Assalam alaykum dada zangu wa kiislam...........!!!!Amir wenu mstaafu leo nawausia tena kwa mara nyingine tena..........karibuni sana mnifuatilie katika makala hii tena.......natanguliza zangu shukrani......lakini pia ni makala mhimu hata kwa BROTHERS kwa hiyo tushilikiane....
Imetafsiriwa na: Ummu Ummu Ayman
Sifa njema ni za Allaah, Bwana wa
Ulimwengu, na rehma na amani zimshukie
Mtume wetu Muhammad na Aali zake na
Swahaba zake.
“'Iyd” ni neno la kiarabu linalomaanisha
jambo la kitabia au ada, lenye kurudi na
kujirejea. 'Iyd au sikukuu ni alama au
nembo inayopatikana katika kila taifa, ikiwa
ni pamoja na mataifa yale yaliyotajwa
katika vitabu vitukufu na yale ya waabudiao
masanamu, pamoja na wengineo, kwa sababu
kusherehekea sikukuu ni jambo la
kimaumbile katika maumbile ya mwanaadamu.
Watu wote wanapenda kuwa na
matukio maalumu ya kufanya sherehe, ambapo
wanaweza kukukusanyika pamoja
na kuonyesha furaha zao.
Sikukuu za mataifa ya makafiri zinaweza
kufungamanishwa na mambo ya kidunia,
kama kuanza kwa mwaka, kuanza kwa msimu wa
kilimo, kubadilika kwa hali ya
hewa, kuanzishwa kwa dola, kutawazwa kwa
kiongozi, n.k. Zinaweza pia
kufungamanishwa na matukio ya kidini, kama ambavyo nyingi ya sikukuu
zinazowahusu Mayahudi na Wakiristo tu,
mfano Alkhamiys ambayo wanadai kuwa
meza maalum iliteremshwa kwa Yesu,
Krismas, Mwaka Mpya, Siku ya
kushukuriana, na sikukuu ambazo watu
hupeana zawadi. Hizi husherehekewa
katika nchi zote za Ulaya na Amerika ya
Kaskazini hivi sasa, na katika nchi
nyengine ambazo ukristo una nguvu, hata kama nchi yenyewe si ya kikiristo
kiuhalisi. Baadhi ya wanaoitwa Waislam
huweza kujiunga katika sikukuu hizi, kwa
sababu ya ujinga au unafiki.
Wamagiani (Magians) nao pia wana sikukuu
zao, kama Mahrajaan, Namrud n.k.
Ma-baatini (Miongoni mwa Mashia) wana
sikukuu zao pia, kama ‘Iyd al-Ghadiyr,
ambapo wanadai kuwa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amempa ukhalifa ‘Ali (Radhiya Allaahu
‘anhu) na maimamu kumi na moja baada
yake.
Waislamu Wanatambulika Kwa Sikukuu Zao
Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) "Kila Umma una
sikukuu yake na hii ni sikukuu yenu"
yanaonyesha kuwa ‘Iyd hizi mbili ni maalumu
kwa Waislamu tu, na kuwa hairuhusiwi kwa
Muislam kuwaiga makafiri na
washirikina katika jambo lolote ambalo ni
maalumu ndani ya sherehe zao, iwapo
kama ni chakula, nguo, kuwasha moto au matendo
ya ibada.
Watoto wa Kiislam wasiruhusiwe kucheza
katika sikukuu hizo za kikafiri, au
kujipamba, au kujumuika na makafiri katika
matukio hayo. Sikukuu zote za kikafiri
au zilizozushwa ni haraam, mfano kama sherehe za Siku ya Uhuru, maadhimisho
ya mapinduzi, miti ya sherehe za sikukuu
au kutawazwa kwa kiongozi, siku za
kuzaliwa, Sikukuu ya Wafanyakazi, Sikukuu
ya Nile, Shamm an-Nasiym (sikukuu
ya majira ya baridi ya Wamisri), siku ya
walimu, na Maulidi ya Mtume (Kuzaliwa
kwa Mtume).
Waislam hawana sikukuu ukiacha ile ya ‘Iyd
al-Fitwr na ‘Iyd al-Adhw-haa, kwa
sababu ya hadiyth iliyotolewa na Anas
(Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
"Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja Madiynah
na watu walikuwa na siku mbili wakicheza
na kufurahi. Akauliza, "Ni siku gani hizi
mbili?" Wakasema, "Tulikuwa
tukicheza na kufurahi katika siku hizi zama za
ujaahiliyya" (zama za ujinga kabla ya
Uislamu). Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) akasema, "Allaah
Amekupeni siku bora kuliko hizo, nazo ni siku
ya ‘Iyd Al-Adhw-haa na siku ya ‘Iyd Al
Fitwr". (Sunan Abi Daawuud 1134)
Yafuatayo ni maelezo kuhusu shari'ah na
adabu za ‘Iyd mbili kwa mujibu wa
Sharia ya Kiislam:
Ahkaamul-'Iyd (Shari'ah Katika 'Iyd)
Kufunga
Ni haraam kufunga katika siku za ‘Iyd
kutokana na hadiyth ya Abu Sa’iyd al-
Khudriy (Radhiya Allaahu ‘anhu), amesema
kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) amekataza kufunga
katika siku ya Fitwr na katika siku ya
Kuchinja (Adhw-haa). (Imeripotiwa na
Muslim, 827)
Shari'ah Katika Swalah Za 'Iyd
Baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa Swalah
ya ‘Iyd ni waajib, huu ni mtizamo
wa wanavyuoni wa Kihanafi na Shaykh
al-Islam Ibn Taymiyah (rahimahu Allaah).
Wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa
akiswali Swalah zote za ‘Iyd na hakuacha
kufanya hivyo hata mara moja.
Wamechukua ushahidi katika ayah (yenye
tafsiri),
"Basi swali na uchinje kwa ajili ya
Mola wako Mlezi" Al-Kawthar: 2
Yaani Swalah ya ‘Iyd na kuchinja baada
yake, ambayo ni amri, na kwa ukweli
kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) aliwaamrisha wanawake
watolewe kuhudhuria Swalah ya ‘Iyd, na
kwamba mwanamke aliyekuwa hana
jilbaab aazime kutoka kwa ndugu yake
Baadhi ya wanavyuoni wanasema kuwa Swalah
ya ‘Iyd ni Fardhu Kifaayah (fardhi
yenye kutosheleza). Huu ni mtizamo wa
Kihanbali. Kundi la tatu linasema kuwa
Swalah ya ‘Iyd ni Sunnah iliyokokotezwa.
Huu ni mtizamo wa Kimaalik na Kishaafi.
Wanachukua ushahidi ya hadiyth ya Bedui
inayosema kuwa Allaah (Subhaanahu
Wa Ta’ala) Hakufaradhisha Swalah yoyote
kwa waja Wake zaidi ya zile Swalah
tano. Kwa hiyo Waislam wafanye hima
kuhudhuria Swalah ya ‘Iyd, hususan kwa
kuwa maoni ya kuwa ni waajib yameegemea
katika ushahidi wenye nguvu.
Neema, baraka na malipo makubwa
yanapatikana kwa kuhudhuria Swalah za ‘Iyd,
na kwa ukweli kuwa mtu atakuwa anafuata
mwendo wa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kufanya
hivyo, basi inatosha kuwa ni
changamoto.
Mambo Ya Lazima Na Wakati Wa
Swalah Ya 'Iyd
Baadhi ya wanavyuoni wa Kihanbali wanasema
kuwa sharti za Swalah ya ‘Iyd ni
iqaamah lazima isomwe na ni lazima
iswaliwe kwa jamaa. Baadhi yao
wamesema
kuwa sharti za Swalah ya ‘Iyd ni sawa na
zile za Swalah ya Ijumaa, isipokuwa
katika khutba, ambapo kuihudhuria si
lazima. Wengi miongoni mwa wanavyuoni
wanasema wakati wa Swalah ya ‘Iyd unaanza
pale jua linapochomoza kwa masafa
ya urefu wa mshale, kwa linavyoonekana kwa
macho matupu, na unaendelea
mpaka jua linapokaribia kuwa sawa sawa.
Maelezo Ya Swalah Ya 'Iyd
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “
Swalah ya ‘Iyd Fitwr na al-Adhw-haa
ni rakaa mbili zilizotimia, sio fupi fupi.
Hii ni kwa mujibu wa maneno ya Mtume, na
muongo ni mwenye kulaaniwa.”
Abu Sa’iyd amesema: “Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam)
amekuwa akija katika pahala pa kuswalia
katika siku za Fitwr na al-Adhw-haa, na
jambo la mwanzo analofanya ni kuswali”.
Takbira inarejewa mara saba katika rakaa
ya mwanzo na mara tano katika rakaa
ya pili, Qur-aan inasomwa baada yake
katika kila rakaa.
Imeripotiwa kutoka kwa A’ishah: Takbira ya
al-Fitwr na al-Adhw-haa ni mara saba
katika rakaa ya mwanzo na mara tano katika
rakaa ya pili, mbali na Takbira ya
rukuu. (imeripotiwa na Abu Daawuud;
imesahihishwa na jumla ya isnaad)
Iwapo mtu amejiunga na Swalah amemuwahi
Imaam wakati wa Takbira hizi za
ziada, ni juu yake kusema “Allaahu Akbar”
pamoja na Imaam, na halazimiki
kuzilipa Takbira ambazo zimempita, kwa
sababu (takbira hizo) ni Sunnah, sio
waajib. Kuhusu nini kinatakiwa kisemwe
baina ya Takbira, Hammaad ibn Salamah
ameripoti kutoka kwa Ibraahiym kuwa
"Waliyd ibn ‘Uqbah aliingia msikitini wakati
Ibn Mas’uud, Hudhayfah na Abu Muusa wapo
hapo, na akasema, “‘Iyd ipo hapa,
nini natakiwa kufanya?” Ibn Mas’uud
akasema: “Sema ‘Allaahu Akbar’, msifu na
mshukuru Allaah, msalie Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na
omba du’aa, kisha sema ‘Allaahu Akbar’,
msifu na mshukuru Allaah, mswalie
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam)….n.k.’ (Imeripotiwa na at-
Twabaraaniy. Ni hadiyth sahihi
iliyonukuliwa katika al-Irwaa’ na kwengineko).
Kusoma Qur-aan Katika Swalah Za 'Iyd
Imependekezwa (mustahabb) kuwa katika
Swalah za ‘Iyd, imaam asome surat
Qaaf (sura ya 50) na surat
al-Qamar (sura ya 54), kama ilivyoripotiwa
katika
Swahiyh Muslim kuwa ‘Umar ibn Al-Khattwaab
alimuuliza Abu Waaqid al-Laythi,
“Nini Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa
akisoma katika [‘Iyd] al-Adhw-haa na
al-Fitwr?” Akasema, “Alikuwa akisoma Qaaf,
Wal-Qur-aan al-Majiyd [Qaaf 50:1] na
Iqtarabat as-saa’ah wa’nshaqq al-qamar
[al-Qamar 54:1].
Ripoti nyingi zinaonyesha kuwa Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alikuwa akisoma Surat al A’laa [87] na
Suurat al-Ghaashiyah {88], kama ambavyo
alivyokuwa akizisoma katika Swalah ya
Ijumaa. An-Nu’maan ibn Bashiyr
amesema:
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika '‘Iyd
mbili na siku ya Ijumaa Sabbih Isma
Rabbikal-a'laa (Al-A'alaa 87:1) na Hal Ataaka
Hadiythul-Ghaashiyah (Al-Ghaashiyah
88:1)" Swahiyh Muslim 878
Samurah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika
‘Iyd mbili Sabbih Isma Rabbikal-a'alaa
(Al-a'alaa 87:1) na Hal Ataaka
Hadiythul-Ghaashiyah (Al-Ghaashiyah 88:1)
Imesimuliwa na Ahmad na wengine ni Swahiyh
[ Al-Irwaa 3/116]
Swalah Inaswaliwa Kabla Ya Khutbah
Moja ya shari'ah za ‘Iyd ni kuwa Swalah ni
lazima iwe kabla ya khutbah, kama
ilivyoripotiwa katika Musnad Ahmad kutoka
katika hadiyth ya Ibn ‘Abbaas, ambaye
ameshuhudia kwamba Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali
kabla ya khutba siku ya ‘Iyd kisha akatoa
khutba (Musnad Ahmad 1905. Hadiyth
hii pia iko katika Swahiyh mbili)
Yeyote Anayetaka Kuondoka Wakati Wa
Khutbah Ameruhusiwa Kufanya
Hivyo
‘Abd-Allaah ibn al-Saab amesema:
"Nilihudhuria '‘Iyd pamoja na Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na
alipomaliza alisema, tutatoa khutba, kwa
hiyo anayetaka kukaa (na kusikiliza)
khutba basi akae na anayetaka kuondoka
basi aondoke (Irwaa al Ghaliyl 3/96)
Swalah Isicheleweshwe Kwa Muda Mrefu
‘Abd-Allaah ibn Bishr, swahaba wa Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam), alitoka pamoja na watu siku ya
al-Fitwr au al-Adhw-haa, na akaonyesha
kutopendezwa kwa kuwa Imaam alikuja akiwa
amechelewa sana.
Akasema:
"Wakati wa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) tungelikuwa
tumeshamaliza wakati wa sasa" na huo
ulikuwa wakati wa Tasbiyh” (Imesimuliwa
na na Al-Bukhaariy).
Swalah Za Sunnah, Pahala Pa
Swalah (Ya 'Iyd)
Hakuna Swalah za Sunnah ambazo zinaswaliwa
kabla au baada ya Swalah ya ‘Iyd,
kama alivyoripoti Ibn ‘Abbaas kuwa "Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) alikuwa akitoka katika siku ya
‘Iyd na akaswali rakaa mbili, bila ya
chochote (Swalah yoyote) kabla au baada
yake". Hali hii ni iwapo Swalah
itaswaliwa pahala pa kuswaliwa au sehemu
ya wazi. Hata hivyo, iwapo watu
wataswali ‘Iyd msikitini, basi watatakiwa
waswali rakaa mbili za Tahiyat al-Masjid
(Swalah ya kiamkizi cha msikiti) kabla
hawajakaa kitako.
Iwapo Watu Hawatokuwa Na Habari Ya 'Iyd
Mpaka Siku Ya Pili
Abu ‘Umayr ibn Anas ameripoti kutoka kwa
‘ami yake miongoni mwa Answaar
kuwa alisema: "Kulikuwa na mawingu na
hatukuweza kuuona mwezi wa
Shawwaal, kwa hiyo tukaanza siku kwa
kufunga, kisha ukaja msafara mwisho wa
siku na wakamwabia Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa
wameona mwezi wa Shawwaal siku moja kabla,
akawaambia watu waache
kufunga na wakaenda kuswali ‘Iyd siku ya
pili" Imeripotiwa na Maimaam watano,
ni Sahiyh; Al-Irwaa' 3/102
Iwapo mtu amekosa Swalah ya ‘Iyd, mtazamo
ulio sahihi kuliko yote ni kuwa
anaweza kuilipa kwa kuswali rakaa mbili.
Kuhudhuria Kwa Wanawake Katika Swalah Za
'Iyd
Hafswah (Radhiya Allaahu ‘anha) amesema:
"Tulikuwa tukiwazuia wasichana
wenye hedhi kuhudhuria Swalah za ‘Iyd.
Kisha akaja mwanamke kukaa katika
ngome ya Banu Khalaf na akatuambia kuhusu
dada yake. Mume wa dada yake
alihudhuria vita kumi na mbili pamoja na
Mtume (na akasema) , Dada yangu
alikuwa naye katika vita sita. Akasema
tulikuwa tukiwatendea walioumia na
tukiwashughulikia wagonjwa. Dada yangu
alimuuliza Mtume kama kuna ubaya
wowote kutokwenda kuswali ‘Iyd ikiwa hana
jilbaab. Akasema "mwache rafiki yake
ampe moja wa jilbaab lake ili
aweze kushuhudia baraka za ‘Iyd na aone kujumuika
kwa Waislamu" Ummu 'Atwiyah alipokuja
nilimuuliza umemiskia Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
akisema hivyo?" Akasema "Baba yangu
achinjwe kwa ajili yake" Na alikuwa
hamtaji ila baada ya kusema "baba yangu
achinjwe kwa ajili yake".
"Nimemsikia akisema kuwa wasichana na wale
wanaotawishwa au wasichana waliotawishwa
na wanawake wenye hedhi ili
washuhudie baraka za ‘Iyd na kujumuika kwa
waumini. Lakini wale wenye hedhi
wakae mbali na sehemu ya kuswali"
(Swahiyh Al-Bukhaariy)
Vijana wa kike (‘awaatik, mmoja ‘aatiq) ni
wale waliokwisha vunja ungo au wako
karibu na kufanya hivyo, au wamefikia umri
wa kuolewa, au walio na thamani
katika familia zao, au wasiofanyishwa kazi
zisizo na heshima. Inaonekana kuwa
wamekuwa wakizuiwa vijana hawa kutoka nje
kwa sababu ya uovu uliojitokeza
baada ya kizazi cha kwanza cha Uislam;
lakini Swahaabah hawakukubaliana na
hilo na wakaona kuwa shari'ah ya wakati wao
lazima ibaki kama ilivyokuwa wakati
wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam).
“Jilbaab lake”- ametakiwa kuazima baadhi
ya nguo ambazo hakuwa akizihitajia.
“Wanaotengwa/Wanaotawishwa”- ambao
wanaowekewa paazia kipembeni mwa
nyumba ambamo wari hukaa nyuma yake.
“Wanawake walio katika hedhi”- huyyadh,
mmoja haaidh– hii inaweza kurejea kwa
vijana wa kike waliofikia umri wa kukua,
au wanawake waliomo katika siku zao na
wasio tohara.
“Wanawake walio katika hedhi wanatakiwa
wajitenge na Swalah – pahala
penyewe” – Ibn al-Munayyir amesema:
"Sababu ya kujitenga na sehemu ya
kuswali ni kuwa wakisimama pamoja na
wanawake wanaoswali japokuwa
hawaswali, itaonekana kuwa hawana heshima
na Swalah au hawajali kwa hiyo ni
bora kwao kuepuka kufanya hivyo"
Imesemekana kuwa sababu ya kutakiwa
wanawake walio katika hedhi kujitenga
na sehemu ya kuswalia ni tahadhari, kuwa
wanawake wasije karibu ya wanaume
bila ya sababu iwapo wao hawaswali, au
wasiwaudhi wengine kwa damu au harufu
yake.
Hadiyth hii inamtaka kila mmoja kuhudhuria
Swalah ya ‘Iyd, na kushirikiana baina
yao katika wema na ucha Mungu. Wanawake walio
katika hedhi wasiachwe nyuma
katika kumtaja Allaah au sehemu njema kama mikusanyiko yenye madhumuni ya
kutafuta elimu na kumtaja Allaah –
ukiachia misikitini. Hadiyth hii pia inaonyesha
kuwa wanawake wasitoke nje bila ya
jilbaab.
Hadiyth hii inatuambia kuwa sio sawa kwa
vijana wa kike na wanawake
wanaotawishwa kutoka nje bila ya sababu
inayokubalika. Inasema kuwa
imependekezwa (mustahabb) kwa wanawake
kuvaa jilbaab, na kuwa imeruhusiwa
kuazimana nguo. Pia imeonyesha kuwa Swalah
ya ‘Iyd ni wajibu.
Ibn Abi Shaybah pia ameeleza kuwa Ibn
‘Umar alikuwa akienda na yeyote
anayeweza kwenda naye katika wanawake wa
nyumbani kwake katika Swalah za
‘Iyd.
Hadiyth ya Umm ‘Atwiyah pia inaeleza sababu
ya shari'ah hii, ni kuwa ili
wanawake waweze kushuhudia baraka ya ‘Iyd,
waone mkusanyiko wa Waislam, na
wapate nao baraka na utukufu wa siku hii.
At-Tirmidhiy (Mwenyeezi Mungu Amrehemu)
alisema katina Sunan yake, baada ya
kutaja Hadiyth ya Umm 'Atwiyah,
"baadhi ya 'Ulamaa wamechukulia Hadiyth hii na
kuwaruhusu wanawake waende katika Swalah
za ‘Iyd na wengineo
hawakupendezewa. Imeripotiwa kuwa
'Abdullah Ibn Al Mubaarak alisema, 'Sipendi
wanawake waende katika Swalah za ‘Iyd siku
hizi. Na mwanamke akishikilia
kwenda basi mumewe amwachilie kwenda
lakini anapokwenda avae nguo zake
kukuuu kabisa na asijipambe. Na
akishikilia kujipamba basi asitoke nje. Na hali hii
mume anayo haki kumzuia kutoka nje.
Imeripotiwa kuwa bibi 'Aishah (Radhiya
Allaahu ‘anhu) alisema, "Kama Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
angeliona hali za wanawake walivyo hivi
sasa angeliwazuia kwenda misikitini kama
vile wanawake wa Bani Israaiyl
walivyozuiliwa" Imeripotiwa kwamba Sufyaan Ath-
Thawriy hakupendezewa wanawake kwenda
kuswali Swalah za ‘Iyd. (At-Tirmidhiy
495)
Umm ‘Atwiyah ametoa fatwa yake katika
hadiyth iliyotajwa hapo juu, muda baada
ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) kufariki, na
haikuripotiwa kuwa yeyote miongoni mwa
Maswahaba amepingana na fatwa hii.
Maneno ya ‘Aa’ishah (Radhiya Allaahu
‘anha), “Iwapo Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) angeona
yanayofanyika kwa wanawake, angewazuilia
kwenda misikitini”, hayapingi hii fatwa
(alimradi tu wanawake wanatimiza
masharti ya Kiislamu ya kutoka kwao nje)
Ni vizuri zaidi iwapo ruhusa itatolewa
kwa wale wanawake wasiotoka kwa ajili ya
kuwaangalia wanaume au kuangaliwa
wao, ambao kuhudhuria kwao hakutopelekea
uovu wowote na wasiokwenda
kusongamana na wanaume mitaani au
msikitini (yaani wanawake ambao kutoka
kwao hakutosababisha fitna au kishawishi
kwake au kwa wanaume).
Wanaume wawakague wanawake wao wanapotoka
nje kwa ajili ya Swalah
kuhakikisha kuwa hijabu zao ziko kamili,
kwa sababu wao ndio “wachungaji”
wenye jukumu kwa “machunga” wao. Wanawake
wanatakiwa watoke wakiwa
katika nguo zisizovutia, wasiwe
wamejipamba au kujitia manukato. Wanawake
walio katika hedhi wasiingie msikitini au
sehemu ya kuswalia; wanaweza kungojea
ndani ya gari, kwa mfano, ambapo wanaweza
kusikia khutbah.
ADAAB ZA 'IYD
Kukoga
Moja ya heshima za ‘Iyd ni kukoga kabla ya
kwenda katika Swalah. Imeripotiwa
katika ripoti sahihi katika al-Muwatta’ na
kwengineko kuwa ‘Abd-Allaah ibn ‘Umar
alikuwa akikoga siku ya al-Fitwr kabla ya
kuja pahala pa kuswalia. (al-
Muwattwa’428)
Imeripotiwa kuwa Sa'iyd ibn Jubayr alisema
"Mambo matatu ni Sunnah siku ya
‘Iyd; kwenda kwa miguu katika uwanja wa
kuswali (MuSwallaa), kukoga, na kula
kabla ya kutoka nje". Hivi ndivyo
alivyosema Sa'iyd ibn Jubayr na labda
amejifunza haya kutoka kwa baadhi ya
Maswahaba.
An-Nawawiy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ametaja
kuwa wanavyuoni wamekubaliana
kuwa imependekezwa (mustahab) kukoga kabla
ya Swalah ya ‘Iyd.
Sababu ya kuwa ni mustahab kukoga kabla ya
Swalah ya Ijumaa na mikusanyiko
mengine pia inahusika katika suala la ‘Iyd
vilevile.
Kula Kabla Ya Kutoka
Mtu asitoke kwenda pahala pa kuswalia ‘Iyd
al-Fitwr kabla ya kula tende, kwa
sababu ya hadiyth iliyosimuliwa na
Al-Bukhaariy kutoka kwa Anas ibn Maalik
ambaye amesema:
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) alikuwa hatoki asubuhi ya ‘Iyd
Al Fitwr mpaka ale tende na alikuwa kila
kwa hesabu ya witri. (Al-Bukhaariy, 953)
Imependekezwa (mustahab) kula kabla ya
kutoka kwa sababu hii inahakikisha
kuwa hatukuruhusiwa kufunga katika siku
hiyo, na ni onyesho kuwa Swawm sasa
imemalizika. Ibn Hajar (rahimahu Allaah)
ameeleza kuwa hii ni kwa ajili ya
kuwakinga watu kuendeleza Swawm na pia
inamaanisha utii kwa Allaah
(Subhaanahu
Wa Ta’ala). (Fat-hul-Baariy,
2/446).
Iwapo mtu hatakuwa na tende, anaweza
kufutari kwa chochote kilichoruhusiwa.
Kwa upande mwengine, katika ‘Iyd
al-Adhw-haa, imependekezwa mtu asile mpaka
baada ya Swalah, ambapo mtu anatakiwa kula
nyama ya mnyama mmojawapo
aliyechinjwa (kwa ajili ya siku hii).
Takbira (Allaahu Akbar) Katika Siku Ya
'Iyd
Hii ni moja ya Sunnah kubwa kabisa ya siku
hii, kwa sababu ya maneno ya Allaah
(yenye tafsiri):
"......Mwenyezi Mungu Anakutakieni
yaliyo mepesi wala Hakutakieni yaliyo mazito,
na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze
Mwenyezi Mungu kwa kuwa
Amekuongoeni ili mpate kushukuru"
[Al-Baqarah 2:185].
Ad-Daaraqutniy na wengine wameripoti kuwa
wakati Ibn ‘Umar alipokuwa akitoka
katika ‘Iyd al-Fitwr na al-Adhw-haa, huwa
anajitahidi kutoa Takbiyr mpaka
anapofika pahala pa kuswalia, kisha
kuendelea na Takbiyr mpaka aje Imaam.
Tendo la kupiga Takbira kutoka nyumbani
hadi pahala pa kuswalia, na mpaka
Imaam aingie, ni maarufu miongoni mwa
Salaf (waliotangulia wema) na
limeripotiwa na waandishi wengi kama Ibn Abi Shaybah, ‘Abdur-Razzaaq na al-
Firyaabi katika kitabu chake Ahkaam
al-‘‘Iydayn kutoka katika kundi la Salaf. Moja
ya mfano wake ni ripoti kuwa Naafi’ ibn
Jubayr alikuwa akitoa Takbira na alikuwa
akishangaa kwa nini watu hawafanyi hivyo.
Alikuwa akiwaambia watu, "Kwa nini
hamfanyi Takbira? Ibn Shihaab Az-Zuhri
kasema, "Watu walikuwa wakipiga
takbira kuanzia wakati wanapotoka
majumbani mwao hadi anapoingia Imaam".
Wakati wa kutoa Takbira katika ‘Iyd
al-Fitwr unaanza usiku wa kuamkia ‘Iyd
mpaka wakati Imaam anapofika kuongoza
Swalah.
Maneno Ya Takbira
Ibn Abi Shaybah ameripoti katika
al-Muswannaf kuwa Ibn Mas’uud (Radhiya
Allaahu ‘anhu) alikuwa akitamka takbira
katika siku za Tashriiq kama ifuatavyo:
“Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa ilaaha
illa-Allaah, wa Allaahu Akbar, Allaahu
Akbar wa Lillaahi’l-hamd (Allaah ni Mkubwa
kabisa ….hakuna Mungu isipokuwa
Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, na sifa
zote njema ni za Allaah)’. Ibn Abi
Shaybah aliripoti haya mahala pengine
katika isnaad hiyo hiyo, lakini ikiwa na
pamoja na maneno “Allaahu Akbar” ikirejewa
mara tatu.
Al-Muhaamili pia ameripoti kuwa Ibn
Mas’uud alikuwa akisema : “Allaahu Akbar
kabiyran, Allaahu Akbar kabiyran, Allaahu
Akbar wa ajall, Allaahu Akbar wa
Lillaahi’l-hamd (Allaah ni Mkumbwa kabisa,
Allaah ni Mkubwa kabisa, Allaah ni
Mkubwa kabisa, Allaah ni Mkubwa kabisa na
Mtukufu, na sifa zote njema ni za
Allaah)”. (al-Irwaa’, 3/126).
Kupongezana
Watu wanaweza kupeana pongezi na Salaam
njema za ‘Iyd, bila ya kujali aina ya
maneno. Mfano wanaweza wakaambizana,
“Taqabbal Allaah Minnaa Wa Minkum
(Allaah Azikubali [Swawm na ibada] zetu na
zenu” au “‘Iyd Mubaarak” na mfano
wa hayo katika Salaam zilizoruhusiwa.
Tendo la kupeana Salaam limekuwa maarufu
wakati wa Maswahaaba na
wanavyuoni kama Imaam Ahmad na wengine
wameruhusu hilo.
Kuna ripoti
zinazoonyesha imeruhusiwa kuwapongeza watu
katika matukio maalum.
Maswahaba walikuwa wakipongezana wakati
linapotokea jambo zuri, mfano pale
Allaah Alipokubali toba ya mtu n.k.
Hakuna shaka kuwa kumpongeza mtu kwa namna
hii ni moja kati ya namna ya
heshima zaidi katika tabia njema na ni
moja kati ya muamala mzuri sana
wa jamii
ya Waislam.
Kuvaa Vizuri Zaidi Siku Ya 'Iyd
'Abdullaah bin 'Umar (Radhiya Allaahu
‘anhu) amesema, 'Umar alichagua jubbah
(nguo refu inayovaliwa juu ya kanzu)
ambayo ilitengenezwa kwa hariri na ilikuwa
ikiuzwa kwa bei ya takhfifu sokoni,
aliileta kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) na akasema, "ewe
Mtume nunua hii na uvae kwa ajili ya ‘Iyd na
watakapokuja wageni" Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
akasema "Hizi ni nguo za yule ambaye
hana sehemu akhera (imeripotiwa na Al-
Bukhaariy 948)
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) alikubaliana na mawazo ya
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) ya mtu kuvaa
vizuri zaidi, lakini alikataa na
kupingana na mawazo ya kununua jubbah hilo kwa sababu lilikuwa
limetengenezwa kwa hariri.
Al-Bayhaqiy ameripoti kuwa Ibn ‘Umar
alikuwa akivaa nguo zake nzuri siku ya
‘Iyd, kwa hivyo wanaume wanatakiwa wavae
nguo nzuri zaidi walizokuwa nazo
wanapotoka kwa ajili ya ‘Iyd.
Kwa upande mwengine, wanawake, wajiepushe
na mapambo wanapotoka kwa ajili
ya ‘Iyd, kwa sababu wao wamekatazwa
kuonyesha mapambo yao
mbele ya
wanaume wasio mahrim (wasio na uhusiano
nao wa damu) zao. Mwanamke
anayetaka kutoka ameharamishiwa kujitia
manukato au kujionyesha kwa njia ya
kushawishi mbele ya wanaume, kwa sababu
yeye ametoka kwa ajili ya ibada tu.
Je, unafikiria kuwa ni sahihi kwa mwanamke
muumini kumuasi Yule Ambaye yeye
(mwanamke) anatoka kwenda kumuabudu, na
kwenda kinyume na amri Zake kwa
kuvaa nguo za kuvutia zenye kumbana na za
rangi zinazong’ara au kujitia
manukano n.k?
Shari'ah Katika Kusikiliza Khutba Za 'Iyd
Ibn Qudaamah (Radhiya Allaahu ‘anhu)
amesema katika kitabu chake cha al-Kaafi
(uk.234):
Imaam anapotoa Salaam (mwisho wa Swalah)
atoe khutba sehemu mbili kama
khutbah ya Ijumaa kwa sababu Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alifanya hivyo. Khutba ya ‘Iyd ni tofauti
na khutbah ya Ijumaa kwa mambo
manne, jambo la nne ambali ni Sunnah na
sio fardhi kusikiliza kwa sababu
imeripotiwa kwamba 'Abdulla bin Al-Saa'ib
alisema, "Nilihudhuria ‘Iyd na Mtume
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) na alipomaliza kuswali, alisema
"tutatoa khutbah sasa kwa hiyo
anayependa kukaa (na kusikiliza) akae na yeyote
anayetaka kuondoka basi na aondoke".
Katika al-Sharh al-Mumti’ ‘ala Zaad
al-Mustanfi’ cha Ibn ‘Uthaymiin, 5/192,
kinasema:
“Maneno [ya Ibn Qudaamah], ‘kama khutbah mbili za Ijumaa’ inamaanisha kuwa
anatakiwa atoe khutbah mbili, hata kama kuna kutokubaliana katika jambo hili,
kama ambavyo tumetaja hapo juu. Khutbah ya
‘Iyd, imeegemea katika shari'ah
zilizo sawa na za Ijumaa, hata katika
nukta ya kuzungumza wakati wa khutbah
hiyo ni haraam, lakini sio wajibu
kuhudhuria, hali ya kuwa kuhudhuria khutbah ya
Ijumaa ni wajibu, kwa sababu Allaah (Subhaanahu
Wa Ta’ala)) Amesema:
"Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swalah
siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri
ya Mwenyezi Mungu, na wacheni
biashara" Al-Jumu'aah :9
Kuhudhuria khutbah ya ‘Iyd sio wajibu, na
mtu anaruhusiwa kuondoka, bali iwapo
atabakia, ni lazima asizungumze na yeyote.
Hivi ndivyo muandishi alivyokusudia
aliposema ‘kama
khutba mbili za Ijumaa’. “
Mmoja wa wanavyuoni amesema: “Si wajibu
kusikiliza khutba za ‘Iyd, kwa sababu
kama ingelikuwa ni wajibu kuzihudhuria na
kuzisikiliza basi ingekuwa ni haraam
kuondoka. Lakini kwa kuwa imeruhusiwa
kuondoka, basi si wajibu kusikiliza”.
Hata hivyo, iwapo mazungumzo yatawakera
wale wanaosikiliza, ni haraam
kuzungumza kwa sababu ya kero hizo, sio
kwa sababu ya kutokusikiliza. Kwa
msingi huu, iwapo mtu atakuwa na kitabu
wakati Imaam anakhutubia, basi
ameruhusiwa kukisoma, kwa sababu kufanya
hivyo hakutomkera yeyote.
Mtu Kutoka Kwa Njia Moja Na Kurudi Kwa
Kutumia Njia Nyengine
Jaabir bin ‘Abd-Allaah (Radhiya Allaahu
‘anhu) ameripoti kuwa Mtume (Swalla
Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
alikuwa akibadilisha njia siku ya ‘Iyd.
(imeripotiwa na al-Bukhari, 986)
Imeripotiwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa
akitoka kwa miguu, na alikuwa akiswali
bila ya adhana wala iqaamah, kisha hurudi
kwa kutumia njia nyengine tofauti.
Inasemekana kuwa njia hizi mbili zitamtolea
ushahidi siku ya Qiyaamah, kwa sababu siku
hiyo ardhi itasema juu ya kila kitu
kilichofanywa juu yake, zuri na baya. Vile
vile inasemekana kuwa imefanywa hivi
ili kuonyesha alama na utamaduni wa
Kiislam katika njia zote mbili; kutoa
ukumbusho wa Allaah; kuwavunja moyo
wanafiki na Mayahudi na kuwaogopesha
kwa wingi wa watu walio pamoja nae; kutimiza
mahitaji wa watu kwa kuwapa
fatwa, kuwasomesha na kuwawekea mifano ya
kuifuata; kuwapa sadaka wale
wanaohitajia; au kuwatembelea jamaa zake
na kukuza mahusiano yao.
Tahadhari Juu Ya Kufanya Maovu
1. Baadhi
ya watu wanadhani kuwa Uislam unatuambia kukesha na kuswali
usiku wa ‘Iyd, kwa kunakili hadiyth ya
uongo inayosema "Yeyote
atakayekesha usiku wa ‘Iyd moyo wake
hautokufa siku ya kufa moyo wake"
Hadiyth hii imeripotiwa katika isnaad
mbili moja ambayo ni dhaifu na ya pili
ni dhaifu sana. Uislam hautuambii kuutenga usiku wa
‘Iyd kwa kukesha na
kusali; hata hivyo, iwapo mtu ana tabia ya
kuamka na kusali usiku
(Qiyaam), hakuna ubaya wa kufanya hivyo
katika usiku wa ‘Iyd pia.
2. Mchanganyiko
wa wanawake na wanaume katika maeneo ya Swalah,
mitaani, n.k. Inasikitisha kuwa haya
yanatokea sio misikitini tu, bali hata
katika sehemu tukufu zaidi, al-Masjid
al-Haram [Makkah]. Wanawake
wengi, Allaah Awaongoze wanatoka wakiwa
hawajajisitiri, wamejipamba na
kujitia manukato, wanaonyesha mapambo yao, wakati kuna
mkusanyiko
mkubwa katika msikiti huo. Hatari ya hali
hii iko wazi kabisa. Kwa hiyo wale
wahusika ni lazima wapange Swalah za ‘Iyd
vizuri, kwa kuweka milango
tofauti na njia tofauti kwa wanawake na
wawacheleweshe wanaume kutoka
mpaka wanawake wawe wameshatoka.
3. Baadhi
ya watu wanajikusanya siku ya ‘Iyd kwa ajili ya kuimba na kufanya
aina nyengine za ….burudani, na hii
haikuruhusiwa.
4. Baadhi
ya watu wanashereheka katika ‘Iyd kwa sababu Ramadhaan
imemalizika na kuwa hawahitajiki tena
kufunga. Haya ni makosa, waumini
wanasherehekea ‘Iyd kwa sababu Allaah
Amewasaidia wao kumaliza mwezi
wa Swawm, sio kwa sababu ya kumalizika kwa
Swawm ambayo watu
wengine wanaichukulia kuwa ni mzigo.
Tunamuomba Allaah Azikubali ibada zetu na
toba zetu. Allaah Ampe rehma Mtume
wetu Muhammad.
No comments:
Post a Comment