiwa kuondoka, basi si wajibu kusikiliza”.
Hata hivyo, iwapo mazungumzo yatawakera wale wanaosikiliza, ni haraam
kuzungumza kwa sababu ya kero hizo, sio kwa sababu ya kutokusikiliza. Kwa
msingi huu, iwapo mtu atakuwa na kitabu wakati Imaam anakhutubia, basi
ameruhusiwa kukisoma, kwa sababu kufanya hivyo hakutomkera yeyote.
Mtu Kutoka Kwa Njia Moja Na Kurudi Kwa Kutumia Njia Nyengine
Jaabir bin ‘Abd-Allaah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ameripoti kuwa Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akibadilisha njia siku ya ‘Iyd.
(imeripotiwa na al-Bukhari, 986)
Imeripotiwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa
akitoka kwa miguu, na alikuwa akiswali bila ya adhana wala iqaamah, kisha hurudi
kwa kutumia njia nyengine tofauti. Inasemekana kuwa njia hizi mbili zitamtolea
ushahidi siku ya Qiyaamah, kwa sababu siku hiyo ardhi itasema juu ya kila kitu
kilichofanywa juu yake, zuri na baya. Vile vile inasemekana kuwa imefanywa hivi
ili kuonyesha alama na utamaduni wa Kiislam katika njia zote mbili; kutoa
ukumbusho wa Allaah; kuwavunja moyo wanafiki na Mayahudi na kuwaogopesha
kwa wingi wa watu walio pamoja nae; kutimiza mahitaji wa watu kwa kuwapa
fatwa, kuwasomesha na kuwawekea mifano ya kuifuata; kuwapa sadaka wale
wanaohitajia; au kuwatembelea jamaa zake na kukuza mahusiano yao.
Tahadhari Juu Ya Kufanya Maovu
1.         Baadhi ya watu wanadhani kuwa Uislam unatuambia kukesha na kuswali
usiku wa ‘Iyd, kwa kunakili hadiyth ya uongo inayosema "Yeyote
atakayekesha usiku wa ‘Iyd moyo wake hautokufa siku ya kufa moyo wake"
Hadiyth hii imeripotiwa katika isnaad mbili moja ambayo ni dhaifu na ya pili
ni dhaifu sana. Uislam hautuambii kuutenga usiku wa ‘Iyd kwa kukesha na
kusali; hata hivyo, iwapo mtu ana tabia ya kuamka na kusali usiku
(Qiyaam), hakuna ubaya wa kufanya hivyo katika usiku wa ‘Iyd pia.
2.         Mchanganyiko wa wanawake na wanaume katika maeneo ya Swalah,
mitaani, n.k. Inasikitisha kuwa haya yanatokea sio misikitini tu, bali hata
katika sehemu tukufu zaidi, al-Masjid al-Haram [Makkah]. Wanawake
wengi, Allaah Awaongoze wanatoka wakiwa hawajajisitiri, wamejipamba na
kujitia manukato, wanaonyesha mapambo yao, wakati kuna mkusanyiko
mkubwa katika msikiti huo. Hatari ya hali hii iko wazi kabisa. Kwa hiyo wale
wahusika ni lazima wapange Swalah za ‘Iyd vizuri, kwa kuweka milango
tofauti na njia tofauti kwa wanawake na wawacheleweshe wanaume kutoka
mpaka wanawake wawe wameshatoka.
3.         Baadhi ya watu wanajikusanya siku ya ‘Iyd kwa ajili ya kuimba na kufanya
aina nyengine za ….burudani, na hii haikuruhusiwa.
4.         Baadhi ya watu wanashereheka katika ‘Iyd kwa sababu Ramadhaan
imemalizika na kuwa hawahitajiki tena kufunga. Haya ni makosa, waumini
wanasherehekea ‘Iyd kwa sababu Allaah Amewasaidia wao kumaliza mwezi
wa Swawm, sio kwa sababu ya kumalizika kwa Swawm ambayo watu
wengine wanaichukulia kuwa ni mzigo.
Tunamuomba Allaah Azikubali ibada zetu na toba zetu. Allaah Ampe rehma Mtume
wetu Muhammad.

Thursday, August 9, 2012

falsafa ya mwezi tukufu wa Ramadhan


FALSAFA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI
.
Kwa Kuhusiana na mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, Mimi ninapenda kuwaambieni baadhi ya mambo yaliyo muhimu kwa sababu sisi ni miongoni mwa wale watu waliobahatika kupata fursa hii kwa mara nyingine tena hata bila ya kumuomba Allah Subhanahu wataala.  Kwa mara nyingi, mwanadamu hawezi kukadiria kiasi cha fadhila alizojaaliwa na Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kutokujua umuhimu wake, na vilevile hawezi kushukuru neema hizo wala kufaidika na fursa hizi ambazo amefunguliwa njia zake. Kwa upande mwingine kanuni za fursa nazo ni za aina pekee kama vile ilivyooelezwa katika riwaya mbali mbali kuwa fursa zinakuja kama mawingu na kuondoka vivyohivyo. Fursa hizo hazisubiri wala kumbishia hodi mtu mlangoni mwake mara kwa mara, na hazirejei tena. Wanadamu maishani mwao kwa mara moja au kwa baadhi ya nyakati huwa wanabahatika kupata fursa kama hizo, na kwa hivyo inawabidi wawe wenye kushukuru kwa neema hizo. Na inawabidi kukaribisha neema hizo, na kuzikumbatia na vilevile kushikamana nazo. Kwa hakika kwa lenyewe, maana ya fursa na tawfiq inahitaji pia kuangaliwa. Ama kwa wakati huu, inatubidi sisi tuelewe kwamba mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ni miongoni mwa fursa nyingi kubwa ambazo Allah swt. Ametuzawadia.
Kwa hakika hili siyo jambo dogo kuwa maisha yetu kwa kipindi cha mwaka mzima yamepita na tumeweza kuingia kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu. Chcochote kile ambacho Qur’ani tukufu imezungumzia kuhusu mwezi huu mtukufu  wa Ramadhani kwetu sisi tunaelewa vyema na taswira ambayo Qur’ani tukufu imetuwekea katika akili na fahamu zetu ni kwamba:
“Shahru Ramadhanalladhii anzala fihil Qur’aan Hudalinaasi wabayinatim minal huda walfurqan.”
Mwezi huu Mtukufu ni mwezi uliyoteremshwa Qur’ani Tukufu kama mwongozo wa wanadamu. (Surat Al-Baqarah; 2:185) Hakika katika Mwezi huu mtukufu Qur’ani Tukufu iliteremshwa kama kuwaongoza wanadamu
 Qur’ani Tukufu inazungumzia kuwa mwezi huu ni wa kuteremshwa Qur’ani tukufu.  Na katika riwaya inapatikana kuwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unaitwa Rabiul Qulub, yaani ni mwezi wa machipuo kwa ajili ya mioyo. Vile mchipuo unavyokuja ardhini,  ndivo hivyo hivyo mioyo yetu inavyokuwa katika hali ya mchipuo. Ni Kipindi au msimu  wa mchipuko siyo kwa majina tu ya kubadilika kwa kubadilika usiku na mchana.  Kwa hakika wenyewe tunaona na kushuhudia kuwa katika msimu huo hali ya ardhi inakuwa katika sura  tofauti kabisa na misismu mingine.
Katika hali hii tunaona ghafla kwa kudra za Allah Subhanahu Wataala kuwa ardhi ambayo ilikuwa ni ngumu, kavu, tasa, iliyogeuka kuwa  jangwa, ikawa ya mchanga, ilikuwa ya mawe na ambayo haikuwa na maji, sasa inageuka kuwa ardhi laini ambapo tunaona majani na mimea na maua vinachipua.
Katika mmojawapo ya miujiza ni kwamba hakuna mtu ambaye anatifua au kulima  katika ardhi hiyo lakini zile mbegu zilizokuwa zimefukiwa ambazo zilikuwa zimeshakufa tunaona zinapata uhai na kuchipua. Sisi sote tumeona vile majani na mimea inavyochipua kutoka ardhini na inaota na kutoa maua na kutoa mbegu na baada ya hapo tunaona miche na miti hiyo inakauka na huku mbegu zake zinakuwa zimefukiwa kwenye ardhi. Kwa kipindi chote cha mwaka mzima kwa vipindi mbali mbali vya kiangazi kipupwe n.k. mbegu inakuwa imebakia imejificha ndani ya ardhi na inapofika msimu wa kuchipua inajichipua na ndiyo kumaanisha kuwa mbegu hiyo inakuwa imehifadhika katika hali yake ya  kuwa imekufa ndani mwa ardhi.  Kwa hivyo unapowadia wakati wa kuchipua mbegu hiyo ambayo ilikuwa imekufa kwa kipindi chote hicho inaanaza kuota  na kutoa majani na hivyo tunaona ardhi inakuwa kijani.  Kwa amri za Allah Subhanahu Wataala ardhi inageuka kuwa laini. Na hivyo kuwa na uwezo wa kuipokea kwenye udongo wake ile mbegu iliyopo na kuipa uwezo wa kupitia hatua mbalimbali na hadi kufikia kuwa rangi ya kijani kwa kuipatia uhai. Na kwa amri za Allah inapotoa majani inatokezea nje ya ardhi, na hapo inakuwa katika mmea ambao unatoa maua na vilevile kufikia hatua ya kutoa matunda. Kwa hakika mandhari hii inakuwa ni nzuri sana na ya kuvutia!  Matunda yanavyokuwa matamu tunayaelewa na manukato ya matunda hayo yanavyokuwa mazuri tunayaelewa. Kwa kifupi tumeona kuwadia kwa msimu wa mchipuo wa mbegu iliyokuwa imekufa kutokea ardhi ambayo nayo ilikuwa imekufa, sasa inaanza kuchipua na hapo ndio tunaona muujiza mkubwa wa Allah Subhanahu Wataala ukiwa dhahir na bayana mbele ya mwanadamu.
Imeelezwa katika riwaya mbali mbali kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mchipuo wa mioyo na vile vile mchipuo wa Qur’ani tukufu. Hii inamaanisha kwamba moyo ambao tunaodhania kuwa uko katika vifua vyetu sivyo hivyo, si moyo ule ulionyuma ya mapafu,  bali ni moyo ule ambao ni nafsi zetu. Na ambao kwa hakika ndiyo moyo wa hisia wa mwanadamu. Hata hivyo moyo huu wa nafsi, unapitia katika vipindi mbalimbali. Vipindi  vya machipuo, kiangazi, masika nk. Bila shaka wengi tutakuwa tumeshaona vile ardhi inavyoonekana katika kipindi cha baridi, wakati ambapo hewa baridi ipo na unakuta maji yanakuwa yemeganda na barafu inadondoka. Na katika hali hii vitu laini vinaganda na kuwa vigumu na vivyohivyo ndivyo moyo wa mwanadamu unakuwa hivyo. Kuna baadhi ya nyakati katika maisha ya mwanadamu ambapo moyo wake unakuwa umeganda kama vile barafu inavyoganda. Hivyo katika hali hiyo kumkumbuka Allah Subahanahu Wataala kunakuwa ni kugumu sana kwa moyo kama huo. Ndio maana baadhi ya nyoyo zinakuwa zimekufa kama miche na mimea inavyokufa katika nyakati mbalimbali katika mwaka. Na hivyo moyo kama huo haukubali kuongozwa. Ili kutaka moyo huo uwe katika hali nzuri na ya kuweza kuchipua na kuzaa majani na matunda mazuri basi moyo huo wa mwandamu ambao unasemwa kuwa Kalbul-Mu’min ashurihaman, na hivyo ndiyo maana Allah Subhanahu Wataala ameuweka msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ili nyoyo zetu ziweze kuchipua. Kuja kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani pasi na kufanya yoyote mioyo yetu inakuwa laini.  Tumeona siku moja imepita na hata siku ya leo imetupita na hali ya siku iliyopita yaani jana na hali ya siku tuliyopo leo ni tofauti. Ingawaje jua na mwezi vinachomoza na kuzama kama kawaiada na usiku na mchana inakuwa sawa lakini leo tunakuwa na hisia yenye nguvu na ya aina  pekee.  Leo tunakuwa na mtazamo ulio wa kitayari, matayarisho tofauti kabisa na yale tuliyokuwanayo siku iliyopita. Na tunaona kuwa nyoyo zetu zinakuwa tayari kupokea jambo fulani na vilevile zinatafuta jambo fulani.
Nuzul ya Qur’ani tukufu si jambo la kufikiria au kudhania au kama vile tunavyofikiria sisi kwa kawaida. Iwapo kutakuwa na majaaliwa Inshallah tutalizungumzia swala hili kwa mapana zaidi katika nyakati nyinginezo. Kwa hakika sisi tunavyolifikiria suala hili la Nuzul ni kwa kile tunachokiona, yaani kwa kitu chenyewe na kuteremka kwake kidhahiri, kama vile kitu kilichopo juu ya paa la nyumba yetu kikija chini au tone la mvua linalodondoka kutokea mawinguni, ndio hapo  tunaposema kitu fulani kimeteremka yaani kimekuja chini. Sisi tunachukulia kuteremka kama vile kitu kinatoka juu kuja chini kwa mfano kunapokuwa na ile lift katika jengo inapoteremka kutoka juu kuja chini tunasema hiyo imeteremka. Kwa hakika fikra kama hii haiwezekani kuzungumziwa kwa ajili ya Qur’ani tukufu. Qur’ani haijateremka katika sura kama hii tunavyoielewa, yaani katika sura fulani au ilikuwa katika mbingu ya saba sasa ikaja chini kwani mbingu ni juu na ardhi ni chini ndio maana tukasema inateremka, sivyo hivyo. Kwa hakika sivyo hivyo kabisa, kwa hakika Qur’ani tukufu ni nuru, mwongozo na vile vile ni neno la Allah Subhanahu Wataala. Kamwe haikuwa katika sura ya kitu fulani kabla au baada yake. Kama kuna mahala ambapo ni nafasi ya Qur’ani tukufu,  basi si katika sura ya kitu fulani au katika hali fulani na nafasi yake ni katika nyoyo zetu. Moyo wa  mwanadamu ndio nafasi ya Qur’ani tukufu.
Maana ya kuteremka ni kwamba Qur’ani ilikuwa katika hali ambayo mwongozo huu, hidaya hii ya Mola Wetu ilikuwa katika hali ambayo sisi hatuwezi kuifikia. Na ilikuwa ni  nje ya uwezo wa uelewa wetu. Qur’ani  tukufu ilikuwa katika ‘Lawhi Mahafudh’. Lawhi Mahafudh siyo jina la kitu au chombo fulani kama vile tunavyoona fremu za mbao au fremu zilizotengenezwa kwa mawe. Kamwe hatuwezi kusema ni kitu kinachoshikika. Lawhi Mahafudh ni mahala au hadhi. Katika kuumbwa kwa ulimwengu mzima ni mahala pamoja na Qur’ani nafasi yake ndio hiyo ambapo sisi daraja letu ni la chini kabisa kama vile Qur’ani tukufu inavoelezea “
Asfala Safilini.”  (Sura ya 95: Aya 5)
Sasa wakati Qur’ani tukufu ilipokuwa katika hali iliyoifadhiwa kwa hiyo haikuwa wepesi kwetu sisi kuelewa kwani sisi tukiwa katika daraja la Asfala Safilin. Sasa kile ninachowaambieni mimi kuwa Qur’ani haikuwezekana kueleweka, haimaanishi kuwa Qur’ani tukufu ilikuwa ni jambo moja lililogumu kabisa nje ya uwezo wetu, au Qur’ani ilikuwa na maajabu yasiyoeleweka au kulikuwa na matatizo ndani yake, laa, bali Qur’ani daima imekuwa ndio mwongozo wetu na ndio iliyokuwa ikituongoza katika kila jambo na daima imekuwa ikituita sisi katika kutuongoza na daima imekuwa jambo moja lililo wazi  na lililo bayana na lililokuwa limefunguka vizuri kwa kueleweka kwa ukamilifu. Lakini swala lililopo hapa ni kwamba uwezo wa wale waliotaka kuielewa umekuwa na mipaka yake, nafasi zao zimekuwa ni za chini kabisa, uelewa wao pia ni mdogo sana hivyo hawawezi kuielewa Qur’ani tukufu kwa ukamilifu. Kwa mfano, iwapo kutatolewa mhadhara wa kitaaluma fulani wa hali ya juu kwa mtoto mdogo basi itamaanisha kuwa unazungumzia jambo moja lililo na mafumbo mengi taabu na lisilo wazi kueleweka kwa mtoto huyo. Ingawaje wewe unalolizungumzia liko wazi kabisa bayana lakini kwa upande wa pili msikilizaji wako ni mtoto kwani yeye anao upeo mdogo wa kuelewa. Wewe jambo unalolizungumzia ni la hali ya juu kabisa wakati yule anayekusikiliza anao upeo mdogo sana wa kuelewa. Vile vile baadhi ya nyakati inaelezwa kuwa wakati mtu anapozungumza jambo lenye elimu ya hali ya juu basi miongoni mwa wale wasilikilizaji wanasema kuwa jambo unalolizungumzia ni la hali ya juu sana ambalo liko nje ya uwezo wetu wa kuelewa hivyo tunakuomba kidogo urahisishe lugha yako ili watu waweze kukuelewa vyema.
Ndivyo hivyo hivyo ilivyo maana ya Nuzul, yaana kwamba hadi katika hali ya sasa hivi ipo katika hali ambayo inaweza kueleweka vyema kabisa kwa wale wenye upeo mdogo wa kuelewa. Qur’ani tukufu imejaribu kuelezea kila jambo kiasi kwamba kila mtu anaweza kulielewa vyema na kwa hivyo ndio maana inaelezwa kama nuzul (kuteremka).
Kwa hakika Qur’ani imekuwa katika hali ya upeo mkubwa kabisa wa juu wa kueleweka, kama haingekuwa katika hali liyopo ya sasa hivi basi ingelikuwa ngumu sana kuielewa. Na hii ndio maana ya nuzul ya Qur’ani tukufu, yaani kuwepo katika hali ambayo tunaweza kuielewa vyema au tukawa na uwezo au upeo wa kuielewa hiyo. Na pale Qur’ani inapokuwa katika hali ya kuweza kueleweka, basi kwa ulimi wetu tu hatuwezi kuielewa Qur’ani tukufu, au kwa kuisikiliza tu hatuwezi kuielewa Qur’ani tukukufu. Kwa hakika mahala ambapo Allah Subhanahu Wataala ametujalia sisi kuielewa Qur’ani tukufu ni katika kalb yaani moyo wetu. Lakini katika kalb hii, misimu mingi inapitia na mavuno ya aina nyingi yanapitia humo, na sura mbali mbali. Na baadhi ya nyakati moyo huu unakuwa mgumu kabisa kama vile inavyosema pale, “kal Hijara au ashadu kaswatan” baadhi ya nyakati inakuwa kama jiwe, na hata kuzidi ugumu wa jiwe. Baadhi ya nyakati moyo huu unakuwa, “Bal Alahah Kulubu Atfaluha” yaani ikimaanisha baadhi ya nyakati nyoyo zinakuwa kama zimefungwa kwa kufuli, na baadhi ya nyakati moyo wetu unakuwa na machafu au uchafu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Qur’ani tukufu, ”Rain ala Kulubihim”, yaani baadhi ya tabaka za uchafu zinakuwa zipo juu ya nyoyo zetu. Nyoyo zao zinakuwa zimefungwa kwa mihuri na Allah Subhanahu Wataala ”Khatamalahu Alakulubihim,” Nyoyo zilizopigwa mihuri. Yaani ni kwamba, baadhi ya mioyo ni mawe, na baadhi ya mioyo ni migumu kuliko hata mawe, baadhi ya mioyo inakuwa imefungwa, na baadhi ya mioyo inakuwa imepigwa mihuri kabisa, na baadhi ya mioyo inakuwa imeishaanza kuwa na uchafu, na baadhi ya mioyo inakuwa na tabaka za maovu mbali mbali. Sasa kwa kutaka nyoyo hizi ziwe zimejihusisha na Qur’ani tukufu, ili kuzileta nyoyo hizi karibu na Qur’ani tukufu, Allah Subhanahu Wataala ndio ametujalia neema hii kubwa ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Bila ya sisi kusema, kwa kutambua tu haja zetu, Allah Subhanahu Wataala ametujalia muhula huu. Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuchipua kwa mioyo. Hii inamaanisha kwamba mioyo ambayo ilikwisha kuwa migumu, migumu kuliko hata mawe au mioyo ile ambayo imekwisha fungwa na kupigwa mihuri, basi mioyo yote hiyo katika mwezi  huu mtukufu wa Ramadhani inalainika. Huu ni msimu wa kuchipua na katika kila hali ya ardhi inakuwa laini. Lakini iwapo ardhi hii itawekwa vile ilivyo bila kuzalisha chochote wala kupanda mbegu yoyote au kumwagia maji au kwa kujali basi daima itabakia ardhi iliyokufa kama vile itakavyokuwa imetangulia. Msimu wa kuchipua utakuja na utakwenda lakini ardhi hiyo itabakia ngumu na yenye mawe tupu. Kwa hivyo kuna haja kwetu sisi kuifanya ardhi hii iweze kulainika, inatubidi tuitayarishe tupande mbegu tuimwagilie maji na kupanda kitu chochote katika ardhi hiyo. Ndipo hapo ardhi hiyo itakuwa ina rutuba na yenye kuzaa matunda. Kwa hakika ardhi hii ni ngumu kabisa na kwa  upande mwingine ni msimu wenye maajabu, na msimu wa machipuo, mbegu yoyote utakayoipanda ndani yake itaota yaani itazaa matunda. Na kwa maana hii Allah Subhanahu Wataala ndipo alipouzungumzia mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kama ni mwezi wa nuzul ya Qur’ani tukufu.
Kwa hakika swaum ndio mojawapo ya nguzo muhimu ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Ukuu na hali ya mwezi mtukufu wa Ramadhani si kwa sababu ya kufunga swaumu, bali utukufu na ukuu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwa kutokana na Qur’ani tukufu. Kwa hakika swaum inakuja katika nguzo mojawapo. Ni utaratibu wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwamba tufunge swaum katika mwezi huu.  Na mtu yeyote ambaye hafungi swaum katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani basi mtu huyo hana adabu nzuri. Na vile vile haimaanishi kuwa mtu yeyote anayefunga katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ataweza kubarikiwa baraka zote za Qur’ani tukufu, au kujipatia baraka zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufunga swaum moja tu! Kwa hakika swaum inaifanya mioyo yetu kuwa milaini. Na vile vile swaum inatoharisha nafsi zetu kwa uelewa bora wa Qur’ani tukufu na kuweza kukubaliwa Hidaya kwa urahisi.
 Baadhi ya nyakati sisi tunasikia, na vile vile tunatamka senteso hii kwa ndimi zetu wenyewe, na utakuwa umesikia kwa watu wengi, na unapowauliza je kwa nini haukuja katika darsa za masomo ya Qur’ani, darsa za tafsiir na sherehe ya Qur’ani, masomo ya Qur’ani, je kwa nini hakuna darasa ya kutoa masomo ya Qur’ani? Ukasema hivyo, wao watajibu – kwa sababu sisi tunafunga swaum. Kwa hiyo mtu anapokuwa katika hali ya swaum anakuwa hayuko imara sawasawa, yaani anakuwa hana nguvu, dhaifu, hawezi kusimama katika hali ya kuwa na swaum. Sasa unaona vile madhumuni ya swaum yanavyokuwa yameuliwa hapa. Allah Subhanahu Wataala ameifanya Swaumu ili kuweza kuelewa Qur’ani. Kufunga swaum kwetu sisi imekuwa ni kikwazo cha kuelewa Qur’ani. Je kwa nini wewe hauisomi Qur’ani? Je Kwa nini hutimizi wajibu wa ibada zingine? Je kwa nini? Majibu ya maswali haya yote atakwambia kwamba yuko katika hali ya swaum. Je, Swaum inakuwa kikwazo kwa kupata Hidaya? Allah Subhanahu Wataa  Amefaradhisha swaum ili kwamba katika hali ya swaum sisi tuweze kuelewa vyema zaidi na kuwafanya wengineo waelewe vizuri zaidi. Kwa hakika sisi tunavyochukulia kuwa swaum ni kikwazo katika kuielewa Qur’ani kwa hakika ni kisingizio tu.  Kwa hakika hii ni fursa moja ya hali ya juu kabisa na umuhimu wake ni kupita uwezo wa vile tunavyoweza kufikria au kudhania katika akili zetu.
Fursa hii tumepewa na Allah Subhanahu Wataala bila ya sisi kuiomba Kwake, bali hata bila ya kuitaka kwa kupitia njia za kuomba. Kwa hiyo inatubidi sisi tuitayarishe mioyo yetu iwe laini mbele ya Allah Subhanahu Wataala na tuseme, ”Ewe Allah Subhanahu Watalaa mbegu yoyote Wewe unayoipendelea, panda katika mioyo yetu hii iliyo lainika na mimi ninauwakilisha moyo wangu huu laini ukiwa kama ndiyo ardhi laini kwako Wewe.” Na kwa hakika Allah Subhanahu Wataala atapandikiza mbegu ya hidaya katika sura ya Qur’ani tukufu. Kwa hakika ni muhimu sana kuisoma hivyo, na kupata kuielewa kwake vilevile ni muhimu mno kwetu sisi. Na vilevile ni muhimu kwetu sisi kupitisha wakati wetu wa mchana na usiku pamoja na Qur’ani tukufu. Na ni muhimu kwetu kujihusisha na Qur’ani tukufu na vilevile tuwe Waislamu maharam kwa Qur’ani tukufu, maharam ni wale walio halalika na wala tusiwe na-maharam wasiohalalika katika kutokuielewa Qur’ani.
 Yaani tusiwe watu na-maharam kwa Qur’ani tukufu. bali inatubidi tuwe watu maharam  kwa Qur’ani tukufu. Msemo huu wa maharamiati, (uhalalifu ), ni nzuri na unaoeleweka kwa urahisi. Kwa hakika sisi tumezoea kusikia Maharam na na-maharam kwa wanaume na wanawake tu, lakini maharamiati ina wigo mpana zaidi kuliko huu. Wakati unapokwenda kuhiji (Hajj), na wakati unapokuwa umevaa Ihram basi wewe unakuwa mahrimu, basi wewe unakuwa umeingia katika haram ya Allah Subhanahu wataala, na hapo ndipo unakuwa maharam.  Muhurim (yule anayevaa  Ihramu) anakuwa maharim wa Allah Subhanahu Wataala na hapo ndipo anasema, ”labbayk” (nimekuja nimeitikia wito wako), na wakati anaposikia jambo anasema Labbayk. Hapo huyo anakuwa ameingia katika kuta nne, anakuwa ameingia katika haram, na yeye sasa ni Muhirimiaji na hivyo mahrim, na yeye sasa anakuwa ni balozi wa siri za miongozo ya kiroho ya Allah Subhanahu Wataala hivyo ndivyo inavyotubidi sisi tuwe mahrim kwa Qur’ani tukufu. Sisi tusichukulie Qur’ani tukufu kama na-maharam, na wala tusiwe na mwelekeo kama  na-maharam pamoja na Qur’ani tukufu. Tusiishi na Qur’ani kama wageni nayo.
 Kubali Qur’ani tukufu na jambo hili litakuwa ni bora kabisa kwetu kama iwapo tunapata fursa hiyo. Wewe umejionea mwenyewe, kuwa mimea na miche inayoota katika kipindi cha mchipuo na mavuno yake yanayofuatia na hali ya ukijani unaokuwa juu ya ardhi, unabakia kwa kipindi cha mwaka mzima. Hata katika kipindi cha kiangazi baadhi ya ukijani unakuwa bado ukionekana, baadhi ya matunda pia yakiwepo na hata maua pia yanaonekana. Maua haya si maua ya kipindi cha kiangazi, maua haya yanakuwa yanatokana na kipindi kile cha mchipuo ambapo bado yanakuwa yanahifadhika hadi katika kipindi kile cha kiangazi, na hata yanakuwa yanahifadhika katika kipindi cha  baridi. Na maua ya msimu huo wa mchipuo yanakuwa katika msimu mwingine pia. Wale wanaokuwa wamelala katika kipindi cha mchipuo basi vipindi vya misimu mingine inakuwa ni misimu yao pia. Na wale wanaokuwa macho katika kipindi cha mchipuo, basi msimu huo wa mchipuo unakuwa bado uko katika misimu mingine inayofuatia.
Jambo hili liko katika uwezo wetu, na iwapo tutataka sisi kufanya msimu huo na misimu yote ikawa ni misimu ya mchipuo, basi itabidi tuelewe thamani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ili tuweze kufaidika na baraka zake zote katika misimu yote. Tunamuomba Allah Subhanahu Wataala atujalie fursa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa kutilia maanani thamani na ubora wa kipindi hiki; na Insha’allah kwa uwezo wa Allah Subhanahu Wataala sisi sote tutajitumbukiza katika hidaya ya Qur’ani tukufu.
Wabilahi taaufiki.
 Tamati,
Bil-kheir.


Uteremsho wa Qurani












Adabu za kusoma Qurani