Tuesday, February 26, 2013

Msiba Mkubwa kwa jamii ya wasomi wa baadae.



 TAARIFA YA MTOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 HAYA HAPA 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012

1.0    UTANGULIZI

Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.  Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0    MTIHANI WA MAARIFA (QT)

2.1           Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2          Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).

3.0    MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012

Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.

3.1          Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa

(a)          Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67.  Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012  ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.

(b)            Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia 55.50.  Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro,  ugonjwa na vifo.

(c)             Watahiniwa wa Kujitegemea
Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 na wavulana 30,084  wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23  hawakufanya mtihani.

4.0        MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

(a)                 Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.

(b)                Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani.  Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361. 

5.0                 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
Daraja
Idadi ya Wavulana                Idadi ya  Wasichana    Jumla
I           1,073                       568                                 1,641
II          4,456                     1,997                               6,453
III        10,813                   4,613                               15,426
I-III      16,342                   7,178                               23,520
IV        64,344                  38,983                             103,327
0         120,664                120,239                            240,903

6.0        SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE
            WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5.  Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :
NAFASI           JINA LA SHULE         IDADI YA WATAHINIWA       MKOA
1                      ST. FRANCIS GIRLS                  90                              MBEYA
2                      MARIAN BOYS S.S                    75                              PWANI
3                      FEZA BOYS S.S                          69                              DAR ES SALAAM
4                     MARIAN GIRLS S.S                    88                              PWANI
5                     ROSMINI  S S                               78                               TANGA
6                    CANOSSA S.S                               66                               DAR ES SALAAM
7                    JUDE MOSHONO S S                   51                              ARUSHA
8                    ST. MARY’S  MAZINDE JUU        83                             TANGA
9                   ANWARITE GIRLS S S                   49                              KILIMANJARO
10                KIFUNGILO  GIRLS S S                 86                              TANGA
11                  FEZA GIRLS                                   49                              DAR ES SALAAM
12                  KANDOTO SAYANSI GIRLS SS  124                            KILIMANJARO
13                 DON BOSCO SEMINARY SS         43                              IRINGA
14               ST.JOSEPH MILLENIUM                 133                            DAR ES SALAAM
15              ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS       64                              KIGOMA
16              ST.JAMES SEMINARY SS                  44                             KILIMANJARO
17             MZUMBE SS                                       104                            MOROGORO
18            KIBAHA SS                                          108                             PWANI
19             NYEGEZI SEMINARY SS                    68                             MWANZA
20             TENGERU BOYS SS                             76                             ARUSHA

7.0        SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
NAFASI           JINA LA SHULE         IDADI YA WATAHINIWA    MKOA
1                     MIBUYUNI S.S                                 40                       LINDI
2                     NDAME  S.S                                     41                       UNGUJA
3                     MAMNDIMKONGO S.S                63                        PWANI
4                     CHITEKETE S.S                              57                        MTWARA
5                     MAENDELEO S.S                         103                        DAR ES SALAAM
6                     KWAMNDOLWA S.S                     89                         TANGA
7                      UNGULU S.S                                 62                         MOROGORO
8                      KIKALE S.S                                   60                         PWANI
9                      NKUMBA S.S                              152                         TANGA
10                   TONGONI S.S                                56                         TANGA


8.0           TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
               MWAKA 2012 

8.1         Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali
               inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi
               ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.  Aidha,
               shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

(i)                 Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;

(ii)               Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa
 maktaba kwa ajili ya kujisomea; na Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.

8.2            Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja
              na kufanya mambo yafuatayo:

(i)                      Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka
 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule.  Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.

(ii)                    Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.

(iii)                  Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.

(iv)           Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo
               baina ya shule na shule.

(v)            Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha
                Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za
                Sekondari zilizo katika maeneo yao.

9.0           MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA

               Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:
(a)           Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada
                wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02)            
              toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.

(b)           Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012
               bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada
              hiyo katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.

10.0             MATOKEO YA MITIHANI  YALIYOFUTWA

10.1              Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu
              Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu
             Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika
            mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa kujitegema
           ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.

Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama ifuatavyo:

S/N      AINA YA UDANGANYIFU   IDADI YA WATAHINIWA
(i)        Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti
            katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja. 04

(ii)       Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’     170

(iii)      Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.           590

(iv)      Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.         04

(v)       Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.         06


(vi)      Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa
           lengo la kufanya udanganyifu. 15

            JUMLA            789

10.2     Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti Zao

(i)                    Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali.
             Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani
             kinachosomeka:

“Written responses to any examination question which carry words, drawings or pictures connected to sex or abusive language in such a way that it becomes offensive shall consitute an examination offence and a candidate who commits such an offence shall be punished by the Council.”
Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo  yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka: 
“A candidate found to have committed an examination offence shall – (a) have his examination results nullified”

(ii)         Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti) kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza kuwavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali itaangalia hatua zaidi za kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote walioandika matusi.
Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b) cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika skripti zao hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania  kwa kipindi cha mwaka mmoja (01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.

           

8 comments:

  1. tatizo ni nini?
    1,watoto hawasomo,
    2.feki hazipatikani au
    3.walimu wamesusa?

    ReplyDelete
  2. A.W.W. Sifa ya amir awe msomi wa dini na mwenyebusara

    ReplyDelete
  3. baada ya salam, rejea qur an (shikamanen ktk dini ya Allah wala mctengane] naomba mc2gawe msateku 2najuana. MAONI, Shekh MAZIKU awe AMIR WA JUMUIA INSHAALLAH, SABABU uwelewa wa DINI ambao amejaliwa, uzoefu ktk uongozi na mambo ya HARAKATI, pia anabusara na hekma. plz plz and plz concda my opnion.

    ReplyDelete
  4. salam ghalyka shekh. keita

    ReplyDelete
  5. Asalm ghalykum!Pongez na shukurani nyingi kwa uongozi uliopita wa MSATEKU kwa kadar ya Alah alivyowajalia na kwa kadri ya uwezo wao walivyojitahidi katika kuuongoza UISLAMU na WAISLAMU wa Teofilo Kisanji University (Msateku) hi ni kwamba kwa kuwa walifaham uongozi ni dhamana, amana na hata ni JALALA kwani matizo yote na shida za kibinadamu huelekezwa kwa viongozi, kwa hili wao wameliweza Allah atawalipa malipo yalomema Inshaalah, Allah pia awaongoze katika njia iliyoyooka, awape umri ulio mrefu wa kumtumikia Alah. Pongezi za dhati pia ziende kwa uongozi ULIOTANZWA tareh 5may 2013 ukiongozwa na Al-habib shekh ABUBAKARI kama AMIRI wa MSATEKU, shekh Allah amuoggoze pia katika uongozi wake kwa maslah ya UISLAMU na WAISLAMU wa msateku.keita

    ReplyDelete
  6. si ktk busara kumsema kingozi baada ya kuchaguliwa, pia si busara kusambaza sms kwa waislamu eti kwa kuwa wewe humtaki kiongozi kwa matashi yk, pia si busara kubdilisha maana ya aya ya m,mungu kwa maslahi ya kwako rejea qur an (shikamanen ktk dini ya Allah wala mctengane]hali ya kuwa wewe ndio untka kuwagawa waislamu kwa kusambaza sms kwa waislamu.,pia si ktk uislam kuwazuia watu wasije ktk darsa duara kwani huo ni utovu wa nidhamu.km ungekuwa na busara nzr, ulitakiwa uwaite viongz na uwaeleze ttzo liliopo lkn c kusambaza sms tena kwa kutumia lg kali, kwani lg hizo hutumiwa na w,siasa na cc ni waislm.

    yawezekn kukawa na tatizo amblo nynyi mmeliona lkn approaching iliyotumika haionyeshi km kuna ttz ila ni utashi wako na misimamo yk ya kuwagawa waislam

    ReplyDelete
  7. MWANAJUMUIA MSATEKUMay 10, 2013 at 1:34 PM

    ASSALAM ALAYKUM WARAH-MATULLAHI WABARAKATUH,pongezi za dhati ziwaendee viongozi wote waliomaliza muda wao katika kuisimamia msateku, mmefanya kazi kubwa sana.Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sijawapongeza kwa yale mliyo yafanya,ALLAH atawalipa malipo yasiyo katika na awanusuru na fitina za dunia inshaallah!! hao wanaosambaza ujumbe wa kupinga uongozi mpya wanaakili kweli? na kuwataka viongozi wao na kuwafanyia kampeni dini sio siasa,hawana hoja ila ni kukosa adabu mbele za ALLAH na udhaifu wa iman na hawajui dini kabisaa,mimi ni mmoja wa wanajumuia msateku nasema akiondoka tu AMIRI aliyechaguliwa ABUBAKAR jueni mmeiua jumuia yetu na mmewafarakanisha waislam,na msihi AMIRI ABUBAKAR asiyasikilize maneno yao na asije ukathubutu kujiuzulu nafasi hiyo utasababisha mengi mabaya yajitokeze ktk jumuia yetu,ALLAH akutangulie na akukinge na fitina za wanafiki hawa wasiojua thamani yako.Nimesikiliza hutuba zako msikiti wa pambogo zinatujenga iman sana MUNGU akuzidishie elimu yenye manufaa kwa waislam inshaallah

    ReplyDelete
  8. A.ALYKM, NASHUKURU ALLAH KWA KUMALIZA SALAMA JUKUMU LA KUTEUWA UONGOZI MPYA WA MSATEKU, PIA NAPENDA KUMSHUKURU BW KATO NA BW FADHILI KWA KUSHIRIKIANA KTK KUFANIKISHA JAMBO HILO, PIA NAPENDA KUWASHUKURU WOTE HASA ILE KAMATI KWA KUUONGOZA VIZURI MPAKA TUKAMPATA KIONGOZI CHAGUO LA WANA MSATEKU KUPATIKANA, ALLAH AWAONGOZE

    ReplyDelete