Hatuna budi kumshukuru Allah kwa kutupa nguvu ya kuziendeleza kazi za jumuiya yetu ya MSATEKU.......leo tena (Jumapili,tarehe 11-11-2012)MSATEKU kupitia idara yake ya ELIMU iliwaandalia wanafunzi wenzetu wa mwaka wa kwanza (I) semina elekezi ili kufanya maisha yao mapya kwa Chuo cha Teku yawe rahisi,Tunawapongeza idara ya Elimu kwa Kuwaandalia ndugu zetu semina hiyo....chini ni baadhi ya picha hizo......
Baadhi ya vijana wa mwaka wa kwanza (I) wakifuatila semina elekezi.
Baadhi ya viongozi wa MSATEKU wakiongozwa na AMIR(MASATEKU) katika mwenye koti jeusi,kushoto ni Amir wa Idara ya Elimu yaBrother Amur......kutoka kulia ni wajumbe wa idara hiyo.Wakifuatilia kwa umakini kile kilichokuwa kinaulizwa na wajumbe.
Brother S-E-S-E-.....nae alikuwepo na makamu Amir wa kitengo cha fedha,akiwa anafanya mawasiliano ili mambo yasiharibike huku semina ikiwa inaendelea.
Ni sehemu ya MATERIALS yanayopatikana katika maktaba yetu ambayo imeanza kufanya kazi,ambapo wanajumuia wanakaribishwa kuja kujisomea materials mbalimbali,imani ya jumuiya maktaba hii kuwa kubwa na yenye kujitosheleza kwa vitabu na mambo mbalimbali ya kujifunzia.
Amir wa Jumuiya akiwa katika ofisi ya jumuiya akianda shughuli mbalimbali za Jumuiya,mara baada ya semina elekezi kuisha mchana wa leo.......pole Brother.......Allah atakulipa kwa jitihada unazofanya za kuipeleka jumuiya ya MSATEKU mbele,mbele yake ni brother Seseme akiwa anahakikisha taarifa za Blog yetu zinawafikia wanajumuiya.......
No comments:
Post a Comment